REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

Baghdad atoboa Siri za Madenti wa Kike katika MWANAFACEBOOK

9:22:00 AM Add Comment







Na Franklin Naceeb-Abood (Mwana FaceBook)


Haya hayaaaa
Kama kawaida...az longer as ni New Segment. Kwa ushirikiano na My Big Boss Frankie, leo nimepita pia katika Page zetu mbali mbali za Face Book, ili kupata kile kinachotokea

Dah......okay. mule mule, yaani leo tumekutana na haya Machache ambapo kama kawaida yangu, "Mwana Facebook" nakumegea haya kwa njia ya Picha.
Drop it nw......



*********************************************************************

BAGHDAD PG KWEKA









Yeees...hii ilipatikana katika Page ya Baghdad PG Kweka kama unavyomuona Pale Juu (Sijui yuko na Shem....hata sjajua). Naona hawa ni wanafunzi....but haya wanayoyafanya...Mhhhhhhhhhhhh...Nyambaaaafu kweli kweli.
Wazazi Mpooooooo? (Dah...halafu huypo anamfunua kabisa yaani ...Duh..)




***************************************************************************


MBUKE MASANJA











Haya haya Kipunga Hichooo...Saaafi. Hii imepatikana katika Page ya Mbuke Masanja (Shemeji Yetu huyu). Unajua Ubwabwa hhuwa una nafasi kubwa sana kwa watoto kama hawa. Hapa hadi raha...ukigonga tonge kubwa, aiza utafinywa, au mmoja wenu kuangua Kilio...Hahaaaa

******************************************************************


FRANKIE JOACQIUM
















Daaaaah...aliyesema "Nani kama Mama", hakukosea. lakini Je unakubaliana na Mimi kuwa "damu ni Nzito kuliko Maji"?..Haya Bhana, My Best Friend and My Big Boss FRANKIE JOACQIUM katika page yake katupia Photo ya Mdogo wake PRISCA STEVEN, ambaye Yuko Uganda akikamua Kitabu...yaani Chuo. Soma Mdogo wetu...Tunakuombea Mengi na Tunakupenda sana
(Ila Siku Nyingine Ukienda Mwanza Mtaarifu kaka..........amekumiss sana). Safari njema Kesho. Si ndo Unarudi Uganda?.. Bro Frankie anakupenda sana . Okay?. Take Care? Be a Good Girl. Okay

DEDICATION FROM YOUR BRO.
FOREVER YOUNG- By Jay Z. (Listen to that Song whenever U miss Em. Okay?)

************************************************************************

Mi Sina Jipya Jaman ndo Nimemaliza hivyooooooooo. Kesho kama Vipi ntakupa ntakachokipata katika "MWANAFACEBOOK" ili kujua mishe zilizojiri katika facebook.










 






MWANASAYANSI WA KWANZA KWENDA MWEZINI AFARIKI DUNIA

8:14:00 AM Add Comment









Na Frank M. Joachim & DW.

Risala za rambirambi zinaendelea kutolewa kufutia kifo cha mtu wa kwanza kufika mwezini, mwana anga wa Marekani Neil Armstrong.

 Armstrong aliyekuwa na umri wa miaka 82, alifariki muda mfupi baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo. Alikuwa kamanda wa kikosi cha safari ya Apollo 11 - pamoja na mwanaanga mwengine Buzz Aldrin. 

Mamilioni ya watu duniani kote waliweza kufuatilia kwenye televisheni  mnamo mwaka wa 1969, jinsi Armstrong alivyotua mwezini, umbali wa kilometa 400,000 kutoka kwenye sayari ya dunia.

 Armstrong alisema wakati huo kwamba alichokifanya, ilikuwa ni hatua fupi kwake kama binadamu mmoja, lakini ilikuwa ni hatua ndefu mbele, kwa binadamu wote duniani. Rais Barack Obama amemsifu mwanaanga huyo kuwa ni shujaa mkubwa kabisa wa Marekani ambae kamwe hatasahaulika.

Maiti Waongezeka katika Mlipuko wa Venezuela

7:56:00 AM Add Comment




Na Franklin Naceeb-Aboud (Mwana Facebook) & DW

Kiasi ya watu 39 wamekufa nchini Venezuela baada ya mripuko kutokea katika mojawapo ya viwanda vikubwa vya mafuta nchini humo hapo jana.

Inaaminika kuwa gesi aina ya propane ilivuja na kusababisha mripuko mkubwa katika kiwanda hicho cha mafuta Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo. Wengi wa waliokufa ni walinzi wa kitaifa. 



 Watu wengine  karibu  80 walijeruhiwa katika mkasa huo. Waziri wa Nishati Rafael Ramirez amesema kumetokea madhara  makubwa katika miundi mbinu na pia katika  nyumba zilizokuwa mbele ya kiwanda hicho. Aliongeza kuwa mripuko huo uliyakumba hadi maeneo yaliyo karibu na kiwanda hicho.

 Lakini hali imerejeshwa kuwa  ya kawaida. Rais Hugo Chavez ametangaza siku tatu za maombolezi akisema mkasa huo ni msiba kwa familia yote ya Venezuela ikiwa ni pamoja na raia pamoja na jeshi.

39 Wafariki China

7:41:00 AM Add Comment




Na Frank M. Joachim & DW

Kiasi ya watu 36 wamekufa leo katika ajali mbaya baada ya lori iliyokuwa imebeba kemikali ya methanol kugongana na basi la abiria la ghorofa mbili.

 Hiyo ndiyo ajali mbaya kabisa ya barabarani kuwahi kutokea China katika kipindi cha mwaka mmoja. Magari yote mawili yaliwaka moto na ni watu watatu tu kati ya 39 waliokuwamo ndani ya basi hilo walionusurika kifo katika ajali hiyo iliyotokea mwendo wa saa nane usiku. 

Kwa mujibu wa shirika la habari la China, Xinhua, jumla ya miili 36 ilichopolewa kutoka kwenye vifusi na watatu walionusurika wakakimbizwa hospitalini. Mnamo mwezi Julai mwaka jana, moto ulizuka ndani ya basi moja lililojaa abiria kupita kiasi, na ambalo lilikuwa limebeba vifaa vinavyoweza kusababisha moto, na kuwaua abiria 41 nchini humo.

MNADA BANNER