Wapiganaji wasiopungua 30 wa kundi la Boko Haram wameuawa
kaskazini mwa Nigeria kufuatia mapigano baina yao na vikosi vya serikali ya
nchi hiyo.
Msemaji wa Jeshi la Nigeria Eli Lazarus ametangaza kwamba, mapigano
makali yamejiri baina ya vikosi vya serikali na wanamgambo wa Boko Haram katika
mkoa wa Yobe ulioko kaskazini mwa nchi hiyo ambapo kwa akali wapigani 30 wa
kundi hilo wameuawa.
Luteni Lazarus amesema kwamba, mapigano hayo yalidumu kwa
masaa kadhaa na kwamba, kamanda wa Boko Haram katika mji wa Damaturu ameuawa
katika mapigano hayo. Taarifa zaidi zinasema kwamba, mapigano hayo yalitokea
baada ya vikosi vya serikali ya Nigeria kuanzisha mashambulio dhidi ya eneo
moja mjini Yobe ambalo ni maficho ya Boko Haram.
Majeshi ya Nigeria
yamefanikiwa kuwatia mbaroni wapigani 10 wa Boko Haram katika mapigano hayo
sambamba na kugundua na kukamata silaha nyingi, imebainisha taarifa ya jeshi la
nchi hiyo.