Riyad Farid Hijab |
Na Frank M. Joachim & DW
AMMAN, Jordan imethibitisha kuwa Waziri Mkuu wa zamani wa
Syria Riyad Hijjab aliyeasi utawala wa Rais Bashar al-Assad yuko nchini humo.
Shirika la habari la nchi hiyo, Petra, limemnukuu msemaji wa serikali, Samil
al-Mayata akisema kuwa Hijjab na familia yake waliwasili jana jioni. Mayata
alikanusha uvumi ulioenea kuwa kiongozi huyo aliingia nchini humo siku ya
Jumatatu. Msemaji wa Hijjab , Mohammed Atari amesema kuwa bosi wake alisubiri
hadi Jumanne usiku ndipo avuke mpaka kuingia Jordan kutokana na ulinzi mkali
uliowekwa kwenye eneo hilo na vikosi vya Syria. Wakati huohuo nchini Syria
mapambano ya kuwania mji wa Aleppo yanazidi kupamba moto. Hapo awali vikosi vya
serikali vilitangaza kulidhiti eneo la salahidini lakini muda mfupi baada ya
taarifa hiyo waasi walikanusha. Hii leo Iran imeandaa mkutano wa mawaziri wa
mambo ya kigeni kwa ajili ya kuujadili mzozo wa Syria. Rais Mahmoud Ahmadinejad anajaribu kuzima
mtazamo hasi wa mataifa ya magharibi na baadhi ya yale ya kiarabu dhidi ya nchi
yake kuhusu mzozo wa Syria.