WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
SUMATRA - MBEYA :HAKUNA LESENI KWA MAGARI YANAYOBEBA ABIRIA WASIOZIDI 14
Mamlaka ya
Uthibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na majini( Sumatra) Mkoani Mbeya
imesitisha utoaji wa leseni ya kubeba
abiria wa kawaida kwa waombaji wapya
wenye magari yenye uwezo wa kubeba abiria
wasio zidi 14.
Aidha Mamlaka hiyo imesema kuwa endapo wamiliki hao
wa magari hayo watahitaji kutoa huduma kwa jamii mamlaka hiyo itatoa leseni kwa ajili ya kubeba watalii tu .
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Mbeya na Kamanda wa Polisi
Mkoani hapa Ndugu Diwani Athumani wakati akizungumza na madereva wa mabasi
madogo yaendayo Mji mdogo wa Tunduma Wilayani
kufuatia kuwepo kwa mgomo uliodumu kwa miezi 3 sasa ambao umefanywa na madereva hao kwa kuto
safirisa abiria waendao Tunduma.
Mgomo huo wa
madereva hao umesababishwa na baadhi ya wamiliki wa magari madogo aina ya(
Noah) ambayo yamekuwa yakifanya shughuli ya kubeba abiria toka Mbeya hadi
Tunduma hali iliyo zua mgogoro mkubwa baina ya wamiliki wa gari hizo Ndogo
pamoja na madereva wa Costa ambao ndio wenye leseni za kusafirisha abiria Toka Mbeya hadi Tunduma.
Awali wakati akizungumzana madereva hao Kamanda Diwani
amewataka mara moja watu wanaofanya biashara hiyo kuacha mara moja kwani sheria
itachukua mkondo wake.
Amesema sababu
kubwa ya kusitisa huduma inayo tolewa na magari hayo madogo ni kuzuia majanga
ambayo yanaweza kutokea kwani gari hizo hazina madirisha makubwa pamoja na
milango yake kuwa midogo ambayo na haina milango ya dharura endapo kunaweza
kutokea tatizo lolote.
Kufuatia hali hiyo Kamanda Diwani amewataka madereva
costa ambao wamekuwa wakitoa huduma hiyo kwa muda mrefu kuachana na mgomo huo badala yake waendelee kutoa
huduma kwa wananchi kama ilivyo kuwa
awali.
MBEYA YETU
PICHA: HIYO TUK-TUK IKO POA BHANA
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli, Mh Edward Lowassa
amekabidhi pikipiki nne za miguu mitatu
maarufu kama majaji za kubebea mizigo
zenye thamani ya kiasi cha
shilingi millioni 50 kwa umoja wa vijana wilaya ya Monduli, ili kusaidia
vijana kukabiliana na tatizo la Ajira.Pichani Mh Lowassa akikabidhi pikipiki
hizo kwa mmoja wa viongozi wa matawi ya vijana wilayani hapo, yumbani kwake
Ngarash Monduli.
DK SHEIN : TUTAMTAFUTA MUUAJI MPAKA TUMPATE
RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, amepokea kwa mshtuko
mauaji ya Padri Evaristus Mushi na kutoa pole kwa waumini, ndugu jamaa, marafiki na wananchi
wote wa Zanzibar kufuatia kifo hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mhe. Mohamed
Aboud ameeleza hayo jana, Jumatatu, Februari 18, 2013 na kusisitiza kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa
kushirikiana na Jeshi la Polisi itawasaka hadi kuwatia mikononi na hatimaye
kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote waliohusika na mauaji hayo.
Waziri Aboud ameyaeleza hayo wakati alipozungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake Vuga, kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kufuatia mauaji
ya Padri Evaristus Mushi wa Kanisa
Katoliki Zanzibar Parokia ya Mtakatifu
ST.Joseph, Shangani.
Hapo jana Dkt. Shein alikutana na Askofu Augustino Shao wa
Kanisa Katoliki, Jimbo la Zanzibar, huko katika Ikulu Ndogo Migombani,
Zanzibar na kueleza masikitiko yake
kutokana na mauaji hayo ya Padri Mushi wa Kanisa Katoliki la Zanzibar, na
kuelezea haja ya kuwepo kwa uvumilivu katika kipindi hichi cha msiba.
Katika mazungumzo na waandishi wa habari, Waziri Aboud alisema kuwa Serikali imejipanga
vizuri kupitia vyombo vyake vya ulinzi
na usalama ili kuhakikisha kuwa watu wote waliohusika na mauaji hayo
wanakamatwa mara moja .
“Kutokana na jiografia ya Zanzibar,Tunaelewa kwamba zipo
sehemu katika kisiwa cha Zanzibar ambazo wahalifu wanaweza kuzitumia, hivyo
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo husika vitaziba mianya yote ili
kupambana na uhalifu “, alisema Aboud.
