WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
"Huruma ya Usher kwenye kifo cha Mtoto Wangu Ni UPUUZI Mtupu!!!- Tameka
Marehemu Kile, Mtoto Wa Tameka. |
Tameka Raymond, na Usher Rymond. |
Ex- Wife wa Muimbaji machachari katika miondoko ya R&B
Usher Rymond, Tameka Rymond , amebainisha kuwa Huruma ya Usher Rymond dhidi ya
kifo cha Marehemu mtoto wake kilichotokea Hivi karibuni, Ni UPUUZI na UNAFIKI
MTUPU!!!!!!!!!!!!
Bibi huyo ambaye bado kabisa yuko kunako Majonzi ya Mtot
wake Mpendwa aliyepata ajali na kuathirika katika sehemu kubwa ya Ubongo,
amesema kuwa Kitendo cha Usher kujifanya anahuruma….kinamkwaza saaaana
“Usher ni Mnafiki sana na ni mpuuzi katika hilo. Anazuga
kuathirika na kuumia sana dhidi ya Kifo cha Mtoto wangu KILE mbele ya marafiki
zake, Mitandao ya Kijamii na Vyombo vya Habari pia".
Mrembo huyo amesema kuwa, Usher amekuwa akijifanya kuwa na Stress kibao hasa
wakati anapokuwa akifanya maintavyuu kibaao
Tameka amefungua Kesi dhidi ya Mkali huyo wa “Dady’s Home”
kwa kushirikiana na Mwanasheria wake, ambapo usher mwenyewe aesema kuwa, kesi
hiyo haitakuwa na manufaa yoyote kwa Tameka, na italeta matatizo chungu mzima
kwa wawili hao na watoto wao wawili ambao bado ni wadogo
“Ukiachana na hayo, Tameka hatapata haki ambayo anaitarajia
maanake, mahakama haitokuwa tayari kusikiliza Kesi ambayo imeanzishwa na Mama
ambaye bado yupo katika maombolezo.” Alidai Usher
Katika madadi Makuu ya Tameka ni kwamba, Mumewe huyo
hakujali hali ya Mtoto wake (Kile) katika Siku za Mwisho alipokuwa katika hali
mbaya Hospitali, licha ya Usher kukubali na kujidhatiti kumchukulia kama Mtoito
wake baada ya wawili hao kufunga ndoa
“Usher alimtembelea
marehemu mwanangu Kile hospitalini mara moja tu, kati ya siku 15 ambazo
mwanangu alikuwa akihangaikiwa kupigania Uhai wake” aliongeza Tameka.
HII SASA KALI!!!!!.....................................
Katika hali ambayo haikutarajiwa, Tameka anongeza kuwa,
alimsihi sana Usher aandike katika Ukurasa wake wa TWEETER kuwa “TAFADHARI,
MUOMBEENI KILE”, lakini Usher alitia ngumu kabisa, na badala yake, Usher
aliweka Picha ya Chai yake katika Ukurasa huo wa TWEETER, huku akiandika chini
ya picha hiyo kuwa “CHAI YA WASHINDI”
Floyd Mayweather aachiwa Huru
Bondia Floyd Mayweather. |
New York, MAREKANI.
The Boxing Champ mwenye Utata Mkubwa, Floyd Mayweather Jr,
ameachiwa Huru siku ya Ijamaa Aasubuhi kutoka katika Jela ya Vegas, ambako
alitumikia Kifungo cha miezi miwili kati ya Mitatu aliyokuwa amehukumiwa
kutokana na ukatili wa Nyumbani
Jembe hilo (Floyd) alihukumiwa kutumikia Kifungo hicho mnamo
December mwaka 2010, baada ya Kushushia
Kifinyo mama wa mtoto wake mbele ya Watoto wake, lakini Mpiga Nyundo (Hakimu)
alimruhusu kuanaza kutumika Kifungo chake Mwezi June, Tarehe 1, kutokana na
Kuwepo kwa Mpambano dhid yake na Miguel Cotto uliopangwa kuchimbika May 05
Mwaka jana, ambapo Floyd alishinda.
