REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MAHAFALI YA CBE : Wahitimu watakiwa Kujiajili

8:59:00 AM Add Comment


 Katibu mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi. Joyce Mapunjo akizungumza na wahitimu 2882 wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) wakati wa mahafali ya 47 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jana jioni Jijini Dar es salaam na kuwataka kutumia elimu yao  kujiajiri na kuwa chachu ya maendeleo nchini.




Kaimu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) Bw. Athman Ahmed  (kulia) akitoa taarifa kuhusu mahafali ya 47 na maendeleo ya chuo hicho kwa mgeni rasmi wa mahafali hayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi. Joyce Mapunjo (katikati).

 

Wahitimu wa mahafali ya 47 ya Chuo cha CBE wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa mahafali hayo katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam 


CONGRATULATION OUR BROTHER AWADH MNYIKA

8:27:00 AM Add Comment
Awadh Mnyika, Mhitimu wa Shahada ya Sayansi ya Kompyuta (Bachelor in Computer Science)

Dear Bro, 
Tunakupongeza sana kwa Kupata Stahili yako uliyoisaka Miaka Mitatu pale katika Chuo kikuu cha UDOM, Mkoani DODOMA. Pongezi zetu za Dhati kwa kuwesza kutimiza Ndoto zako.

Unapongezwa na Wazazi wako Bw. Kagoma Seleman Mnyika, na Bi. Paschazia Mnyika

Unapongezwa na Kaka ako Allawy Mnyika, Wadogo zako Frank M. Joachim, Ashura Mnyika, Johannes Magnus Joachim, Anajoyce Severine, Emannuel Busasaye (B-Kiss), Ndugu, Jamaa na Marafiki zako

Tunakutakia Mafanikio Mema katika Mishe zako.

R.I.P JOHN MAGANGA

8:04:00 AM Add Comment
                                                    Marehem John Maganga


                                                                    Waombolezaji





WATANZANIA WENZANGU NA WADAU WA FILAMU
Majira ya Asubuhi, Taarifa katika Mitandao mbali mbali zilidhihirisha kuwa Tasnia ya FILAMU nchini TANZANIA imempoteza Msanii wake mahiri, JOHN  MAGANGA, ambaye alikuwa akifanya Vizuri sana katika Soko linalokua kwa kasi hapa Nchini.

CHANZO
Kwa Mujibu wa Taarifa za Madaktari ambao walimfanyia Vipimo Marehemu, John amefariki kutokana na Ugonjwa wa KONGOSHO ambao umekuwa ukimsumbua
Awali ilidhaniwa kuwa Marehemu John alikuwa anasumbuliw na Vidonda vya Tumbo kabla ya Tatizo halisi kugundulika, ambapo mpaka jana asubuhi, hali ilibadilika na hatimaye kukimbizwa katika Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya matibabu

Aidha bado inaelezwa kuwa, mpaka hali inabadilika kiasi hicho, Marehemu alivimba tumbo, hali iliyopelekea kufanyiwa Upasuaji ili kuokoa Maisha yake.
Baada ya Tatizo hilo kubainika, Marehemu alikimbizwa Katika Hospitali ya Taifa ya MUHIMBILI kabla ya kupoteza Maisha yake Leo Asubuhi.

MSIBA UKO WAPI...
Msiba wa Marehemu John Maganga uko nyumbani kwao MWANAYAMALA na Tarifa za Mazishi Zitatolewa.

MOVIE ALIZOIGIZA MAREHEMU
1. MREMBO KIKOJOZI
2. CHANZO NI MAMA
3. BAR MAID

HONGERA AT kwa Kupata Ka- Baby Girl

7:43:00 AM Add Comment


Officially anaitwa Ally Ramadhan, but Nick namely anajulikana kama "AT". Pongezi kwake kwa Kupata Mtoto wa Kike ambaye bado kiujumla hajapatiwa Jina

"Nipo Nje Kikazi lakini Taarifa ninazo na ninamshukuru mwenyezi Mungu, kwani Mke wangu ameweza kujifungua bila matatizo."..alisema AT

VIONGOZI WA MAZIWA MAKUU WAKUTANA KAMPALA

7:25:00 AM Add Comment
KAMPALA, Uganda


Viongozi 10 wa nchi za eneo la Maziwa Makuu ya Afrika wanakutana leo mjini Kampala Uganda kwa shabaha ya kuujadili kwa kina mgogoro unaoendelea kutokota huko  mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 

Henry Oryem Okello  Waziri wa Nchi anayeshughulikia masuala ya kimataifa wa Uganda amesema kuwa, kikao hicho kitajikita zaidi kutafuta njia za kuutatua mgogoro huo unaoendelea kuumiza vichwa vya viongozi hao wa Kiafrika na jumuiya za kimataifa. 

Waziri Henry Oryem Okello ameongeza kuwa, kikao cha wakuu hao wa nchi za eneo watajadili mpango wa kutumwa kikosi cha wanajeshi elfu nne huko mashariki mwa Kongo kwa lengo la kupambana na waasi wa M23. 

Uganda ikiwa ni mwenyekiti wa mzunguko wa nchi 11 wanachama wa  eneo la Maziwa Makuu ya bara la Afrika, hivi karibuni ilikuwa mwenyeji wa Marais wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baada ya waasi wa M23 kuuteka mji wa Goma, makao makuu ya jimbo la Kivu Kaskazini.

MNADA BANNER