WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
MISRI : Msafara wa Waziri Mkuu washambuliwa
Waziri Mkuu wa Misri Hisham Qandil, amenusurika kifo baada ya mtu mmoja
mwenye silaha kuushambulia msafara wake.
Tukio hilo lilijiri baada ya mtu mmoja aliyekuwa na silaha kuushambulia kwa risasi msafara wa Qandil, katika viunga vya mji mkuu Cairo. Kwa mujibu wa polisi ya Misri, waziri mkuu huyo hakuathirika katika shambulizi hilo.
Aidha polisi imetangaza kuwa, imefanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa wa shambulizi hilo na kwamba, tukio hilo halina uhusiano wowote na masuala ya kisiasa. Wakati huohuo serikali ya Misri na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kwa pamoja, zimelaani chokochoko na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni nchini Syria.
Serikali ya Misri na Arab League jana zililaani mashambulizi ya anga ya utawala wa Kizayuni huko Syria na kulitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua kali kuhusiana na suala hilo.
SYRIA:20 wauawa kwa mashambulizi ya magaidi
Watu 20 wameripotiwa kuuawa katika mashambulizi ya magaidi
yaliyotokea katika maeneo tofauti nchini Syria.
Mauaji hayo yamejiri katika mashambulizi ya mabomu ya
kutupwa kwa mkono yaliyotokea katika maeneo ya Kafr Nabl mkoani Idlib na
Al-Zahraa katika mkoa wa Aleppo nchini humo ambapo pia watu wengine kadhaa
wamejeruhiwa vibaya.
Kabla ya hapo Wizara ya Ulinzi ya Syria ilikuwa imetangaza
pia habari ya kuuawa kamanda mkuu katika uwanja wa ndege wa kijeshi katika
viunga vya mkoa wa Aleppo kaskazini mwa nchi hiyo. Wakati huo huo, muungano wa
wapinzani wa serikali ya Damascus, wamelaani vikali mashambulizi ya hapo jana
ya utawala haramu wa Kizayuni dhidi ya nchi hiyo.
Katika ripoti iliyosambazwa hapo jana, wapinzani hao pia
wamelaani hatua ya Israel ya kutumia vibaya matukio yanayojiri hivi sasa nchini
humo kutekeleza mashambulizi dhidi ya Syria na kwamba hatua hiyo haikubaliki.
Aidha muungano huo, umeyataja mashambulizi ya Wazayuni
nchini Syria kuwa yanayofanyika kwa malengo maalumu yaliyo nyuma ya pazia.
NIGERIA: Watu 10 wauawa mashariki mwa Nigeria
Polisi ya Nigeria imetangaza habari ya kuuliwa watu 10 huko
kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Polisi hiyo imetangaza kuwa, mauaji hayo
yalijiri hapo jana baada ya kundi moja la watu wenye silaha kukishambulia
kijiji cha Njilang katika mkoa wa Adamawa kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Watu tisa wengine wamejeruhiwa katika shambulizi hilo.
Mashambulizi ya kijiji cha Njilang ni katika mfululizo wa mashambulizi
yanayoendelea dhidi ya maeneo ya mpakani kati ya Nigeria na Cameroon. Baada ya
watu wenye silaha kutekeleza shambulio hilo, walikimbilia nchini Cameroon.
Siku ya Ijumaa Martin
Nesirky Msemaji wa Umoja wa Mataifa alitangaza kuwa, watetezi wa haki za
binaadamu wana wasiwasi mkubwa kutokana na kuendelea kwa machafuko huko
kaskazini mashariki mwa Nigeria, machafuko ambayo yamekuwa yakisababisha mauaji
na majeraha kwa raia wa kawaida.
Subscribe to:
Posts (Atom)