WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
KUNA HILI LA KUJUA KUTOKA KWA HUYU JAMAA... SOMA HAPO..
WIKI Ijayo Itakuwa ni Chance ya Wewe kumfahamu ABDALLAH
“OXS” OKELEKY ambaye ni RAPPER, akiwakilisha Jiji la Mwanza.
Oxs ambaye ni Producer wa METRO FM 99.4 –
Mwanza, na Presenter wa Kipindi Cha RIDDIM ROCKERS kinachoruka Kila Jumamosi
katika kituo Hicho, ameanza Michakato ya Muziki Muda Mrefu na ameweza kufanya
Nyimbo Kadhaa.
Tofauti na Hilo, OXS anayefahamika kama BIG
DADY, pia amehusika kunako Collaborations Mbali mbali na wasnii Tofauti akiwemo
GODFREY TUMAINI Maarufu kama DUDU BAYA, pamoja na wengineo wengi ambao wana
jina Kubwa tu hapa Nchini Tanzania.
Kuanzia Wiki Ijayo, Mikwaju Lukuki ya Oxs,
itaanza Kuflow kunako BLACK TOUCHEZ, na kusambazwa katika Mitandao Tofauti ya
Kijamii.
Get Ready For This, na Kwa Shughuli Nyingine
kama utahitaji kumhusisha, Basi, NEXT WEEK kila kitu Kitakuwa Wazi.
ROCK CITY CHAT: WAKUBWA WA JIJI, TEGA SIKIO BOYS WAMESHUKA, SPEED YA MO MUSIC INATISHA
This week bin Wiki hii TTM tumeweza kustick
kunako jiji la Mwanza na kuona kuwa Yes, Mbadidi la Kumwaga lipo katika Mikwaju
ambayo inazidi kukita kupitia jam session na hata vipindi vingine.
Ni nafasi tamu ya Kuzihesabu zile 5 ambazo
zinafanya Byee kunako Metro Fm kwa Muda wa Wiki Nzinma, nikimaanisha Swagalinyu
za Kuanzia Jumatatu Mpaka Ijumaa
5.
HONEYA- UWE WANGU
Wiki hii katika nafasi ya tano TTM tumemnyaka
This Beautiful Lady mwenye vocali tamu linalohamasisha kukubali kazi yake. Kwa
mujibu wa Info kutoka kwake ni Kwamba hivi sasa tayari ana Package kubwa ya
Mikwaju ambayo ameshaiandaa tayari kwa kuliteka Soko la Muziki. Bibie huyu
ameshafanya Tracks za kutosha na DEEY CLASSIC kutoka revolution Sound, DONCHA
MASTER ambaye hatujui kama still yuko OVER CLASSIC, na hivi sasa anapiga
Projects nyingine na TIDDY HOTTER wa ONE LOVE FX, pamoja na LOLLIPOP wa K-
RECORDS.
Good Info ni Kwamba, Sauti yake hivi sasa
inakita Vizuri kunako Nchi ya Kenya na Cannada, baada ya kupiga Chourus tamu
akiwa na JAMAA TU FULANI, MKENYA mwenye Maskani yake CANNADA, kunao Track ya
FREEDOM ambayo Natty E, kashusha Verse Pia.
Ladies and Gentlemen, katika Nafasi ya Tano, Track
ya UWE WANGU kutka Kwa Honeya.
4.
ZIPATE TUKUJUE- WAKUBWA WAJIJI
Wakiwa bado wanazidi kukomaa na game, this time
Kutoka ROCK CITY Mwanza hapa hapa, wameshuka kutoka nafasi ya Pili mpaka nafasi
ya NNe na Track yao ZIPATE TUKUJUE.
Mpaka hivi sasa kunako Mtandao wa YOUTUBE, Video
ya Wimbo huu imeshatizamwa na watu zaidi ya Miamoja kutoka sehemu Kibao Hapa
Duniani.
Kwa mujibu wa Info za Chini Chini Tu, ni kwamba
Vichwa hivi Vilikuwa vimejichimbia kwa ajili ya kujipanga na Shows ambazo soon
, huenda zikaanza kumiminika.
3.
TEGA SIKIO- K- STAR, NCHAMA THE BEST NA BRYTONE.
BIG UP SANA Kwao watatu hawa Kwa kuzidi kuonesha
Uwezo wao wa hali ya Juu tangia wamefanikisha kuisukuma kazi hii ikiwa ni Track
yao Kwanza kabisa.
.Lakini Guud info ambazo still TTM tunazidi
kuziamini ni Kwamba Vichwa hivi vitatu, K-STAR kutoka Pasiasi, NCHAMA THE BEST
kiutoka Bugarika, na BRYTONE representing Sengerema, Vinatarajia kushusha
Tracks Nyingine ambazo zirtkuwa ni Balaa pengine kuliko hata hii iliyoko kunako
nafasi Hii ya tatu
2.
