WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
PICHA: DAVIDO NDANI YA SKENDO NZITO
IKO HIVI:
Mkali wa DAMI DURO toka pande za OBINA LAND, namaanisha Nigeria, DAVIDO yumo ndani ya Wakati Mgumu baada ya Picha zake alizopiga na Binti mmoja Kitandani kwake kusambaa kwa kasi ya Ajabu katika Mitandao Mbali mbali.
DAVIDO ANASEMAJE:
Kwa Mujibu wa Taarifa ambazo ni rasmi, inasemekana kuwa Davido amezikana Picha hizo huku akisisitiza kuwa, Binti huyo ambaye hata yeye hamfahamu, aliingia katika Chumba chake cha kulala baada ya kuusahau mlango wake wazi, na hatimaye kufanikiwa kupiga Picha hizo pasipo yeye kujua.
JOMBAAAAAKE HUYO DADA!!!!!
HE: MENEJA MASOKO WA STAR TIMES KORTIN
MENEJA Masoko wa Kampuni ya ving’amuzi ya Startimes jijini
dar es salaam David Kisaka (37) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala,
kujibu shtaka la kujipatia vitu kwa njia ya udanganyifu.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Nassoro Katuga alidai
mahakamani kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Januari 5, mwaka huu eneo la
Akiba, Wilaya ya Ilala.
Katuga alidai siku hiyo ya tukio katika eneo hilo mshtakiwa
kwa njia ya udanganyifu alijipatia ving’amuzi 110 na Antena 30 za StarTimes
vikiwa na thamani ya Sh8.4 milioni mali ya Jonathan Mkanaka.
Mshtakiwa alikana shtaka na hakimu Joyce Minde aliahirisha
kesi hiyo hadi Aprili 22 mwaka huu itakapotajwa tena. Mshtakiwa yupo nje ya
dhamana baada ya kupata wadhamini wawili wa kuamina ambao walisaini bondi ya
Sh6 milioni.
SAFARI YA SOUTH AFRICA : DOGO JANJA...YAMEKUWA HAYA?
Baada ya taarifa kuenea kuhusu uwepo wa msanii Dogo Janja
nchini Afrika Kusini kwa show alizopata zilizofanyika ndani ya wiki tatu,
Uongozi wa shule anayosoma ya Makongo Sekondari, umetoa taarifa kuhusu mwenendo
wake pamoja na matokeo aliyopata ya kidato cha pili.
Michael Alfred Mbaula ambae ni Afisa taaluma amesema
“mahudhurio ya Dogo Janja darasani yalikua mazuri na alikua anashirikiana
vizuri na wenzake kipindi kilichopita ila mara yake ya mwisho kuingia darasani
ni novemba 2012, na kwa sasa atalazimika kurudia kidato cha pili kwa sababu
amefeli kwa wastani mdogo ambao usingemruhusu kuendelea na kidato cha tatu”
Kuhusu kauli ya Dogo Janja kwamba juzi alipokwenda Afrika
Kusini alikua ameomba ruhusa ya wiki mbili shuleni, Mbaula amesema “sio kweli
kwamba aliomba ruhusa na wala ofisi haina taarifa japo shule haina tatizo
akitoa taarifa hata katikati ya masomo iwapo anatakiwa kufanya shughuli za
mziki kwa sababu Makongo ni shule ya vipaji, kuomba ruhusa ya wiki moja au
mbili ambazo alikua akiziomba mwaka uliopita ndani ya mwezi mmoja ni sahihi ila
kukaa miezi mitatu bila kuja shule ndio tatizo”
Mbaula amesema “Dogo Janja amefeli kidato cha pili kwa
kupata wastani wa 27 ambapo alifanya vibaya sana kwenye hesabu kwa kupata
sifuri, Civics alipata 27, historia 33, Jiografia 22, Kiswahili 46, Kiiingereza
42, Phisics 20, Chemistry 30, Biology 27, Commerce 8, Bookkeeping 11 hivyo ni
lazima arudie darasa kitu ambacho anaweza kukifanya hapahapa Makongo”
KIMBEMBE NCHINI SYRIA : WANAFUNZI 15 WAUAWA
DAMASCUS, Syria.
Wanafunzi wasiopungua 15 wameuwawa kufuatia shambulizi la
waasi dhidi ya chuo kikuu cha Damascus nchini Syria.
Shirika la habari la
serikali limesema wanafunzi hao walikufa wakati makombora yalipopiga mkahawa
katika kitivo cha usanifu majengo kwenye chuo kikuu hicho.
Chama cha kitaifa
cha wanafunzi wa vyuo vikuu kimelaani vikali mauaji hayo kikiyataja kuwa
"shambulizi la uoga la kigaidi." Wakati huo huo, Uturuki imekanusha
ripoti kwamba imewarudisha nyumbani mamia ya wakimbizi wa Syria kufuatia
mapigano kwenye kambi moja ya mpakani.
HALI YA MANDELA: NELSON MANDELA ANAENDELEA NA MATIBABU
Madaktari wanasema Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson
Mandela, anaendelea kupata matibabu baada ya kulazwa hospitalini kutokana na
maradhi ya mapafu.
Mshindi huyo wa zamani wa tuzo ya amani ya Nobel alipelekwa
hospitalini muda mfupi kabla saa sita usiku siku ya Jumatano. Ofisi ya Rais wa
sasa wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, imetoa taarifa ikisema kiongozi huyo
aliyepinga utawala wa ubaguzi wa rangi, mwenye umri wa miaka 94, anapata
matibabu bora kabisa kadri inavyowezekana.
Rais Zuma amewataka Waafrika Kusini
wasiwe na wasiwasi na wamuombee Madiba. Serikali ya Afrika Kusini imelaumiwa
kwa kutotoa taarifa za kina kuhusu hali ya afya ya Mandela.
Subscribe to:
Posts (Atom)