REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MGOGORO WA SYRIA: UFARANSA NA UINGEREZA KUWAPA SIRAHA WAASI

5:20:00 AM Add Comment



UFARANSA na Uingereza zinajiandaa kuwapa silaha waasi wa Syria hata bila kupata uungwaji mkono kutoka Umoja wa Ulaya. 

Waziri wa mambo ya nchi za kigeni wa Ufaransa Laurent Fabius amesema Ufaransa na Uingereza zitatoa wito wa kusongezwa tarehe ya mkutano ujao wa Umoja wa Ulaya utakaojadili vikwazo vya usafirishaji silaha nchini Syria, na zitaamua kuwapa waasi zana za kivita kama Umoja huo wenye nchi wanachama 27 hautaunga mkono suala hilo. 

                                 WAZIRI MKUU WA UFARANSA, LAURENT FABIUS

Fabius amekiambia kituo kimoja cha redio nchini Ufaransa kuwa nchi hizo mbili zitauomba Umoja wa Ulaya kuondoa vikwazo vya silaha dhidi ya Syria ili waasi wanaopambana kumwondoa madarakani Rais Bashar al-Assad waweze kujikinga. 
                         WAZIRI MKUU WA UINGEREZA, DAVID CAMEROON

Mkutano ujao wa Umoja wa Ulaya utakaojadili vikwazo hivyo unapangwa mwezi mwishoni mwa mwezi Mei, lakini Fabius amesema Ufaransa na Uingereza wanataka mkutano huo uandaliwe mapema. Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron alisema jana Jumatano kuwa Uingereza itazingatia kupuuza vikwazo hivyo vya Umoja wa Ulaya na kuwapa silaha waasi wa Syria, ikiwa hilo litasaidia kumwondoa madarakani Rais Assad.

PAPA MPYA AANZA KAZI RASMI

5:09:00 AM Add Comment

Baba Mtakatifu Francis wa kwanza, ambaye ndiye Papa wa kwanza kuchaguliwa kutoka Amerika ya Kusini, leo amelitembelea kanisa moja mjini Roma katika siku yake ya kwanza ya uongozi wake akilenga kulileta kanisa katoliki karibu na watu. 

Askofi huyo mkuu wa zamani wa Buenos Aires, Argentina, mwenye umri wa miaka 76, Jorge (HORGE) Mario Bergoglio, amehudhuria misa ya maombi katika kanisa la Santa Maria  (MAJIORE) Maggiore mjini Roma, ili kuanza kazi yake kama mkuu wa wakatoliki bilioni 1.2 kote ulimwenguni. Wakati huo huo salamu za pongezi zinaendelea kutumwa kutoka kote ulimwenguni. 

Waziri Mkuu wa Australia Julia Gillard amesema kuchaguliwa Papa kutoka "ulimwengu mpya" ni tukio ambalo lina umuhimu wa kihistoria. Francis ambaye ndiye Papa wa kwanza asiyetoka Ulaya katika kipindi cha takribani miaka 1,300, ameitumia ibada yake ya kwanza kumwombea mtangulizi wake Benedict wa Kumi na Sita na kutoa wito wa kuwepo udugu miongoni mwa waumini wa Kikatoliki. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametuma pongezi zake

PICHA: RAY AKIPIGA MAZOEZI...

4:54:00 AM Add Comment
 Hatua inayofuata ni Ipi Mwalim?......................................

 Anhaaa...kwa hiyo niende juu...chini...juu...chini...juu...chini...okay, nimekusoma

 Duh...siwezi kuvunja Mikono kweli Mwalimu?...maana....

 Twende Kazi...One.... Two

Dah..Siyo Mchezo ...haikuwa Kazi Rahisi Mzeee....Kumbe Hata akina DIAMOND na ALI KIBA waliumia kiasi hiki?

KUMBUKA
Maelezo hayo ya Picha ni Ya Kubuni tu...Hayana ukweli wowote kuhusiana na Ray

DABO KLIK: JE UNAMFAHAMU PAPA FRANCIS WA KWANZA?

4:47:00 AM Add Comment






Alizaliwa Mjini Buenos Aires huko Argentina mwaka1936.
Papa Francis 1 ni mtu wa kwanza katika kipindi cha miaka elfu moja (1,000) kwa mtu kutoka nje ya bara la Ulaya kutawazwa kuwa papa wa Kanisa Katoliki.

Papa Francis 1 ni mwana wa Mtaliano aliyekuwa akifanya kazi katika shirika la gari Moshi kabla ya kuhamia nchini Argentina miaka ya zamani.

Kama kadinali wa Jimbo la Buenos Aires ,Kadinali Bergoglio amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Argentina.

Hata hivyo Kadinali Bergoglio anapendwa sana na wafuasi wa kanisa hilo huko Argentina na hasa watu maskini.

adinali Jorge Bergoglio, mwenye umri wa mwaka 76, kwa karibu miaka yake yote kama Kasisi amehudumu nyumbani kwao Argentina.

Kadinali huyo wa Jimbo la Buenos Aires inasemekana aliibuka nambari mbili wakati Papa Benedict alipochaguliwa mwaka 2005

 Anaaminika kuwa na ujuzi mkubwa ambao wengi wanasema utamsaidia sana katika uongozi wake

Katika maisha yake ya huduma kwa Kanisa Katoliki huko Amerika Kusini ambapo Kanisa Katoliki lina waumini wengi zaidi duniani, Kadinali Bergoglio ameibuka kuwa mtu anayependa sana udhabiti wa kisiasa katika nchi zilizo katika bara la Amerika Kusini.

Bergoglio anasifiwa kwa kuleta mageuzi makubwa katika Kanisa la Argentina huku katika eneo hilo la Amerika Kusini Kanisa bado linashikilia itikadi za kale.

FUSE ODG Kutua KENYA

4:38:00 AM Add Comment
KWA UFUPI
MKALI wa Azonto kutoka Nchini Ghana Fuse ODG (Pichani) anatarajia kuporomosha Bonge moja la Show pande za Kenyatta Land (Kenya) Mnamo Mwezi May Mwaka huu.

FUSE ODG Hivi sasa anakimbiza mbaya na Mkwaju wake wa ANTENA ambao pia una Remix yake ambayo amemshirikisha "The Hait Icon" WYCLIF JEAN

DJ PAUL AHUKUMIWA.....

4:24:00 AM Add Comment
RAPA wa Kundi la Three 6 Mafia Nchini Marekani,Dj Paul, amepewa adhabu ya kifungo cha kufanya kazi za kijamii baada ya kukutwa na hatia ama makosa ya kumiliki Silaha Kinyume cha Sheria Nchini Marekani.

Mnamo Octoba Mwaka jana Dj Paul aliwekwa chini ya Ulinzi na Jeshi la Polisi Nchini Marekani akitoka katika Moja ya Migahawa huku akiwa na Kilevi (Bia) Mkononi, hali ambayo iliwafanya wamhoji zaidi.

Aidha Jeshi la Polisi liliripoti kuwa, Dj Paul alikiri kumiliki Silaha kinyume Cha Sheria, hali ambayo aliwafanya wamkamate.

Kabla ya hukumu hiyo, Dj Paul aliwahi kukana Shtaka la kumiliki Silaha na kusisistiza kuwa hakuwa na kosa, lakini leo alifanya majidiliano na Wanasheria wake pamoja na hakimu, na hatimaye kukiri kosa hilo.

Dj paul atatumikia Masaa 21 ya kazi za kijamii


MNADA BANNER