WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
HALI YA SAJUKI YABADILIKIA JUKWAANI, JIJINI ARUSHA
Msanii wa filamu nchini,Juma Kilowoko akiwa
ameshikwa na wasanii wenzake mara baada ya kuanguka jukwaani juzi ndani ya
uwanja wa Sheikh Amri katika tamasha la wasanii wa muziki wa kizazi kipya na
wale wa filamu.
Msanii huyo akitafakari kwa kina mara baada ya
kuanguka chini ya jukwaa huku wenzake wakimpa pole.
*********************************************************
Msanii wa filamu nchini,Juma Kilowoko akiwa
ameshikiliwa na wenzake wakimshusha chini ya jukwaa mara baada ya kuanguka
alipopewa nafai ya kuwasalimia mashabiki wake
Na: Mahmoud Ahmad,Arusha
HALI ya msanii wa filamu nchini,Juma Said
Kilowoko maarufu kama Sajuki imeelezwa si ya kuridhisha mara baada ya
msanii huyo juzi kuanguka jukwaani mara baada ya kuishiwa na nguvu wakati
alipopewa kipaza sauti kuwasalimia mashabiki waliofurika kumtizama.
Tukio hilo lilitokea juzi jumapili katika
tamasha la wasanii wa filamu na wale wa muziki wa kizazi kipya lililofanyika
ndani ya uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid wakati msanii huyo
alipopandishwa jukwaani kuwasalimia mashabiki wake.
Mara baada ya msanii huyo kupandishwa jukwaani
alipewa kipaza sauti ili aweze kuwasalimia mashabiki wake lakini katika hali ya
kawaida alifanikiwa kutamka neno moja tu”ahhh” na kisha kudondoka chini ya
jukwaa lakini kabla ya kutua chini alidakwa na wasanii waliokuwa pembeni yake.
Hatahivyo,wasanii hao walimkalisha chini ya
jukwaa hilo ili aweze kupumzika na kisha baada ya muda mfupi walimshusha chini
ya jukwaaa hilo ili aweze kupata muda wa kupumzika zaidi.
Akihojiwa na gazeti hili muda mfupi mara baada
ya kushuka jukwaani Sajuki kwa sauti ya upole alisema kwamba hali yake kiafya
si nzuri kwa kuwa hana nguvu na anahitaji matibabu zaidi.
"Kaka hali yangu si nzuri kabisa naumwa sana
sijisikii vizuri”
alisema Sajuki huku akionekana mnyonge zaidi
Hata hivyo,baadhi ya mashabiki waliokuwa
wamefurika uwanjani hapo walionyeshwa kustushwa na hali ya msanii huyo huku
wengine wakiwatupia lawama nzito baadhi ya wasanii wa filamu nchini
walioambatana na msanii huyo kwa madai kwamba wanamtumia ili wapate pesa ilhali
mwenzao ni mgonjwa.
Wakihojiwa kwa nyakati tofauti mashabiki hao kwa
jazba walisema kwamba msanii huyo alipaswa kupewa muda mwingi wa kupumzika
kuliko kuambatana na wenzake mikoani kwani hali hiyo inamchosha zaidi.
“Hawa watu wa Bongo movie ni watu wa ajabu sana
huyu mtu anaumwa sana sisi tunashangaa wanaambatana na mtu mgonjwa mikoani
wampe muda apumzike na si kumtumia kwa kupata pesa”
alisikika shabiki mmoja
akiongea kwa jazba
CHADEMA WAKO TAYARI KUMSHINIKIZA RAIS KIKWETE...
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe
Na Mwandishi wa TANZANIA DAIMA
Katika kikao hicho, mbali na ajenda nyingine, wajumbe
walipokea na kujadili taarifa ya utekelezaji kutokana na maazimio ya kikao cha
dharura kilichokutana Septemba 9, mwaka huu.
Miongoni mwa maazimio hayo, ilikuwa na kupata
majibu ya utekelezaji wa madai yao katika barua rasmi waliyomwandikia Rais
Kikwete kupitia kwa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.
Baadhi ya masuala hayo ambayo yaliazimiwa ni
kuwataka Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, Mkuu wa Jeshi la
Polisi, Inspekta Jenerali wa Polisi Said Mwema, Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la
Polisi, Kamishna Paul Chagonja, na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine
Shilogile wawajibike kwa kujiuzulu nafasi zao au wafukuzwe kazi.
MHE. LOWASA AFUNGUA JOSHO LA KISASA...MONDULI
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge
wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha
Monduli juu,Mkoani Arusha wakati alipokuwa akiwasili kijijini hapo kwa ajili ya
shughuli ya uzinduzi wa josho la kisasa la Mifugo katika kijiji cha Mfereji
Monduli juu
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikaribishwa kwenye kijiji cha Mfereji Monduli juu,wakati alipokuwa akiwasili kijijini hapo kwa ajili ya shughuli ya uzinduzi wa josho la kisasa la Mifugo
Waziri Mkuu Mstaafu na
Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akifunua kitambaa kwenye jiwe la
msingi kuashiria uzinduzi wa josho la kisasa la Mifugo,lililoko katika
Kijiji cha Mfereji,Monduli Juu
Wakazi wa kijiji cha
Mfereji,Monduli juu wakimsikiliza Mh. Lowassa (hayupo pichani)
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikaribishwa kwenye kijiji cha Mfereji Monduli juu,wakati alipokuwa akiwasili kijijini hapo kwa ajili ya shughuli ya uzinduzi wa josho la kisasa la Mifugo
Waziri Mkuu Mstaafu na
Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na Wananchi wa Kijiji
cha Mfereji,Monduli Juu,mara baada ya kuzindua josho la kisasa la
Mifugo
Subscribe to:
Posts (Atom)