WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
MWANAHABARI MWINGINE APIGWA RISASI NA JESHI LA POLISI..
Na Francis Godwin
Mwanahabari mwingine
mkoani Dar es Salaam apigwa
risasi na askari polisi
ambao wanadaiwa kuwa
walikuwa wakimsaka mtuhumiwa wa ujambazi
mwanamke na kuishia kumpiga mwanahabari
huyo mwanaume Bw Shaban Matutu wa gazeti la Tanzania Daima.
Tukio hilo limetokea
jana majira ya saa 2 usiku jijini
Dar es Salaam ambapo askari hao
walipofika nyumbani kwa
mwanahabari huyo na kumgongea mlango na wakati akifungua mlango ndipo
Matutu amepigwa
risasi na Polisi, ambao wanadaiwa walikuwa wanamtafuta mhalifu ambapo katika
zoezi hilo, walienda na kugonga chumbani kwa Mwandishi huyo, kabla ya kutwanga
kwa risasi.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, mara baada ya tukio hilo,
mwandishi huyo amekimbizwa hospitali ya Mwananyamala ambako anaendelea kupatiwa
huduma ya haraka na inaelezwa kuwa, amejeruhiwa lakini hali yake si mbaya sana
Habari zaidi zitakujieni
Taarifa za uhakika na ambazo zimethibitishwa zinaeleza kuwa
jana usiku polisi mwenye silaha, aina ya bastola alimjeruhi begani kwa risasi,
mwandishi wa habari wa Tanzania Daima, Shaaban Matutu.
Risasi bado imenasa kwenye bega lake hadi sasa Matutu
alipigwa risasi nyumbani kwake Kunduchi, Dar es Salaam wakati askari
walipovamia nyumba yake kwa madai kwamba kuna kibaka aliingia kujificha
nyumbani hapo. Hivi sasa Matutu anatibiwa Mwananyamala hospitali, lakini
amepewa rufaa kwenda Muhimbili.
Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Tanzania Bw Absalom
Kibanda, ambaye amefanya jitihada za kumuhamishia Matutu Muhimbili, anasema
hali ya Matutu siyo nzuri na kwamba wanajipanga kwenda Muhimbili kuona iwapo
risasi hiyo itaondolewa mwilini.
Hata hivyo Kibanda ameeleza kusikitishwa kwake ni vitendo vya uvunjifu wa amani dhidi ya wanahabari nchini Tanzania ambavyo vimeendelea kufanywa na jeshi la Polisi nchini na kutaka polisi waliofanya
hivyo kuchukuliwa hatua kali.
Alisema wakati Taifa likiwa bado katika majonzi ya mauwaji ya
kinyama ya Mwandishi wa Chanel Ten mkoa wa Iringa Daudi Mwangosi
leo tunashudia tena unyama mwingine
dhidi ya mwanahabari huyo.
Hivyo iwapo jeshi
la polisi litakosa majibu juu ya sababu
ya kumpiga risasi mwanahabari huyo ambaye hata hivyo hakuwa mlengwa katika msako wao wa kumsaka mtuhumiwa wa ujambazi ambae ni
mwanamke basi itafika sehemu wanahabari nchini watalichukulia jeshi la polisi ni maeneo ya
hatari kwao
TAARIFA KWA UMMA
TANGAZO KWA UMMA.
Mkuu wa Chuo cha ROYAL (Royal College Of Tanzania-RCT) anapenda kuwataarifu kuwa Mahafali ya 11 yatafanyika Disemba 22, 2012 Katika VIWANJA VYA CHUO Hicho.
Watakaohitimu ni :
- Stashahada ya Uandishi wa Habari na Utangazaji (Diploma in Journalism)
- Stashahada ya Ustawi wa Jamii (Diploma in Social Work With Community Development)
- Astashahada ya Uandishi wa Habari na Utangazaji (Certificate in Journalism)
- Astashahada ya Ustawi wa Jamii (Certificate in Social Works with Community Development)
Uthibitisho huo Ufanyike Kupitia namba Zifuatazo : +255756 672 684 au +255713 390 903
Nyote Mnakaribishwa katika Maendeleo ya Tasnia ya Habari Nchini
Imetolewa na
Nsajigwa Mwalugaja,
Mkuu Wa Chuo cha Royal (Royal College Of Tanzania- RCT)
WANANCHI WA ZANZIBAR WATAKIWA KUTEMBELEA UTALII WAO
Na Safiya Mohammed "Safmuu", ZANZIBAR
Wananchi wameshauriwa kutekeleza agizo la Utalii kwa wote
kwa kuyatembelea maeneo mbali mbali ya utalii Zanzibar ili kufahamu historia ya
nchi ya Zanzibar kabla na baada ya Mapinduzi.
