WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
PICHA : NAZINDUA KIWANDA CHA KUSINDIKA MBEGU ZA PAMBA
MBEGU NZURI SANA HIZI: Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama mbegu za pamba wakati alipofungua kiwanda cha kusindika mbegu za pamba za kisasa cha Quton kilichopo Bariadi Februari 18, 2013. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Paschal Mabiti.
NAKATA UTEPE: Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua kiwanda cha kusindika
mbegu za pamba za kisasa cha Quton
kilichopo Bariadi Februari 18, 2013. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Paschal
Mabiti na Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa kiwanda hicho, Morgan Nzwele. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
TUNATAKA ADHABU YA KIFO KWA WANAOTUUA- ALBINO RUKWA
NA HAMZA TEMBA – OFISI YA MKUU WA
MKOA RUKWA
Mwenyekiti wa chama watu wenye
ulemavu wa ngozi Tanzania “Tanzania Albino Society” (TAS) ndugu Ernest Kimaya
ameiomba serikali kupitia upya sheria ya haki ya kuishi kwa kuwapatia adhabu
kali ya kifo wale wote wanaohusika kwa vitendo vya kinyama dhidi ya albino
ikiwepo mauaji na ukataji wa viungo vyao wakiwa hai kwa kile kinachoaminika
katika imani za kishirikina kuwa ni kujipatia utajiri.
Aliyasema hayo jana akizungumza
na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ofisini kwake alipomtembelea
akiongozana na viongozi wengine wa chama hicho kumpa pongezi zake za dhati kwa
kile alichosema ni mfano wa kuigwa kwani tangu vitendo hivyo vianze hapa nchini
kwa muda wa miaka mitano iliyopita ni Mkoa wa Rukwa pekee umefanikiwa
kuwakamata wahalifu wa namna hiyo pamoja na kiungo husika kwa muda mfupi
usiozidi siku tatu.
Amesema kuwa maalbino
wamenyanyasika sana katika nchi yao kwa kukosa uhuru na amani kama watu wengine
jambo ambalo ni kinyume na haki za binadam. “Watu waliokamatwa sio wa kuachiwa
huru, wabanwe hata kuchomwa moto wataje wahusika wengine kwani mtandao wao ni
mmoja na inatia uchungu sana kwa sisi maalbino” alisema mwenyekiti huyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa alimshukuru mwenyekiti wa chama hicho na viongozi wenzake kwa kufika
Mkoani kwake kujionea hali halisi baada ya kuskika kwa matukio hayo ya kinyama
kwa Albino wenzao na pia kuwashukuru wananchi na jeshi la Polisi kwa
ushirikiano mzuri walioutoa kufanikisha watuhumiwa kutiwa mbaroni ili haki
iweze kutendeka. Mkuu huyo wa Mkoa alisema vitendo kama hivo kaamwe havitaweza
kuvumilika Mkoani kwake.
Kumekuwepo na matukio ya
kusikitisha hivi karibuni ya ukatili kwa Albino ambapo mama mlemavu wa ngozi
Maria Chambanenge (39) mkazi wa kijiji cha kavifuli katika Wilaya ya Sumbawanga
alivamiwa nyumbani kwake usiku wa manane na kukatwa mkono wake wa kushoto na
watuhumiwa ambao wameshakamatwa na jeshi la polisi na taratibu za mashitaka yao
zinaendelea.
Vilevile katika bonde la ziwa
Rukwa kata ya Milepa mtoto wa kiume mwenye ulemavu wa ngozi ‘albino” Mwigulu
Matomange Magessa mwenye umri wa miaka saba ameshambuliwa na vijana watatu
waliovaa kininja na kumkata mkono wake mmoja na kutokomea na kusikojulikana.
Polisi wanaendelea na uchunguzi kuwabaini wahusika.
Matukio yote hayo yanahusishwa na
wahalifu kutoka Mkoa jirani wa Mbeya ambapo vitendo hivi vya imani za
kishirikina vimeshamiri
KUTOKA FACEBOOK: KWELI KAKA?
Billy G. Shechambo posted to ROYAL COLLEGE OF TANZANIA - Learn
to serve the Community
Joyce Ndalichako adai Clouds FM imechangia yaliyotokea
Kidato cha Nne!
Adai walimpa 'Promo' kijana aliendika matusi na
"Bongo Flavor" katika mtihani wake wa Kidato cha Nne Mwaka jana kwa
kumfanyia interview katika moja ya vipindi vyake.
MKURUGENZI MPYA WA TTCL HUYU HAPA...
Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL jana imemteua Dkt. Kamugisha Kazaura kuwa
Afisa mtendaji mkuu wa Kampuni hiyo.
Dkt. Kazaura amechukua nafasi ya
aliyekuwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Bw. Said Amir Said ambaye amestaafu hivi
karibuni kwa mujibu wa sheria. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Kazaura alikuwa ni Afisa
mkuu wa ufundi (CTO)wa TTCLBodi ya wakurugenzi ya TTCL imewaomba wafanyakazi na
menejimenti kumpa afisa Mtendaji mkuu mpya ushirikiano wa kutosha ili kuwa na
mshikamamo wa pamoja ili kuleta ufanisi katika utendaji wa kazi.
Kwa kusisitiza Bodi imesema
“Tufanye kazi na tusonge mbele pamoja, kama timu ililyoshikamana pamoja na
iliyodhamiria kuinua utawala bora.”
Dkt. Kamugisha Kazaura
alitunukiwa shahada ya Uzamili (Masters) na Uzamivu (PhD)katika fani ya Habari
na mawasiliano ya simu katika chuo kikuu cha Waseda kilichopo Tokyo, Japani.
Subscribe to:
Posts (Atom)