Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Husein Mwinyi
Na Beatrice Moses
SERIKALI imejiwekea lengo la kutahiri wanaume milioni 2.8
ifikapo mwaka 2015, baada ya kufanikiwa kuwatahiri 287,055 kati ya mwaka 2010
na 2012.
Hayo yamebainishwa katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii, ikifafanua kuwa huduma ya tohara ya kitabibu kwa
wanaume ilianzishwa mwaka 2010.
Imetekelezwa zaidi mikoa ambayo ilibainika kuwa na kiwango
cha juu cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
“Iligundulika kiwango cha juu cha maambukizi ya VVU ambako
kuna kiwango cha chini cha tohara kwa wanaume.
Mikoa hiyo ni ya Iringa, Njombe,
Simiyu, Geita, Katavi, Mbeya, Rukwa, Tabora, Kagera, Mwanza na Mara,” inaelezwa taarifa hiyo.
Inaelezwa kuwa Serikali ilifanikiwa kuwafanyia tohara
wanaume hao kwa kutumia njia ya kuwaelimisha kwa kuwaelezea umuhimu wa tohara
na hatari inayowakabili kwa kuendelea kuishi bila kufanyiwa tohara hasa
kuambukizwa magonjwa ya zinaa ikiwamo VVU.
Pia, taarifa hiyo inaeleza kuhusu mpango wa kuzuia
maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa mwaka 2005, wajawazito
11,435 ambayo ni asilimia tisa ya wenye maambukizi ya virusi.
Inasema walipatiwa dawa za ARVs kuzuia maambukizi hayo
kwenda kwa mtoto.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa, wizara hiyo inaendelea kutoa
kupaumbele maeneo ya kudhibiti magonjwa ya ngono, utoaji ushauri nasaha na
huduma kwa wagonjwa wa nyumbani, elimu na habari, tiba na matunzo, huduma ya
maabara kwa wagonjwa waishio na VVU.
“Hamasa kwa Watanzania imekuwa ikiongezeka hasa baada ya
kampeni iliyoongozwa na Rais (Jakaya Kikwete) mwaka 2007, idadi ya vituo vya
upimaji iliongezeka kutoka vituo 521 mwaka 2005 hadi 2,200 mwaka jana,” inasema
taarifa hiyo na kuongeza:
“Iidadi ya wananchi waliopatiwa huduma hiyo nayo
imeongezeka kutoka watu 365,189 mwaka 2005 hadi watu 17,008,475 Machi mwaka
jana