REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

STORY YA RAH P AKIWA NCHINI MAREKANI, INASIKITISHA KIUKWELI...

9:30:00 AM Add Comment



Nilipotembelea Dar hotwire leo, nilishtuka sana kukutana na Story ambayo inamuhusu mwanadada Rah P, Mtanzania aliyewika sana kipindi cha Nyuma kupitia Track yake kali ya HAYAKUHUSU huku akishirikishwa katika Ngoma ya MIKASI ya Albert Mangwea.
 
Kama ulikuwa Mfuatiliaji wa muziki wa Hiphop hapo siku za nyuma basi huwezi kuwa umemsahau mwanadada Rah P.
Rah P aliamua kwenda Marekani kusaka life la ukweli lakini kilichokuta huko mpaka kuzalishwa watoto wawili mungu peke yake ndio anajua.

Nimejaribu kutafuta VIDEO ambayo inamuonesha Rah P akizungumzia kisa halisi hasa kilichomkuta, lakin Bahati Mbaya haikuwa aikifunguka yote

Video hiyo inapatikana www.kalitv.com

joachimjunior.blogspot.com inajitahidi kupata hasa kilichomkuta RAH P...

HIZI NI BAADHI YA PICHA ZA RAH P AKIWA OUTSIDE OF TANZANIA, yaan AMERICA









IRAEL YAENDELEZA UKATILI...

4:01:00 AM Add Comment
GAZA, Israel


Utawala haramu wa Israel umeendeleza ukatili wake kwa kuwaua shahidi Wapalestina wawili katika hujuma ya hivi karibuni  Ukanda wa Ghaza. Tayari Wapalestina karibu 50 wameuawa shahidi katika mashambulio ya  siku nne ya ndege za kivita za Israel dhidi ya watu wa Ghaza. Wanawake na watoto ndio whanaga wakubwa wa jina zinazoendelea za Israel dhidi ya Wapalestina huko Ghaza. Aidha katika hujuma ya hivi karibuni, ndege za kivita za Israel zimelenga jengo la mashirika ya habari mjini Ghaza ambapo waandishi habari sita wamejeruhiwa.

Wakati huo huo katika hatua ya kulipiza kisasi jinai za Israel, wanamapambano wa Palestina wamevurumisha makombora zaidi katika mji wa Tel Aviv.

Wakati huo huo viongozi wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu wamekutana mjini Cairo Misri na kusema wanaunga mkono Wapalestina katika kipindi hiki ambacho wanakabiliana na hujuma ya Israel. Hata hivyo viongozi hao wa nchi za Kiarabu wameshindwa kuchukua hatua za kivitendo za kukabiliana na ukatili wa Israel dhidi ya Wapalestina.

SHEIN AHAIDI KULINDA MUUNGANO

3:29:00 AM Add Comment


  Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, na Rais Wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amesema atahakikisha anatekeleza Ilani ya chama hicho inayosisitiza kulinda Mapinduzi na Muungano wa Tanzania wenye muundo wa Serikali mbili. 

Dk Shein Ameongeza kuwa, Muungano wa Serikali mbili ndio ulioasisiwa na viongozi wawili, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Abeid Amaan Karume, kwa kuwa waliona una maslahi kwa pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais wa Zanzibar amesisitiza kuwa, ana uhakika wapo watu ambao hawautakii mema Muungano uliopo na ndio maana wamekuwa wakitoa kila aina ya sababu na chokochoko za kutaka kuuvunja Muungano. 

Dk Shein amesema Wazanzibari waliopo Tanzania Bara wapo huru kufanya shughuli zao za kibiashara zinazowapatia kipato kikubwa huku wakiendesha maisha yao vizuri na kusisitiza kuwa hizo ndizo fursa za Muungano. 

Msimamo huo unatarajiwa kuwa mwiba miongoni mwa wanasiasa wengine ndani ya serikali ya umoja wa kitaifa Visiwani Zanzibar.

DK. SLAA AMEICHAMBUA HIVI CCM

3:05:00 AM Add Comment
Katibu Kuu Wa CHADEMA, Dr. Willibroad Slaa



ADAI WATEULE WAPYA WANA TASWIRA YA UFISADI

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ameichambua safu mpya ya uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyoundwa hivi karibuni mjini Dodoma, akisema wana taswira ya ufisadi.
Amesema kuwa hali hiyo inatokana na baadhi yao kuhusika kwenye matukio kadhaa ya kifisadi moja kwa moja.

