WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
EMINEM AZUNGUMZIA KITENDO CHA 50 CENTS KUONDOKA KATIKA LEBO YAKE.
KITENDO Cha 50 CENTS Kuondoka Shady
Records, Aftermath Entertainment na Iterscope Records, Zimewastua Wengi sana
ambao walikuwa wanafahamu uhusiano mzuri na wa karibu baina ya 50 Cents
Mwenyewe, Eminem na Dr.Dre.
Lakini baada ya Kutoa Taarifa
hapo jana Kuwa ameamua Kutemana na Kampuni hizo ambazo ndizo zimemtoa katika
Music Industry Ulimwenguni kote na Kufikia hapo alipo hivi sasa, Mmoja kati ya
Wamiliki wa Lebo hiyo ambayo ilikuwa ikimsimamia 50 Cents na kazi zake kwa Muda
sasa, EMINEM, amesema kuwa anajivunia Kumfahamu 50 Cents, na Kitendo cha yeye
kuondoka kwao, hakitaathiri Urafiki wao wa muda Mrefu.
Aidha Emenem ambaye pia
anafahamika kwa jina la Slim Shaddy, amesema Kuwa, yeye pamoja na SHADY RECORDS,
wanajivunia Kuwa sehemu ya Mchango wa Mafanikio ya 50 Cents katika Muziki.
Tofauti na hapo, Eminem aliongeza
kuwa, Kama isingekuwa uwepo wa 50 Cents katika Studio Hizo, basi hata Shady
Records isingekuwepo hapo Ilipofikia.
Kwa Upande wake 50, amesema kuwa
amekuwa na Muda Mzuri sana wakati akifanya kazi na Shady/Aftermath/ na
Interscope Records, huku akiwashukuru sana Dr. Dre na Eminem maana amejifunza
Mengi kutoka Kwao. Lakini hivi sasa anahitaji kwenda sehemu Nyingine na
Kujifunza Mtazamo Mpya.
50 Cents anaelekea katika Studio
za Caroline,iliyotokana na CAPITOL RECORDS.
Ingawa Hivi sasa anajiandaa
kushusha Albam yake Mpya ya THE ANIMAL AMBITION, Albam ya GET RICH OR DIE
TRYING ambayo ilikuwa na Mikwaju kama Vile IN DA CLUB, MANY MENT, P.I.M.P,
ilisukwa Vizuri na Lebo ambayo anatemana nayo
NDIO MWISHO WA SAUTI SOUL?..AU KUNA NINI KINACHOENDELEA
SAUTI SOUL Kutoka Nchini Kenya, Limekuwa ni
kundi ambalo wengi wamevutiwa nalo huku wao wakipata mafanikio makubwa sana
barani Afrika.
Kwa Mujibu wa Chanzo ambacho kilipiga Story na
Standard Media Nchini Humo, inasemekana kuwa, kuna uwezekano Mkubwa wa Memba wa kundi hilo kufanya Kazi za Peke yao,
yaani SOLO,ukizingatia hawajafanya hivyo kwa Muda Mrefu.
Ingawa Memba Wote wa SAUTI SOUL awali walikanusha uvumi kuwa kundi hilo
limevinjika, hivi sasa wamekuwa wawazi kuwa, kila memba atashiriki katika
Project yake Mwenyewe, ili kucheki uwezo wao, pamoja na Kupeana uhuru katika
baadhi ya kazi na uwezo wao nje ya Kundi.
DELVIN MUDIGI ambaye Pia ni Memba wa Kundi hilo,
amesema kuwa ameshiriki kazi mbali mbali za Kundi, lakini hivi sasa anatakiwa
kupima Uwezo wake hasa kimuziki, nje ya kundi, lakini Kundi bado Liko poa.
The same to POLYCARP FANCY FINGERS,
amedhihirisha kuwa Kundi bado lipo, na Still litazidi kuwepo, lakini kwa Hivi
sasa, wameamua kwa pamoja na kwa makubaliano, kufanya kazi za Pekeyao, hasa kwa
Kila Memba
LUDACRIS NDANI YA JANGA LA KIFEDHA, AMESHINDWA KUMHUDUMIA MTOTO WAKE.
WENGI Wanaweza Kujiuliza inakuwa Vipi Awe katika
Tatizo la Kiuchumi wakati mwaka Jana alikuwa katika List ya Orodha ya Forbes
kwa Rappers ambao wanaongoza kwa Mkwanja, lakini ukweli utabaki Pale pale.
TTM tumezinyaka kuwa inasemekana LUDACRIS
amevuna Dola za Kimarekani 55,000 sawa na Tshs Milioni 88 kwa Mwaka 2013, jambo
ambalo limemfanya kushindwa kumhudumia Mtoto wake
Kwa Mujibu wa maelezo yake wakati yuko
mahakamani alikoshtakiwa na TAMIKA FULLER, ambaye ni mama wa Mtoto wake wa Kike
mwenye Umri wa Miaka Miwili, Luda alikiri kuwa ni kweli hajamhudumia Mtoto wake
huyo ambaye anatakiwa ampatie Dola 15, 000 Kwa Mwezi , sawa na Tsh Milioni 24,
kwa ajili ya matumizi.
Pia Luda aliongeza kuwa alitarajia kuvuna
Mkwanja Mrefu kupitia Muvi ya FAST & FURIOUS 7, na kuliweka sawa hilo suala
la Kiasi hicho cha gharama za Mtoto, lakini mabo yalienda Ndivyo sivyo baada ya
kusitishwa kwa Muda Utengenezaji wa Muvi hiyo kutokana na Kifo cha PAUL WALKER
LUDA alisema kuwa hivi sasa anaweza kutoa Dola
18000 sawa na Tsh Milioni 2, na Elfu Themanini na nane.
Hakimu wa Kesi Hiyo, alimuamuru LUDA kulipa
gharama za Dola 7000 sawa na Tsh Milioni 11, na Laki 2 kwa ajili ya Matumizi ya
Mtoto huyo, wakati mahakama Ikipitia Taarifa zake za kifedha.
Kama utakuwa ni Mfuatiliaji mzuri wa Ludacris,
Hajawahi kuachia Albam Nyingine tangia Mwaka 2010, aliposhusha Albam ya BATTLE
OF THE SEXES
Subscribe to:
Posts (Atom)