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa
Divisheni ya Makumbusho Zanzibar Khamis Abdallah Ali wakati alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari katika ziara iliyojumuisha wanahabari na
maafisa wa Makumbusho.
Pia ameongeza kuwa katika kutekeleza agizo la Utalii kwa wote
wananchi wanapaswa kushajihishwa kutembelea maeneo ya kihistoria badala ya
kuwaachia watalii peke yao kufanya ziara katika maeneo hayo. Bw. Abdala amesisitiza kuwa ni jambo
la kusikitisha kuona wenyeji hawana hamu ya kujua historia ya nchi yao na
kuwafanya wageni kujua historia ya Zanzibar.
Aidha Mkuu huyo wa makumbusho amemaliza kwa kusema kuwa Idara ya
Makumbusho imeweka kiwango kidogo cha Shilingi 1000 ili kumrahisishia mwenyeji
pale anapohitaji kwenda kutembelea maeneo ya makumbusho kwa ajili ya kujua
historia ya nchi yao
HAWA NDIO VODACOM.....KAZI NI KWAKO SASA.
Taarifa kwa vyombo vya Habari
* Vodacom na
Nokia yaja na ofa ya funga mwaka
* Maelfu ya
zawadi kushindaniwa kwa wanunuzi wa simu za Nokia
* Pia kufaidika
na SMS, muda wa maongezi na internet za
bure
Dar es Salaam, Disemba 4, 2012 ... Wakati shamrashamra za
maandalizi ya msimu wa sikukuu za mwishoni mwa mwaka yakiwa yanaendelea,
Kampuni ya Vodacom Tanzania na Nokia
zimetambulisha ofa kabambe kukamlisha furaha ya kuelekea kufunga mwaka wa 2012.
Kampuni hizo kwa
pamoja zimezindua rasmi shindano litakalomuwezesha mteja yeyote atakayenunua
simu ya mkononi aina ya Nokia,
kujishindia zawadi mbalimbali papo kwa hapo, pamoja na kupata fursa ya kuingia
kwenye droo kuu.
Mteja atakayenunua simu ya Nokia na kisha kuweka muda wa
maongezi wa aidha Tsh 1,000 au Tsh 1,500
atapata kifurushi cha BURE chenye muda wa maongezi wa dakika 10, SMS 50 na internet ya MB10 kila siku kwa muda wa
wiki moja. Kila simu ya Nokia itakayonunuliwa itakua na namba maalumu/kuponi
ambayo mteja atatakiwa kutuma namba hiyo kwa SMS kwenda 15544 ili kuingizwa
kwenye droo. Kila SMS itakayotumwa kwenda kwenye namba 15544 itatozwa gharama
ya kawaida ya SMS.
Washimdi wa droo hizo zitakazokuwa zikichezeshwa kila siku
watakuwa wakijishindia zawadi za simu, chargers, t-shirts na headphones
zitakazotolewa kwa wateja kama zawadi za papo hapo.
"Ushiriki wa kubahatika kujishindia zawadi za papo hapo
humuwezesha mteja kuingia moja kwa moja katika Droo kubwa ya mwisho
itakayofanyika Januari 11, 2013 ambapo washindi watapata simu za kisasa za
Nokia Lumia."Alisema Mkuu wa Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin
Twissa
Washindi wa zawadi za kila siku watachukua zawadi zao katika
maduka ya Vodacom yaliyochaguliwa, ambapo watapatiwa huduma stahiki
Shindano hilo litafikia tamati ifikapo Januari 10, 2013,
majira ya usiku, na Januari 11, 2012 ndiyo siku ambayo Vodacom na Nokia
zitachezesha droo itakayoshirikisha washiriki wote wa shindano hili toka
mwanzo, na kati yao mshindi atatangazwa
Subscribe to:
Posts (Atom)