MPEKUZI
MREMBO aliyewahi
kupamba video kadhaa za wasanii wa Bongo Fleva ukiwemo wimbo wa Kidato Kimoja
ulioimbwa na J.I, anayekwenda kwa jina la Maya Silemwe, amedaiwa kumtelekeza
mwanaye wa kumzaa aitwaye Junior Justine (3).
Tukio hilo la kusikitisha
lilitokea hivi karibuni katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini
Dar es Salaam
ambapo mtoto huyo aliokolewa na msamaria mwema.
Akisimulia mkasa mzima ulivyokuwa, shangazi wa mtoto huyo
aliyejitambulisha kwa jina moja la Monalisa, alisema wao kama familia
wameumizwa sana
na kitendo kilichofanywa na Maya.
“Maya amezaa na kaka yangu Justine anayeishi Marekani na
amekuwa akimjali sana
kwa kumtumia fedha za matumizi mara kwa mara. Kisa ni kwamba kaka alimwambia
Maya ampeleke mtoto Bukoba (nyumbani kwa baba wa mtoto) akasalimie, Maya
akakubali lakini akamwambia atapitia kwanza Arusha (nyumbani kwao) ndipo waende
Bukoba.
“Justine akamuelewa lakini kumbe alidanganya, hakwenda
Arusha na kuna watu walimuona akiingia kwenye klabu moja hapahapa Dar es Salaam ,
wakamjulisha kaka. Sasa alipompigia kumuuliza, akawa anajing’atang’ata, siku
iliyofuata akadamkia Ubungo ili kumsafirisha mtoto kwenda Bukoba kwa mama yetu
(bibi wa mtoto) lakini alitaka kumsafirisha kwa kumtumia kondakta,” alisema
Monalisa na kuongeza:
“Alikubaliana na kondakta huyo kisha akamwachia namba ya
simu ya mama na yake ili waweze kuwasiliana na kumpokea mtoto huko Bukoba.
Kwa bahati mbaya siku ile yule konda alikuwa hasafiri mpaka
siku inayofuatia. Mtoto akaanza kuhangaika stendi siku nzima bila uangalizi
mzuri.
“Bahati nzuri mama mmoja msamaria mwema akafuatilia na
kuonana na huyo konda, akamuomba namba za mama wa Bukoba kisha akawasiliana
naye, kwa kuwa alikuwa na safari ya kwenda huko siku iliyofuata, akaamua
kuchukua jukumu la kusafiri naye.”
Monalisa alikubali kutoa namba za simu za msamaria
aliyejitolea kusafiri na mtoto huyo, alipopigiwa alikiri lakini aliomba sana asitajwe .
“Mimi kama mzazi iliniuma sana kumuona mtoto mdogo anahangaika stendi
bila uangalizi. Nilishangaa sana
kuona mzazi aliyeingia ‘leba’ anawezaje kumwacha mwanaye mdogo namna ile
asafiri mwenyewe?” alisema.
Naye baba mzazi wa mtoto huyo, Justine aishiye
Marekani ambapo alisema kuwa:
“Jambo hilo limeniumiza
sana . Kwa kweli
kama ningekuwa huko nyumbani (Bongo)
ningehakikisha namfundisha adabu huyo mwanamke kupitia sheria.
“Nashukuru kusikia kwamba mwanangu alifikishwa salama
Bukoba.”
Mama wa mtoto huyo alipopigiwa simu alizua kioja baada ya
kukataa kwamba hajawahi kumuacha mtoto kwa konda Ubungo na pia akadai eti hana
mtoto na wala hajawahi kuzaa katika maisha yake yote.
Wakati tukijiandaa kwenda mitamboni juzi Jumatatu, habari
zilizopenyeza katika chumba chetu cha habari zilisema kwamba mrembo huyo
alimpigia simu mama mkwe wake na kumchimba mkwara mzito.
EmoticonEmoticon