VIONGOZI WA BARAZA LA SANAA LA TAIFA (BASATA) WAKIWA KATIKA
MKUTANO WA MAANDALIZI YA FAINALI ZA
TAIFA ZA MISS UTALII TANZANIA NA
BODI YA MISS UTALII TANZANIA 2012/2013
ZITAKAZO FANYIKA HIVI KARIBUNI.
BODI YA MISS UTALII
TANZANIA WAKIWA KATIKA KIKAO CHA PAMOJA NA VIONGOZI WA BARAZA LA UTAMADUNI
TANZANIA (BASATA) WAKIENDELEA NA KIKAO.
WAJUMBE WA BODI YA
MISS UTALII TANZANIA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA VIONGOZI WA BARAZA LA
SANAA TAIFA (BASATA) BAADA YA KIKAO CHA MAANDALIZI YA FAINALI HIZO ZA MISS
UTALII 2012/2013.
Wakati kambi ya Miss Utalii Tanzania 2012/2013 ikikaribia
kuanza katika Hotel ya Ikondolelo Jijini Dar es salaam, juzi tarehe 14.12.2012
Bodi ya Taifa ya mashindano hayo ilifanya kikao na Serikari kupitia Baraza la
Sanaa la Taifa katika ukumbi wa Baraza hilo. Katika kikao hicho ambacho kilijadili maandalizi ya fainali na mpango
mkakati wa fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania mwaka huu.
Katika kikao hicho Bodi ya Miss Utalii Tanzania iliwasilisha
taarifa ya kukamilika kwa maandalizi kwa Serikali ambapo bodi iliitaarifu
Serikali kuwa maandalizi ya fainali hizo yamekamilika kwa asilimia tisini 90%
ikiwemo katika maeneo ya kambi na mafunzo, ukumbi, Zawadi, wadhamini,Washiriki,
Nk.
Bodi ilibainisha kuwa kwamba jumla ya washiriki sitini (60)
wakiwakilisha mikoa yote ya Tanzania na Kanda maalum za vyuo vikuu watapanda jukwaani kuwania taji la Miss
Utalii Tanzania 2012/2013. Pia Bodi ilibainisha kuwa zawadi zitakazo tolewa kwa
washindi zimelenga zaidi kuwanufaisha washiriki , jamii zao na taifa. Zawadi
hizo ni pamoja na Nafasi za masomo za elimu ya juu, mikataba ya kazi ,Safari za
kushiriki mashindano ya Dunia na Kimataifa , Tuzo za heshima za kijamii,
kitalii, kitamaduni, urembo na mitindo.
Aidha Bodi ilielezea kuwa imejipanga kuzifanya fainali za
Taifa za Miss Utalii Tanzania 2012/2013 kuwa tukio kubwa la pekee Kihistoria na
kitamaduni kuwahi kufanyika nchini kabla na baada ya uhuru. Ambapo wakiwa kambini washiriki watafanya
shughuli mbalimbali za kijamii pamoja na kupata mafunzo stadi mbalimbali za
maisha , uhamasishaji na utangazaji wa elimu , utalii, utamaduni,
uwekezaji,mazingira, michezo na afya.
Nayo Serikali ilipongeza Bodi ya maandilizi ya miss utalii
Tanzania kwa mpango mkakati na maandalizi yenye kukidhi na kulenga kupromoti
utalii uhamasishaji na utangazaji wa elimu , utamaduni, uwekezaji,mazingira,
michezo na afya.Akizungumza katika mkutano huo Kaimu Katibu mtendaji wa Baraza
la sanaa la Taifda Ndugu. Malimi Mashili alipongeza mpangilio wa zawadi na tuzo
kwa washindi pamoja na washiriki ambapo tofauti na mashindano mengine ambapo
zawadi zao huwa ni mzigo kwa washiriki na wakati mwingine zisizo na manufaa kwa
jamii wala Taifa."Miss utalii
Tanzania katika kipindi cha miaka mitano tangu kuanzishwa kwake imekuwa ni fahari ya Taifa na kielelezo cha
utamaduni wa Tanzania kitaifa na kimafaifa ambapo limekuwa ndilo shindano pekee
linalo la tangaza nchi yetu kwa kushinda mataji ya Dunia na kimataifa kila
mnapo shiriki". Aidha akiahirisha mkutano huo aliihakikishia Bodi kuwa
Serikali inatambua juhudi na mchango wa waandaaji na mashindano ya miss utalii
tanzania katika kukuza utalii, utamaduni na michezo nchini na kwamba
Serikali sikuzote ipo bega kwa bega na
waandaaji wa mashindano haya katika kuhakikisha kwamba hayakwami na iko tayari
kusaidia kwa hali na mali ili yaweze
kufanyika kwa kiwango cha kimataifa.
Imetolewa na,
Mratibu Matukio,
Hamis .A. Mkongowale