Na Nathaniel Limu., SINGIDA
Jeshi la polisi mkoa
wa Singida linamshikilia mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya
sekondari ya Chief Senge mjini Singida Ibrahimu Saidi (17), kwa tuhuma ya
kumwingilia kimwilia kinyume na maumbile
(kumlawiti) mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka minne (jina tunalo).
Kamanda mpya wa jeshi
la polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela, amesema tukio hilo la kusikitisha limetokea Aprili 11 mwaka
huu saa 11.30 jioni katika mtaa wa Majengo manispaa ya Singida.
Amesema mtuhumiwa ambaye ni mkazi wa kijiji cha Mtamaa
manispaa ya Singida, amepanga nyumba moja na wazazi wa mwaathirika/mlalamikaji.
Kamanda Kamwela amesema mtoto aliyefanyiwa kitendo hicho cha
kinyama alikuwa na mazoea ya kuingia chumbani kwa manafunzi huyo na hakukuwa na
matatizo.
Amesema siku ya tukio, kama
kawaida alipomwona mwanafunzi anaingia chumbani kwake, mtoto huyo naye
alimfuata na kuingia chumbani humo.
Kamwela amesema mtoto huyo baada ya kuingia chumbani kwa
mwanafunzi, mwanafunzi huyo alitumia fursa hiyo kumfanyia kitendo hicho na
kumsababishia maumivu makali.
Amesema hivi sasa
wanakamilisha uchunguzi ili waweze kumfikisha mahakamani mwanafunzi huyo ili
kwenda kujibu shitaka linalomkabili.
Kwa upande wake mama mzazi wa mtoto huyo Agnes Paulo,
amesema siku ya tukio akiwa amepumuzika na wapangaji wengine, alimwona mtoto
wake akitokea chumba cha mwanafunzi huko akilia kwa uchungu mkubwa.
“Nilipomuuliza, aliniambia kuwa Ibarahimu amemfanyia kitendo
kibaya huku akionyesha kwa kidole sehemu yake ya siri ya nyuma.Baada ya
kumchunguza,niliona damu zikimtoka kwenye hiyo sehemu ya siri”,alisema kwa
masikitiko.