Alisema matendo ya uhalifu yanafanywa katika mazingira ya
usiri mkubwa kwa hivyo ili wahalifu hao wakamatwe wananchi hawana budi kutoa
mashirikiano kwa Jeshi la Polisi pale
wanapohitajika.
Akijibu suali la Mwandishi, Mhe.Aboud alikanusha taarifa
zilizozagaa mitaani za kuwepo silaha nyingi mikononi mwa watu wasiohusika na
kuwataka wananchi kuondoa hofu.
Sambamba na hayo, Mhe. Aboud amewataka viongozi wa dini
mbali mbali pamoja na waumini wa dini
zote hapa Zanzibar kuwa wastamilivu
katika kipindi hiki kigumu cha maombolezi.
Aidha, Waziri Aboud alisisitiza haja ya kuwepo uvumilivu kwa
waumini wa dini zote ili kuirejesha Zanzibar katika historia yake ya kutokuwa
na migongano ya kidini.
MWANAFUNZI AJITEKETEZA KWA MOTO
Na John Banda, Dodoma
Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Sekondari
Nzuguni iliyopo manispaa ya Dodoma amekufa kwa kujichoma moto baada ya Mjomba
wake kumchapa viboko kutokana na kosa la kutomsaidia Bibi yake kuosha vyombo.
Tukio la kifo cha mwanafunzi huyo lilitokea jana jumapili
ambapo saa 11 jioni katika hospital Rufaa ya General Dodoma baada ya kulazwa
kwa masaa kadhaa
Samwel alisema mama huyo alimjibu kuwa Katherine alipofika
alitoka na hajui alipoelekea ndipo alipomsubili mpaka aliporudi akamuuliza
kwamba kwanini alimuacha Bibi yake afanye kazi wakati anajua haoni vizuri ndipo
akamua kukata fimbo na kuanza kumchapa alipotosheka akamuacha baada ya muda
akiwa nyumba jirani alisikia kelele nyumbani.
''ndugu yangu nilikuta mjomba anaungua mwili mzima kuanzia
kichwani tuliposaidia na kumpeleka hospital mwili wote haukuwa na kazi bali
moyo tu ndiyo ulikuwa ukidunda pekee na jana jumapili saa 11 jioni alikata roho
kwa weli ameniuma sana maana ni kama mdogo wangu maana mama yake alimuacha
akiwa mdogo sana'', alisema Samwel
Kwa upande wa Wanafunzi wenzake waliofika kuomboleza
nyumbani hapo walisema Marehemu alikuwa akilalamika mara kwa mara kuwa alikuwa
akiteseka sana nyumbani kiasi cha kila siku kupewa adhabu za vipigo na mjomba
wake huku akitaka fedha kwa Babu yake za kunulia vifaa vya shule na mahitaji
mengine kama mtoto wa kike alikuwa anachapwa pia.
Wanafunzi hao Desleria Lupembe, Elika Zabron, Maria Paul na
Anastadhia Boniface Wote wa kidato cha pili Nzuguni walisema kwa siku
zilivyokuwa zinazidi kusogea karibu na kifo chake walikuwa wakimshangaa mwenzao
huyo.
''Mara kwa mara alikuwa akituambia wakati wowote atakufa
hivyo tumpe picha zetu ili awe anatuangalia na sisi hapa unayetuona tulishampa
zetu, lakini alhamis akawa serios sana akasema mambo yamezidi hata jumatatu
hatakuja shule na hatutaonana kwasababu siku hiyo alinyimwa hela na Babu yake
mzee Samwel pamoja na kuchapwa sana huku akiambiwa amfuate mama yake'', alisema
Maria paul [15]
Nae Bibi wa marehemu Juliana Samwel akizungumzia tukio hilo
alisema baada ya kuchapwa na mjomba wake Kathe alichukua mafuta ya taa na
kujimwagia mwili mzima na mengine akayanywa kisha akijiwasha na njiti ya
kiberiti akawaka mwili mzima kiasi cha yeye kushindwa kumsaidia.
mwanangu mtoto aliungua karibu mwili mzima maana alikuwa
amejiviringisha kanga toka chini mpaka juu nilipiga kelele majirani wakaja
kuzima ule moto na kumbe alishaungua sana hata ngozi ilikuwa ikijichubua
yenyewe, mzee Samwel angekueleza mengi lakini kaenda hospital kuuhifadhi mwili
maana mama ya mrehema ndiyo leo anatoka Dar hivyo mazishi ni kesho mapema,
kuhusu kifo sina cha kufanya imetokea imetokea nitafanyeje'', alisema. mama
huyo wa umri kati ya 50/55
Kwa upande wa majirani walisema tukio hilo lilikuwa la
kutisha na si la kawaida kuwahi kutokea imeonyesha watoto wa sasa siyo wa
kunyanyaswa hovyo, wakatoa ushauri kuwa kila mwenye mtoto akae na mwanae
asimuamini mtu ndiyo sababu ya watoto wengi hasa wa kike kuharibikawa kutokana
na kukosa uangalizi.
Subscribe to:
Posts (Atom)