BASI NENDA- MO MUSIC
Hakuna ambaye atabishana na TTM kuwa Moja kati ya
Vijana ambao wanasauti Nzuri na Ya kujivunia Ni huyu jamaa. Off Course ni
Kwamba VIDEO yake ambayo ina wiki Moja tu ikiwa Imewekwa katika mtandao
waYOUTUBE, imetizamwa na Watu zaidi ya
1000, huku audio Ikipata Airtime kali ya kutosha kunako Media mbali mbali
Nchini Tanzania
Lakini, kama Ulikuwa Hufahamu, this Bway ni Ex-
Memba wa Kundi la wakubwa wa jiji.
Katika nafasi ya pili Kimwanza mwanza, wiki hii,
Mo Music, na Track ya BASI NENDA.
1.HAINAGA
NOMA- NATTY E
Katika nafasi Hii, wala huwa hainipi Noma, coz Mhusika Mwenyewe hanaga Noma, Track yenyewe hainaga Noma, na hata Producer aliyehusika Hanaga Noma.
Katika nafasi Hii, wala huwa hainipi Noma, coz Mhusika Mwenyewe hanaga Noma, Track yenyewe hainaga Noma, na hata Producer aliyehusika Hanaga Noma.
Ikiwa ni baada tu ya Kuachia Mbwadidiz kibao
ambazo zimempatia heshima yake, This Time amekuja Kwa Level Nyingine, na Mzuka
Mwingine.
Tofauti na hilo, Kipaji cha Mamito huyu
kimedhihirika baada ya kukatanishwa na JAMAA TU FULANI, na hatimaye kupika
Track ya Freedom Chini ya Deey Classic, na mwisho wa yote kila Kitu kikawa Byee
Ladies andGentle men, katika Nafasi ya Kwanza
Wiki hii Kutoka hapa hapa Rock City, NATTY E, HAINAGA NOMA.
2 CHAINZ KUPANDISHWA MAHAKAMANI JUMA LIJALO
MIEZI 10 liyopita Rapper 2 Chainz alikutwa na
msala wa Kukamatwa na Dawa za CODEINE ambazo mara nyingi hutumika kutengenezaa
dawa za Kulevya aina ya SIZZURP.
TTM tumezinyaka kuwa Rapper Huyo ambaye maskani
yake ni GEORGIA, Marekani, Week Ijayo atapandishwa Kizimbani ili Kesi yake hiyo
iweze Kusikilizwa na hata maamuzi kutolewa.
Aidha Info ambazo TTM tumezinyaka Pia, ni kwamba
Endapo 2 Chainz atabainika Kuwa na hatia, basi atatumikia Kifungo cha Takribani
Miaka 3 Jela.
Tofauti na kukutwa na Aina hiyo a Madawa ya
Kulevya, 2 Chainz ambaye ni Mbaya katika Collable anazopewa, aliwahi Kudakwa na
BANGI jambo ambalo linamuweka mahali pabaya.
BONGO MOVIE KUNA HILI LA KUJIFUNZA.
Ukubali ukatae, TIM TUKO MBELE Still tunakubali
sana Kila Product ya Burudani kutoka Nchini Tanzania.
SONGERA ZIGI ZIGI kwa Kitengo Chimbua Chimbua
kwa kuweza kulibaini hili na Sisi kamwe hatuwezi kuikataa Ripoti yao.
NCHI ya Kenya imekuwa ni moja kati ya Mfano
mzuri sana wa kuigwa Tangia LUPITA NYONG’O aonekane kuwa na mafanikio mazuri sana katika
tasnia ya Filamu Ulimwenguni, lakini kadri Siku zinavyozidi Kwenda, ulimwengu
wa Filamu Nchini humo unazidi kuingia katika mabadiliko mazuri na Makubwa.
TTM tumeapata nafasi ya Kucheki Kipande cha
Filamu ya PUMZI ambacho kinagharimu jumla ya Dakika 21kutoka Nchini Kenya
kikiwa kina maudhui ya Science Fiction.
Tunapozungumzia Filam za Scince Fiction,
Tunamaanisha Filam ambazo zinahusisha masuala ya Kisayansi ambayo hukushawishi
wewe mtizamaji kuamini kuwa Hilo linalofanyika hapo, ni Kweli loipo na
limetokea, ingawa huwa ni Masuala ya kibunifu.
Filamu hiyo Fupi ya Pumzi ambayo Imeongozwa na
Muongzaji Mkenya WANURI KAHIU, inazungumzia AFRIKA MASHARIKI Ijayo, Miaka 35
Baada ya Kutokea kwa Ukame wa maji ikiwa ni madhara ama Athari ya VITA KUU YA
PILI YA DUNIA.
Filamu Hii imenekana Kupendwa na wengi na Kuendana
na Uhalisia wa tamko la UMOJA WA MATAIFA (UN), kuwa Mpaka kufikia Mwaka 2030,
Kuna Uwezekano wa kuwepo kwa Uhaba wa maji Duniani kutokana na Ongezeko la
watu.
Binafsi tunadhani BONGO Moviez wanatakiwa
kutumia akili pana zaidi, kuendana na matukio makubwa ambayo hulenga Kumtokea
mwanadamu hasa katika maisha yake, tofauti na Kufikiria Ideas za kawaida tu
ambazo Ni MAPENZI kwa asilimia kubwa
Subscribe to:
Posts (Atom)