Nimebahatika kusikia Nyimbo tofauti sana za
wasanii wengi wa kike kutoka jijini Mwanza. Tunashukuru wengine walitangulia
katika mafanikio huku wakiibeba Heshima ya jiji Hili na Kuifikisha Sehemu
Nzuri. Naweza kusema Ahsanteni sana.
Lakini hivi sasa Muziki umekuwa sana, na Vizazi
vipya zinazidi Kuusukuma mpaka kuufikisha hapa ulipo.
Pasipo Kificho, Muziki wa Mwanza ni Mzuri sana,
na kwa mtu yeyote anayeishi Mwanza, hakika hawezi kupingana na Hilo. Lakini
kumekuwa na Changamoto kubwa sana ambayo inaukabili Muziki huu, na hata kufikia
hatua ya kujenga “Ukuta” mkubwa baina ya mafanikio haya ya Muziki wa jiji hili,
pamoja na soko kiujumla.
WAKAZI WA MWANZA wamekuwa ni sehemu kubwa ya
kukwamisha maendeleo ya Muziki wa jiji hili tofauti na ilivyo katika JIJI la
ARUSHA. Kuanzia kuusikiliza, kuufuatilia, kuusambaza na hata kuuandalia
matamasha mbali mbali, vitu hivi vimekuwa ni historia kwa wasanii wa Mwanza na
kazi zao. Ni sehemu chache sana hasa za Ndani, ambazo zimekuwa zikupa “Kik”
Muziki huu, Mfano Mzuri ni UKEREWE.
Tofauti na Hilo, WADAU WA MUZIKI “FEKI” wamekuwa
Wengi sana. Tukubali tukatae, Suala la “Menejimenti” Limekuwa ni tatizo kwa
Mwanza Tu, bali hata Nchi nzima. Tumekuwa tukisikia wasanii kadhaa wakubwa
wakilalamika Utapeli na ujinga unaofanywa na Wanaojiita mameneja, lakini Mwisho
wa siku hakuna kinachofanyika katika kufaidika na Muziki wao. Tunakubali, ni
vema kujitolea kumsaidia Msanii kuanzi kumsimamia katika kazi zake, lakini
ukweli ni kwamba, mameneja hawa pamoja na Wadau wengine “feki” wanaongeza kila
siku, na wanawatumia sana wasanii hasa hawa chipukizi ama wenye hamu ya kufanikisha
kazi zao, kujinufaisha wao wenyewe.
UDHAMINI hasa katika matamasha, umekuwa kikwazo
pia. Iko hivi, katika jiji la Mwanza, ukiandaa Tamasha (Shows, Events) ambazo
zitawahusisha wasanii wa Mwanza tu, halafu ukaombe udhamini, Hesabu maumivu
kabisa. Lakini ukiandaa tamasha ambalo litamuhusisha Diamond, Madee, Chege, na
wengineo wengi tu, wenye majina, basi hapo utawapata unaowataka. Undhani hii
itaufanya Muziki wa Mwanza ufikie pale unapotakiwa Kufika?
EMMY SANGO NA HONEYA…WANAHITAJI KUFIKA PAZURI.
Usinibanie Ndiyo Track ambayo
Kiujumla ilimtambulisha Emmy katika Muziki wa Zouk hapa Mwanza, na hata
kwingineko. Uwezo wake ulidhihirishwa na Track yake ya Pili inayofahamika kwa
Jina La RADIO PRESENTER.
Kiufupi, Uwezo wake uko Vizuri
sana, tangia nimeanza kumsikiliza, kuurudia mara kadhaa, kuwahusisha wenzangu,
hakika anaweza kushindana na Wasnii wa kike kama akina linah, na Wengineo.
Infact, UWE WANGU, ndiyo Track
yake ya Kwanza kaisa kurecord na hata Kuiachia. Ukiisikiliza kwa Umakini,
unabaini kabisa kuwa bnti huyu anaimba kwa hisia sana, na anajua kipi ambacho
anatakiwa kufanya katika “TOPIC” ya Wimbo anaouimba.
Sauti yake na mpangilio wa
uimbaji wake, lazima utadhani amepitia “Training “ yoyote ya sauti, lakini
nilipozungumza naye alisema hajawahi kupitia Training College yoyote hasa ya
Sauti.
KWA MANTIKI HIYO, hebu tutafanye kitu kimoja.
Sisi wasikilizaji, Wadau wa Muziki, watangazaji wa Redio mbali mbali kama Mie,
Bloggers wote ambao tumejitambulisha ku-support Muziki wa Tanzania,
tuwasikilize mabinti hawa, na tuwasukume. Ingawa ni kweli mapungufu yapo,
lakini kupitia wewe, kila kitu kitakuwa ni funzo tosha kwao, na hatua nyingine
nzuri zaidi kwao.
Mwanza is the Best
PATA NAFASI YA KUZISIKILIZA NYIMBO ZAO KWA UMAKINI