Mkuu Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist
Ndikilo akitoa taarifa ya mkoa kuhusu kanusho la kuwepo kwa mgonjwa wa Ebola
wilayani Sengerema
|
Na G.SENGO BLOG, Mwanza
TAARIFA
zinazosambazwa kuwa kuna mgonjwa wa Ebola kagundulika wilayani Sengerema mkoani
Mwanza, si za kweli.
Akizungumza na waandishi wa habari
hii leo jijini Mwanza, Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza Dr. Kengia amesema
utafiti wa awali kabla ya majibu kamili ya vipimo unatosha kujidhihirisha kuwa
mgonjwa aliyedaiwa kufariki dunia hivi majuzi Salome Richard (17) siyo kweli
kwamba amefariki kwa Ebola.
Hata hivyo kulikuwa na uchukuaji wa vipimo vya awali ambapo, Majibu ya Vipimo vya awali yamepatikana tarehe 19/10/2014 saa 3:00 asubuhi
VIPIMO WALIVYOPIMA
1. Dengue fever
2. Chikungunya Virus
Majibu ya vipimo hivyo walionekana ni Hasi (Negative)
VIPIMO VINGINE VINAVYOENDELEA
(1) Liver function - kuangalia kama ini la mgonjwa ambaye ni marehemu lilikuwa kinafanya kazi vizuri au la.
(2) Bilirubin kuangalia kiwango cha protein kwenye ini kama kilikuwa sahihi au kimeongezeka.

Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza Dr.
Kengia.
|
Taratibu zinaendelea kati ya Mkuu wa Maabara ya Taifa na Wizara ya Afya kuhusu sampuli hii kupelekwa Mbeya au jijini Nairobi nchini Kenya kwaajili ya uchunguzi wa virusi ya Ebola au Marbug.
Awali
kutokana na hofu ya ugonjwa huo huku taarifa zisizo rasmi zikizidi kusambazwa
kwa njia ya mitandao ya simu na internet wananchi wa wilaya ya Sengerema na
vijiji vya karibu walihaha katika vyombo vya usafiri husussani daladala
wakikataa kugusana kwa kuwa Ebola imeingia Mwanza, huku wafanyakazi na
wafanyabiashara wanaoishi mkoani Mwanza na kufanya shughuli zao wilayani
Sengerema wakiahirisha kuelekea wilayani humo kutokana na vitisho vya taarifa walizopata.