Akizungumza na Tanzania Daima jana kuhusu mtazamo wake kwa safu hiyo mpya ya uongozi wa CCM iliyoundwa na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, katika mkutano mkuu uliomalizika juzi, Dk. Slaa alisema haoni jambo jipya.
“Nadhani hakuna jambo jipya, kipya ni kwamba wameteuliwa jana, lakini wote ni wazoefu wachafu,” alisema.

Katika safu hiyo, Kikwete anasaidiwa na makamu wawili, Philip Mangula wa bara na Dk. Ali Mohamed Shein wa visiwani na pia alimteua kada mkongwe, Abdullahman Kinana kuwa Katibu Mkuu mpya wa CCM.

Wengine wanaounda Sekretarieti ni Zakhia Meghji, Mwigulu Nchemba, Asha-rose Migiro, Vuai Ali Vuai, Nape Nnauye na Mohamed Seif Khatib.
Akimchambua mmoja baada ya mwingine, Dk. Slaa alimtuhumu Mangula kuwa ni mmoja wa watu waliohusika na ufisadi wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania.

“Makamu Mwenyekiti Mangula anahusika na EPA, vimemo vingi vya kutaka fedha za EPA vimetokea kwake…sioni leo atajisafishaje kuleta tumaini jipya kwa Watanzania,” alisema.
Kuhusu Meghji, Dk. Slaa alisema huyo ndiye aliyeandika barua na kudanganya kuwa fedha hizo za EPA zimetoka kwa ajili ya Usalama wa Taifa.

“Sasa mtu kama huyo aliyedanganya, leo hii ukamweka kwenye fedha maana yake ni ku-‘recycle material’ ile ile,” alisema Dk. Slaa.

Akimchambua Katibu Mkuu, Kinana, alisema kigogo huyo ana mkono katika biashara chafu za makampuni ya meli na kwamba hajakanusha mpaka sasa.

Dk. Slaa alisema Kinana ambaye alikuwa meneja kampeni wa mgombea urais wa CCM mwaka 2010, katika chaguzi hizo CCM imeshutumiwa kwa kuiba kura, hivyo uteuzi wake ni kukubali kuzika demokrasia nchini.

Alisema timu hiyo imeundwa mahsusi kwa ajili ya kujiandaa kuiba kura mwaka 2015.
Dk. Slaa aliongeza kuwa baada ya uchaguzi, CCM walitumia fedha nyingi kwa ajili ya kwenda kufanya utafiti wa kukijenga upya chama chao, ambao uliozaa kauli mbiu ya ‘Kujivua Gamba’, kwamba pamoja na kazi ya kitaalamu wameshindwa kuvuana magamba.
Alifafanua kuwa hatua hiyo inatokana na ukweli kwamba walioitwa magamba sasa wamo kwenye safu mpya ya uongozi wa CCM.

Katika kile kinachoonekana kuwa ni kumjibu Rais Kikwete hasa kutokana na kauli yake kuwa wapinzani wanafanya kazi ya kueneza uongo na kuwataka makada wa CCM kujibu mapigo, Dk. Slaa alimtaka aache kuwadanganya Watanzania.
Dk. Slaa alisema kuwa Rais Kikwete huenda hasomi, anadanganywa au anapenda lugha rahisi za kusema wenzake waongo.

“Mawaziri wameutumia Mkutano Mkuu kwa mbwembwe kueleza uongo…katika ripoti ya Juni 2012, hali ya uchumi wa taifa, iliyoandikwa na Ofisi ya Rais, Ofisi ya Mipango, na kelele zote zilizopigwa kuhusu maendeleo yaliyopatikana kwenye barabara.

“Kwenye ripoti hiyo imeandikwa kuwa mwaka 2011 barabara zilizokuwa katika hali nzuri ni kilomita 5,976 sawa na asilimia 30.4 ya barabara zote za mikoa,” alisema.

Ukilinganisha na mwaka 2010, barabara zilizokuwa na hali nzuri ni kilomita 11,012, maana yake ni kuwa nusu ya barabara zilizokuwa nzuri mwaka 2010 leo mwaka mmoja baadaye ni mbaya.

Aliongeza kuwa wakizitumia takwimu hizo ambazo zimeandikwa na Ofisi ya Rais, bado wanaambiwa ni waongo.

Alisema itakumbukwa kwenye viwanja vya Mwembe Yanga wakati alipotoa orodha ya mafisadi, Rais Kikwete alimjibu kuwa kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kulala lakini leo amekiri ufisadi upo CCM.