Msemaji wa Mpiga Masumbwi huyo, amefafanua kuwa, jombaa
alihukumiwa kifungo cha Miezi 6, baada
ya kugundulika kuwa na makosa, sambamba na kuwakung’uta watoto wake katika
Tukio hilo.
Jamaa huyo naongeza kuwa Floyd alionesha Tabia nzuri akiwa
katika kifungo hicho, ambapo pia alitumikia masaa 100 katika shughuli za
Kijamii.
Kim Jong Un, Rais wa Korea Kaskazini |
Pyongyang, Mji Mkuu wa Korea Kaskazini. |
Na Frank M. Joachim & DW
Pyongyang, KOREA KASKAZINI
Korea ya Kaskazini inahitaji msaada wa haraka wa chakula,
baada ya mvua kubwa kuuwa idadi kubwa ya watu na kusababisha mafuriko katika
maeneo mengi ya kilimo.
Haya yametangazwa na afisa wa Umoja wa Mataifa jana, ambapo amesema ofisi ya Umoja wa Mataifa katika mji
mkuu wa Korea Kaskazini Pyongyang imethibitisha hali hiyo baada ya kuyazuru
maeneo yaliyoathirika mwanzoni mwa wiki.
Mvua kubwa iliyonyesha mara mbili iliuwa watu 119 na
kuharibu maelfu ya nyumba za watu, hii ikiwa ni kwa mujibu wa vyombo vya habari
vya serikali ya Korea Kaskazini. Marekani imesema inatathmini msaada inaoweza
kuutoa, ingawa haijapata ombi kutoka kwa Korea Kaskazini. Mvua hizo ambazo
zilifuatia kipindi kirefu cha ukame, imezusha wasiwasi juu ya uwezo wa Korea
Kaskazini kutosheleza mahitaji ya chakula kwa watu wake.
Mwezi Juni Umoja wa Mataifa ulisema theluthi mbili ya wakazi
milioni 24 wa Korea Kaskazini hawana chakula cha kutosha.
Urusi yatuma Meli za Kivita Nchini Syria
Moja kati ya Meli Hatari za Kivita za URUSI. |
Na Frank M. Joachim & DW
Moscow, URUSI.
Watu wengi wameuawa katika mitaa ya mji wa Hama ulio
katikati mwa Syria, ambao umezingirwa na wanajeshi wa serikali.
Ripoti hii ni kwa mujibu wa Shirika la Kuchunguza Haki za
Binadamu la nchini Syria lenye makao yake nchini Uingereza. Shirika hilo
halikutaja idadi kamili ya waliokufa, likisema mawasiliano ya simu katika
wilaya ya Al-Arbaeen yalikuwa yamekatwa.
Hata hivyo, Kamati ya Kuratibu Shughuli za Wanaharakati imesema
waliokufa, ambao ni raia na waasi, hawapungui 50. Hakuna shirika lisiloegemea
upande wowote lililothibitisha idadi hiyo.
Msemaji wa Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Syria Hisham
Hassan amesema wameondoa wafanyakazi wao kwa kuhofia usalama. Huku hayo yakiarifiwa, Urusi imetuma meli
tatu kubwa za kivita nchini Syria, zenye kubeba nyambizi 120 kila moja.
Shirika la Habari la Urusi limemnukuu afisa wa Urusi
akithibitisha kutumwa kwa meli hizo, lakini sababu ya kile zinachokwenda
kukifanya haikutajwa. Wakati huo huo tangazo la kujiuzulu kwa mpatanishi wa
kimataifa nchini Syria Kofi Annan ifikapo mwishoni mwa mwezi huu, limechukuliwa
na wachambuzi kama kutoweka kwa uwezekano wa kupatikana kwa sulihisho la amani
katika mzozo wa Syria.
Subscribe to:
Posts (Atom)