REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

EXCLUSIVE : CHRIS BROWN AACHANA NA MPENZI WAKE KARRUECHE...KISA RIHANNA

1:13:00 PM Add Comment


HAYA SASA

Ngoma Ikivuma....ikavuma...vuuumu...vuuuumu...vuuuumu..Basi lazima ipasuke.
Hayo ndiyo yaliyojiri leo.
Baada ya Masikio mengi kuhamishiwa kwa Rihana na Chris Brown, hatimaye Chris Brown AMEMBWAGA RASMI mpenzi wake Karrueche Tran

Kwa Mujibu wa Maelezo ya Chris mwenyewew, amesma kuwa ameamua kumuacha Rasmi mpenzi wake huyo ili kuepuka kumuumiza zaidi
"Sitaki kumuona akiumia hasa kwa sababu ya Urafiki wangu na Rihana" 



Brown amedhihirisha hayo kwa Umma hasa juu ya kutengana na Tran baada ya kuonekana kuwa karibu sana na Rihana..
"nimeamua kuwa Single (Peke yangu) nikitazama na kuwa karibu na Fani yangu ya Muziki. Nampenda Karrueche sana, na kamwe sitaki kumuona akipata maumivu na wakati mgumu juu ya urafiki wangu na Rihanna" alisema Chris Breez

Mkali huyo wa "Look at Me Now" ameongeza kwa kusema:
" Ni bora nikawa Single ili sote wawili, mimi na Karrueche kuwa na furaha maishani Mwetu"

CHANZO CHA KIBUTI
Uamuzi huo wa Chris Brown umekuja rasmi baada ya Chris mwenyewe kuonekana katika Picha tofauti akiwa karibu sana na Rihana katika Tamasha lilifanywa na JAY Z huko Brooklyn, huku wakionekana kulala Hoteli Moja siku hiyo.


KARRUECHE KASEMAJE?
Kitu ambacho mpenzi huyo wa Chris Brown aliyebwagwa, ameonekana akipost katika ukurasa wake wa TWEETER kauli nzito sana
"BYE BABY" (Kwa Heri Mpenzi )




EXCLUSIVE : MARIAH CAREY- NIKI MINAJI AMETISHI KUNI-SHOOT

12:03:00 PM Add Comment



MAAJABU YA MUSA

Katika hali isiyo ya Kawaida, Msanii Mkongwe wa Muziki wa R & B na Jaji wa Kipindi cha AMERICAN IDOL, Mariah Carey, amesemakuwa Nicki Minaji amemtishia Kumpiga Risasi

Kwa Mujibu wa TMZ inasemekana kuwa Msanii huyo wa Kundi la YMCMB na Jaji wa Kipindi Hicho cha AMERICAN IDOL, amesema maneno hayo jana baada ya Kupishana Kauli kwa Muda Mrefu

KAULI YA NICKI MINAJI.....
Kwa Mujibu wa Maelezo ya Mariah Carey (MC), Niki Minaji ametoa Kauli hiyo baada ya kuondoka katika Jopo la Majaji waliokuwepo jana..
"aliondoka baada ya kupishana katika Maamuzi. lakini kama haitoshi, Zaidi ya watu watatu wamemsikia Niki akisema - Kama ningekuwa na Gun, ningempiga Risasi Huyo Mwanamke"
Alisema Mariah Carey huku akionekana kuwa na Hofu


KUHUSU KUOMBA RADHI KWA KAULI HIYO
Bibie Huyo Msariah carey ambaye pia ni Mke wa NICK CANNON, amsema kuwa, Licha ya Kutoa kauli hizo hatarishi, Bado Nicki Minaji hajaomba radhi kwake (Mariah), jambo ambalo linaonesha Kibuli balaa cha Mwanadada Huyo

HII KALI...

Aidha Mpaka Mida hii, Mariah Carey ameamua kutafuta Ulinzi Binafsi ili kuweza kuweka Maisha yake sala salimin baada ya kutishiwa kuuawa !!!!!