Mwanasiasa huyo machachari, alisema kuwa Rais Kikwete amesikika mara kadhaa akilalamika kuhusu ufisadi ndani ya chama chake na kuhoji kati yake yeye na Kikwete nani muongo?

“Aidha Rais sio makini; anapenda maneno rahisi…tunamwambia aweke hadharani takwimu asilete propaganda,” alisema.

Slaa alikumbusha pia jinsi ambavyo Rais Kikwete na CCM walivyowaita ni waongo wakati CHADEMA walipokuja na sera ya matumaini kwa Watanzania mwaka 2010, wakisema nyumba za tembe na nyasi sasa basi na kueleza mikakati yao ya kushusha bei ya saruji na vifaa vya ujenzi.

Katika hilo Dk. Slaa alisema kuwa alifurahi juzi kusikia CCM katika maazimio ya Mkutano Mkuu wao wakisema kuwa watashusha bei ya saruji na vifaa vya ujenzi.
“Sasa CCM na CHADEMA nani waongo? Mimi nasema hakuna kitu kinachotushangaza katika uongozi wa sasa, timu ni ile ile ya mafisadi,” alisema

Aliwataka Watanzania kuwa makini akidai kuwa waliowekwa kwenye safu ya uongozi CCM ni mafundi wa ufisadi na kutoa wito kuwa wajiandae kulinda kura.

Naye Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi Samuel Ruhuza, alisema wao kama chama wanawapongeza CCM lakini kwa jicho la siasa hawaoni kipya na kwamba viongozi wapya ni wachovu wale wale.

“Hawana jambo jipya kwa sababu CCM imechoka sana haina watu wapya ni walewale, sasa hivi tulitegemea vijana wapya lakini hilo halijatokea,” alisema Ruhuza.

JK awasuta wabaya CCM
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM), Rais Jakaya Kikwete, amewashambulia wanachama wa chama hicho waliokuwa na ndoto za kuona mkutano mkuu wao ukimalizika kwa mpasuko, akisema kuwa wameshindwa.

Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana ikiwa ni siku moja baada ya kuiteua sekretarieti ya chama hicho, itakayoongozwa na Katibu Mkuu, Abdullahman Kinana.

Akiwatambulisha rasmi wateule hao, Rais Kikwete alisema anawashangaa baadhi ya wanachama ambao wanaifahamu vizuri CCM lakini walikuwa wakiombea mabaya ili mkutano umalizike vibaya waweze kujivunia kile walichokikusudia.

“Namshukuru sana Mungu tumemaliza salama; kuna watu walikuwa wakitambika usiku na mchana CCM imalize vibaya mkutano wake na walitamani itoke na vipande lakini wameshindwa na sijui watamdai nani gharama zao?” alihoji.

Alisema watu hao wamepoteza muda wao bure na CCM imara imeweza kumaliza mkutano wake vizuri na kupanga safu ya ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na kuingia Ikulu mwaka 2015.

“Nimesikia mambo mengi na kuna watu kabisa walikuwa wakinijia wakiniambia kuwa kuna jambo hili na hilo, lakini nilikuwa nawaambia kuwa watulie kwani kuna watu wana ndoto za mchana wanatumia nguvu nyingi, wanatumia muda wao bure na wanapoteza wakati wao,” alisema.

Rais Kikwete alitamba kuyatekeleza maazimio yote waliyoazimia moja baada ya lingine ili kuhakikisha wanayatimiza kwa wakati na kwa muda mfupi ili Watanzania kuendelea kujenga imani na chama hicho.

Alisema wajumbe wa NEC wanatakiwa kutumia muda wao mwingi kuifanya kazi ya chama ili kuweza kukijenga chama hicho kwa kiwango kikubwa.

NYOTA NDOGO AMESEMA HIVI KUHUSU YEYE KUWA MJAMZITO...

2:40:00 AM Add Comment
IKO HIVI JAMANI.......


Muimbaji wa nchini Kenya Nyota Ndogo amekanusha info na udaku ulioenea sehemu mbali mbali afrika Mashariki kuwa ni mjamzito.

Mama huyo wa watoto wawili na mwenye miaka 31 aligeuka kuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na madai kuwa anategemea kupata mtoto wa tatu.

Muimbaji huyo ambaye jina lake halisi ni Mwanaisha Abdallah alikiambia kituo kimoja cha radio mjini Mombasa kuwa, “Nimenepa tu na nipo kwenye hatua katika maisha yangu ambapo nimerelax. Ni mapema mno kwangu kuwa na mtoto wa tatu. Mtoto wangu wa pili ndio ana miaka miwili sasa.”

MNADA BANNER