IGP SAID MWEMA
Na Edwin Moshi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia Jonathani
Charles Naftari (26) mkazi wa kijiji cha Uruila baada ya kukamatwa na bunduki
ya kivita na risasi 37 ndani ya hifadhi ya Katavi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa katavi Dhahiri Kidavashari
aliwaambia waandishi wa habari kuwa mtuhumiwa alikamatwa hapo jana majira ya
saa 8:00 mchana katika eneo la Kalumbi ndani
ya hifadhi ya Katavi akiwa na Bunduki Sub-Machine Gun (SMG)yenye namba M22 – 13350 pamoja na risasi
37 zikiwa ndani ya magazine yake na risasi nyingine saba zilikuwa ndani ya
mfuko wa serikali.
Mtuhumiwa alikamatwa siku hiyo kufuatia msako mkali ambao
ulifanywa na askari wa jeshi la polisi kwa kushirikiana na askari wa hifadhi ya
kataviKidavashari alieleza kuwa mtuhumwa ambaye alikuwa na wenzake watatu
walipozungukwa na askari wa polisi na Tanapa na kutakiwa kujisalimisha
walikataa kutii amri hiyo na ndipo walipoanza kuwafyatulia askari risasi hovyo
kuwalenga askari
Ndipo askari walipojibu mapigo ya risasi na hatimaye
majangiri hao walianza kutimua mbio na askari kwa ustadi mkubwa walifanikiwa
kumkamata Jonathani na silaha hiyo ya kivita.Baada ya mtuhumiwa kukamatwa
alipekuliwa na kukutwa na risasi saba ndani ya mfuko wa saluari pamoja ana
panga na kisu ambacho kilikuwa na damu.
Kamanda Kidavashari alisema mtuhumiwa alipofikishwa katika
kituo cha polisi alidai kuwa silaha hiyo
ilikuwa ni mali yake na yeye na
wenzake waliingia ndani ya hifadhi kwa lengo la kuwinda wanyama.