WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
FROM MY FACEBOOK PAGE : HII Minato ya Wiki hii...Duuuh
Hahahahahaaaaa.....Usinirenge, but...oooooh My God, hiyo ishara unafahamu ni ya nini?, au ulitia Swagg tu?..Haya bhana
Kama wewe ni Mtoto wa Kiume na Utotoni hujagusa kitu hiki, basi we ulikuwa wa kishua na Geti kali kinoma....Ilikuwa ni balaaa enzi zangu wakati nafukuzia Foward pale kati, nilikuwa naua kinoma noma
Haya bhana....wewe ndo Mweko Mwenyewe....sijapata kukuona ukiwa ndani ya Mkato huo aisee...
What a guuuuud Pouz, ingawa sjafahamu ilikuwa Wapi.. Thats my Beautiful Girl, Jamila on the Left Side alongside Dora Rodrick...I like dem smiles
Yah...yah...yah..Tru dat. Tufanye Magumashi, Mbwembwe, Michakato, Mishe na kila aina ya Swaggz, but when it comez to church...aaaah...jamani, lazima tumkumbuke Mwenyezi Mungu... Thats my Young Sister Ashy Racka
KALAMU YA NANDONDE WIKI HII : MWANAMKE ATANDIKWA MIJAREDI MPAKA KUTOLEWA JICHO na MUME WAKE
Na Ahmad James Nandonde, MUSOMA
Mwanamke mmoja Christina Fabian mwenye umri wa miaka (27)
ametandikwa na mijaredi na anayedaiwa kuwa mmewake maginga kisiri na kupelekea
kutolewa jicho moja la upande wa kulia
Akizungumzia tukio hilo mbele ya waandishi wa habari mapema
leo hii mwanamke kuyo amesema January mosi aliondoka nyumbani kwake anapoishi
katika kijiji cha baranga wilayani tarime kwa lengo la kwenda kumwogesha mama
mkwe anayeishi katika kijiji hicho ambaye ni mgonjwa na aliporudi ndipo
alikutana na adha ya kipigo kutoka kwa mume wake
Amesema aliporudi nyumbani majira ya jioni ya siku hiyo
alimkuta mume wake amesharudi nyumbani na kumuuliza sababu za kuchelewa
nyumbani akiwa anamjibu kilichopelekea kuchelewa kurudi ndipo akaanza kumchapa
sehem mbalimbali za mwili kwa kutumia mjeredi ndipo alipofikia mpaka kwenye
jicho la kulia
Aliendelea kusema baaada ya kuona amempasua jicho alimuacha
na asubuhi yake alimchukua na kumpeleka hospitali ya mkoa wa mara kwa ajili ya
matibabu lakini walishindwa kumtibu hadi atakapo peleka pf3 kutoka polisi ndipo
atibiwe
Hata hivyo wakiwa njiani kwenda polisi mume wake alimwonya
kuwa asiseme kama yeye ndiye aliyempiga na aseme wamevamiwa na majambazi na
kupelekea Bi Christina kusema hivyo walipofika polisi
Akizungumzia tukio hilo mkurugenzi wa shirika la kutetea
haki za wanawake na watoto la ABC Foundation Bw. Robert Moro amesema jamii
haina budi kubadilika kutokana na kujichukulia uamuzi wa kupiga katika suala
ambalo linaweza kuzungumzika.
MARA MILK WAINGIA HASARA YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 8
Na Ahmad James Nandonde, MUSOMA
KIWANDA CHA MAZIWA CHA MARA (MARA MILK) MUSOMA KIMEPATA
HASARA
ZAIDI YA SHILLINGI MILIONI 8 ILIYOSABABISHWA NA ITILAFU YA
UMEME ILIYOTOKEA JANUARI 9 MWAKA HUU.
AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE LEO HII
MKURUGENZI MTENDAJI WA KIWANDA HICHO JAMES MATHAYO AMESEMA KUWA KIWANDA HICHO
KIMESIMAMA KWA MUDA WA SIKU MBILI KUTOKANA NA UHARIBIFU WA BAADHI YA VIFAA VYA
KIWANDA HICHO
AMESEMA KUWA BAADA YA ITILAFU YA UMEME KUTOKEA VIFAA VIWILI
VYA MOTO VILIUNGUA AMBAVYO ALIVITAJA KUWA NI HEATER ELEMENT YENYE GHARAMA YA
SHILINGI 3.6 NA PAMPU YAKUPOOZA MAJI CHILLER MACHINE YENYE THAMANI YA SHILINGI
MILLIONI 1.2. NA KWAMBA VINAPATIKANA NCHI JIRANI YA KENYA NAITAWALAZIMU
KUVINUNUA.
NAYE KAIMU MENEJA WA KIWANDA HICHO AMBAYE PIA NI PLAN
ENGENEER WA TANESCO MKOA WA MARA AMEKIRI KUWEPO KWA TATIZO HILO NA AMESEMA KUWA
WANATAMBUA MCHANGO WA KIWANDA HICHO KWA SHIRIKA LA UMEME MKOANI HUMO NA WAMEOMBA
RADHI KWA USUMBUFU HUO NA KWAMBA WANAENDELEA KULITAFUTIA UFUMBUZI.