KWA UPANDE WAKE NICKI MINAJI
 Kwa upande wake Mkali wa Starship Nicki Minaji, amepost katika ukurasa wake wa TWEETER kuwa yeye hajali wala halaumu Mtandao wa TMZ na Mwandishi wa habari hizo, ila anajiamini yeye kama Yeye..
"Siilaum TMZ wala Barbara (Mwandishi). Ninasimama mimi kama mimi. Sihitaji na Sintohitaji Jeshi la Ulinzi. Mungu ni Mwema"

RAIS KIKWETE AKIWA CANADA

11:27:00 AM Add Comment
Rais Jakaya Kikwete akikagua Gwaride Nchini Canada, alipokuwa Katika Ziara ya Kikazi hapo Jana

Rais Jakaya Kikwete Akiwa katika Toroli la Farasi alipokuiwa Ziarani Canada hapo Jana

MAREKANI YAZIDISHA CHUKI DHIDI YA UISLAAM

11:23:00 AM Add Comment


Serikali ya Marekani kwa kupitia Mahakama ya Washington, inakusudia kuonyesha propaganda zilizo dhidi ya Uislamu katika mitaa na barabara za Washington, mji mkuu wa nchi hiyo.

Serikali ya Marekani imeeleza kuwa, mpango huo unasubiri hukumu ya mahakama ya Washington ambayo inatarajiwa kutolewa wiki ijayo. Propaganda hizo ziliwahi kuonyeshwa na kubandikwa kwenye vituo vya treni ya chini ya ardhi mjini New York wiki kadhaa zilizopita. 

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, propaganda hizo ambazo zimepewa jina la 'Kufeli kwa Jihad' zilisambazwa kwa makusudi mwezi uliopita mjini New York, na zimepangwa kuonyeshwa tena hivi karibuni mjini Washington baada ya kupatikana kibali cha mahakama ya jiji hilo. 

Takwa la makundi ya Kiislamu nchini Marekani la kuondoshwa propaganda hizo kwenye vituo vya treni za chini ya ardhi mjini New York, lilipelekea kuibuka misuguano mikali  kwenye vyombo vya mahakama vya eneo hilo, na kupelekea Jaji wa Mahakama ya Fideral kueleza kwamba hatua hiyo iko  sahihi kutokana na kuwepo sheria ya uhuru wa kujieleza. Inatarajiwa kuwa, faili hilo litachunguzwa zaidi kwenye mahakama ya Washington kabla ya kutolewa kibali cha kusambazwa propaganda hizo zilizo dhidi ya Uislamu.

"ISRAEL NDIO WANAONEZA UGAIDI DUNIANI"- RAIS WA IRAQ

11:18:00 AM Add Comment
RAis wa Iraq Jalal Talaban

Rais Jalal Talabani wa Iraq amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel ndiyo muenezaji wa ugaidi ulimwenguni. 

Rais wa Iraq amesema hayo mjini Baghdad katika mazungumzo yake na Brigedia Jenerali Ahmad Vahidi, Waziri wa Ulinzi wa Iran na kusisitiza kwamba, Israel ikiwa na lengo la kulinda maslahi yake na uwepo wake imekuwa ikieneza ugaidi katika Mashariki ya Kati. Rais wa Iraq ameashiria uhusiano mkongwe wa Iran na Iraq na kubainisha kwamba, kiwango cha uhusiano wa nchi mbili hizo ni imara na kisichoweza kutiwa dosari.

 Kwa upande wake Brigedia Jenerali Ahmad Vahidi, Waziri wa Ulinzi wa Iran amesifu ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tehran na Baghdad katika uga wa kiulinzi. 

Waziri wa Ulinzi wa Iran aliwasili jana mjini Baghdad kwa mwaliko wa Sadun Farhan al-Dulaymi, Waziri wa Ulinzi wa Iraq ambapo akiwa nchini humo tayari amekutana na viongozi mbalimbali wa nchi hiyo akiwemo Rais Talabani, Waziri Mkuu Noury al-Maliki na viongozi wengine wa ngazi za juu wa nchi hiyo.

KIMENUKA TENA LIBYA-WATU WENYE SILAHA WAUA ASKARI WATATU

11:11:00 AM Add Comment
Watu wenye silaha wamewaua polisi watatu katika kituo kimoja cha upekuzi na usalama mashariki mwa Libya. 

]Hayo yamethibitishwa na polisi ya Libya kwamba polisi hao wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana ambapo askari mwengine amejeruhiwa vibaya katika tukio hilo. Serikali ya Libya tayari imetangaza kuanzisha uchunguzi ili kuwajua wahusika wa mauaji hayo. 

Tangu ulipoangushwa utawala wa dikteta Muammar Gaddafi na hususan katika miezi ya hivi karibuni, askari wa ulinzi wakiwemo wa polisi na jeshi la nchi hiyo, wamekuwa wakikabiliwa na mashambulizi ya watu wenye silaha wanaosadikiwa kuwa na mahusiano na Kanali Muammar Gaddafi.

MNADA BANNER