WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
MAREHAMU HUGO CHAVEZ APEWA HESHIMA ZA MWISHO
HESHIMA ZA MWISHO: Mwili wa Chavez ukipitishwa katika barabara za mji mkuu Caracas
MWILI wa marehemu rais Hugo Chavez wa Venezuela , umelazwa katika kituo cha mafunzo ya
jeshi katika mji mkuu Caracas
Mapema leo mwili wa marehemu Chavez ulipitishwa kwenye umati
mkubwa wa wafuasi wake katika mitaa ya mji mkuu Caracas .
Watu wengi waliangua kilio huku wakichukua picha za kiongozi
wao aliyefariki dunia .
Mama yake na watoto wake walikusanyika mbele ya jeneza kutoa
heshma zao .
Makamu wa rais Nicolas Maduro anaongoza shughuli hiyo.
Mwili wa rais Chavez umepelekwa katika chuo cha kitaifa cha
mafunzo ya kijeshi ambapo utazikwa kesho Ijumaa.
Bwana Chavez alifariki akiwa umri wa miaka 58 baada ya
kuugua Saratani kwa zaidi ya miaka miwili.
Maelfu ya watu awali walikwenda barabarani mjini Caracas kutoa heshima zao za mwisho kwa Chavez wakifuatana
na gari lililokuwa limebeba jeneza lake
kuelekea katika chuo cha
mafuzno ya jeshi.
Mazishi ya kitaifa ya Chavez yatafanyika Ijumaa.
Mkuu wa ulinzi wa Rais alinukuliwa akisema kuwa alikuwa na
bwana Chavez alipofariki.
Generali Jose Ornella, alisema kuwa Chavez alifariki
kutokana na mshtuko wa moyo na katika siku zake za mwisho kabla ya kifo cha
ealisema angependa kuendelea kuishi.
Jeneza lake
lililokuwa limefunikwa
bendera ya nchi hiyo uliwekwa katika ukumbi ambao ni kumbukumbu ya waliopigania
uhuru wa watu wa Amerika ya Kusini
Maelfu ya watu walipanga foleni kutoa heshima zao za mwisho
kwa marehemu Chavez, wakiwemo maafisa wa serikali na viongozi wa Amerika ya
Kusini,kama Rais wa Bolivia Evo Morales na Rais wa Argentina Cristina Fernandez
de Kirchner.
ELIMU NA AFYA: WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI ITALAZYA MBEYA VIJIJINI HATARINI KUKUMBWA NA MAGONJWA YA MLIPUKO KUTOKANA NA VYOO DUNI
HATA WAO: Hivi Ndivyo Vyoo vya Walimu wa Shule hiyo ya Msingi
WANAJISAIDIA HAPA : Haya Ndiyo Matundu ya Vyoo vya Wanafunzi wa Shule Nzima
MALIWATONI : Hivi Ndivyo Vyoo vya Wanafunzi wa Shule hiyo ya Italazya
TAIFA LA KESHO : Wanafunzi wakiwa Darasani
TUNATAFUTA DIVISION 1. Wanafunzi walio katika hatari ya kukumbwa na Magonjwa ya Mlipuko wakiwa Darasani
MALIWATO MAPYA: Hii ndiyo sehemu ambayo wanafunzi hao wasadikiwa kujisaidia kwa sasa
PICHA: KAMANGA MBEYA

UKATILI KWA WANAHABARI TANZANIA: ABSALOM KIBANDA ASAFIRISHWA KWA MATIBABU ZAIDI
NDANI YA NDEGE: Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari
(2006) Limited, Absalom Kibanda, akiwa ndani ya Ndege ya Flightlink
POLE MUME WANGU : . Absalom Kibanda akiwa na mkewe ndani ya Ndege, Anjella Semaya, tayari kuanza safari ya kuelekea nchini Afrika ya Kusini kwa matibabu
TUKO PAMOJA NAYE : Baadhi ya waandishi na viongozi wa jukwaa la wahariri wakiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbi kwa ajili ya kumjulia hali.
MSAADA : Wafanyakazi wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink wakimpandisha Absalom Kibanda ndani ya Ndege.
TUMESIKITISHWA SANA : Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Hussein Bashe akizungfumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio la kutekwa kwa, Absalom Kibanda
POLE SANA : Mwenyekiti wa CHADEMA, Freema Mbowe akimjulia hali Absalom Kipanda katika Hospitali ya Taifa ya Mhumbili Dar es Salaam.
PICHA: AMANI TANZANIA

Subscribe to:
Posts (Atom)