AMESEMA KUWA ITILAFU HIYO IMETOKEA KUTOKANA NA KUANGUKA KWA
TRANSFOMA INAYOHUDUMIA KIWANDA HICHO NA TAYARI WAMEKWISHA BADILISHA NA KUWEKA
TRANSFOMA NYINGINE.
KIWANDA CHA MAZIWA MARA MILK KINAZALISHA MAZIWA YA MTINDI,
YOGATI, NA MAJI YA KUNYWA AINA YA SUPER WATER.
CHEMUNDUGWAO : "Asilimia 95 ya Wasanii wa Filamu, Hawajitambui "
MWANAMUZIKI mahiri wa muziki wa asili hapa nchini, Che
Mugundugwao amewaeleza wasanii wa filamu kuwa wanakabiliwa na tatizo kubwa la
kutojitambua.
Amesema kutojitambua huko kunapelekea wasanii kuwa chachu ya
mauzo ya magazeti ya udaku kutokana na skendo zao.
“Nadhani hawajui hilo lakini kama wanajua basi hawapo sawa
kiakili, jambo litakalozidi kuifanya tasnia ya filamu kukosa nidhamu na
kuonekana kama fani ya wahuni”, alisema Chemundugwao.
NA SALUTI 5
ALIYPIGA PICHA NA LEMA, MIAKA MINNE JELA
Na: Daniel Mjema-Moshi
MTU aliyepiga picha na Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema
akiwa amevalia sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), amehukumiwa
kifungo cha miaka minne jela. Abubakari Kikulu (29), alipiga picha na mbunge
huyo Desemba 23 mwaka jana, baada ya Lema kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara
eneo la Mererani, ikiwa ni sehemu ya mikutano aliyoifanya kutokana na Mahakama
ya Rufani Tanzania kumrejeshea ubunge wake.
Mbali na kupiga picha hiyo na Lema pamoja na Mbunge wa
Arumeru Mashariki Joshua Nassari, kijana huyo alionekana katika picha hiyo
akionyesha vidole viwili, ambayo ni alama ya Chadema.
Hata hivyo, baada ya picha hiyo, JWTZ lilimtilia shaka
kijana huyo na kutangaza rasmi kumsaka, ili lijiridhishe kama ni mmoja wa
wanajeshi wake.
Baada ya kumsaka kwa takriban siku 12, kijana huyo
alikamatwa Januari 13, katika Mji wa Bomang’ombe wilayani Hai na baada ya
kupekuliwa alikutwa na sare hizo.
Jana, Kikulu alifikishwa mahakamani mjini Moshi, akiwa chini
ya ulinzi wa polisi na kusomewa mashtaka mawili, ambayo yote alikiri kuyafanya
kama ilivyodaiwa mahakamani.
Baada ya kukiri kosa hilo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama
ya Mkoa wa Kilimanjaro, alimhukumu kifungo cha miaka minne jela, ili iwe
fundisho wa wakosaji wengine wa aina hiyo.
Kabla ya hukumu hiyo, Wakili wa Serikali, Ignas Mwinuka
alimsomea mshtakiwa huyo mashitaka yake mawili, likiwamo la kujifanya Ofisa wa
Jeshi, wakati akijua ni uongo.
Wakili huyo alidai mahakamani kuwa Januari 3, mwaka huu
katika eneo la Bomang’ombe wilayani Hai, mtuhumiwa huyo alijitambulisha kama
mtumishi wa umma.
Katika shtaka la pili, wakili huyo alidai siku hiyo hiyo
katika Mtaa wa Msikitini, eneo hilo la Bomang’ombe, mtuhumiwa alipatikana na
sare za JWTZ kinyume cha sheria.
Sare hizo ni pamoja na suruali moja, mashati mawili na kofia
mbili, vyote vikiwa na alama za Jeshi la Wananchi wa Tanzania la Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baada ya Hakimu Kobelo kumuuliza mshtakiwa kama ni kweli
alitenda makosa anayoshitakiwa, mshtakiwa huyo alikiri makosa yake katika hali
ambayo haikutarajiwa.
Kutokana na kukiri kwake makosa hayo, Hakimu Kobelo
alimhukumu kifungo cha miaka miwili kwa kosa la kwanza la kujifanya Ofisa wa
JWTZ na miaka mingine miwili kwa kosa la pili.
Hata hivyo, Hakimu Kobelo alisema kuwa kwa kuwa adhabu hizo
zinakwenda kwa pamoja (concurrent), mshtakiwa huyo atatumikia kifungo cha miaka
miwili jela.
Kwa mujibu wa hakimu huyo, kosa alilolifanya mtuhumiwa huyo
ni baya na linastahili adhabu kali, ili iwe fundisho kwa watu wengine
wanaotumia vibaya sare za majeshi nchini.
Subscribe to:
Posts (Atom)