REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

Watalii wa Kigeni Watekwa Nyara Nigeria

4:06:00 PM Add Comment


                                                                 Lagos, Nigeria

Na Frank M. Joachim.

Watu wenye silaha wameivamia mashua inayomilikiwa na kampuni ya huduma za mafuta katika bandari ya Nigeria leo, na kuwateka nyara raia wanne wa kigeni na kuwaua Wanigeria wawili.

Msemaji wa Jeshi la majini la Nigeria, Kabir Aliyu, amethibitisha kutekwa kwa wataalamu hao wanne wa kigeni na kuuawa kwa mabaharia wawili.

Pia ameongeza kuwa, uraia wa wageni waliyotekwa nyara bado haujathibitishwa. Maafisa sita wa jeshi la majini, ambao wote ni raia wa Nigeria walikuwepo kwenye mashua hiyo, ambayo inamilikiwa na kampuni ya Sea truck Oil Services, kuhakikisha usalama.
Wawili kati yao waliuawa na wawili walijeruhiwa, alisema Aliyu. Aliongeza kuwa jeshi la majini la Nigeria limetuma boti na helikopta katika eneo la tukio.

CHONDE CHONDE KENYA!!!!

3:53:00 PM Add Comment

 


 A

Raisi wa Kenya, Mwai Kibaki, na Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton

Na Frank M. Joachim & DW
Nairobi, KENYA
 Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Hillary Clinton, ameitaka Kenya iendeshe uchaguzi huru na wa haki, ili iwe mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine duniani.
Clinton amezitaka mamlaka zinazohusika na kuandaa uchaguzi wa mwakani, kuhakikisha kuwa nchi hiyo haitumbukii tena katika machafuko kama yaliyotokea mwaka 2007, ambapo watu 1,200 waliauwa. Waziri Clinton alikutana na rais Mwai Kibaki, ambaye kikatiba haruhusiwi kuogombea muhula mwingine, na Waziri Mkuu Raila Odinga, anayeongoza katika kura za maoni kuelekea uchaguzi huo.
Clinton alisema serikali ya Marekani iko tayari kuisiadia Kenya kuhakikisha inaendesha uchaguzi huru na wa haki na kuwataka raia wote wa Kenya kuungana pamoja na kuandaa uchaguzi utakaokuwa mfano wa kuigwa. Clinton, aliyeko barani Afrika kwa zaira ya mataifa saba, alitarajiwa pia kukutana na rais wa Somalia, Sheikh Sharif Ahmed, na maafisa wengine wa nchi hiyo, kabla ya kuelekea Malawi na Afrika Kusini.

MNADA BANNER