WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
BAN KI MOON: BIASHARA YA MAGENDO YA BINADAMU
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka zifanyike juhudi
zaidi kwa shabaha ya kupambana na magendo ya binadamu ulimwenguni.
Ban Ki moon amesema kuwa, kuna udharura wa kuwepo
ushirikiano kati ya nchi, asasi na taasisi zote ulimwenguni kwa shabaha ya
kukabiliana na vitendo hivyo hatari kwa amani na usalama wa dunia.
Amesema
kuwa, magendo ya binadamu huharibu uchumi wa mataifa, kwani mapato ya mabilioni
ya dola yanayotokana na biashara hiyo haramu, hutumiwa katika muamala wa
kununua na kuuza madawa ya kulevya na jinai nyingine.
Kwa mujibu wa ripoti ya Ofisi ya Kupambana na Jinai na
Mihadarati ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa mwaka 2012, watoto wadogo
wanaunda moja ya tisa ya wahanga wa
magendo ya biashara ya binadamu ulimwenguni kote kati ya mwaka 2007 hadi 2010.
MALI: JESHI LAWAFUATA WAASI
Vikosi vya jeshi la Mali hii leo vimeelekea kwenye mji wa
kaskazini mashariki wa Kidal ikiwa ni kabla ya muda uliopangwa na serikali wa
kuukomboa kutoka katika mikono ya waasi wa Tuareg wanaotaka kujitenga
Vikosi vya Ufaransa vilivyokuwa vikipambana na waasi
kaskazini mwa Mali viliwaruhusu waasi wa MNLA kudhibiti mji wa Kidal katika
miezi ya hivi karibuni, lakini serikali ya Mali inataka kuudhibiti mji huo
kabla ya uchaguzi wa rais na Bunge unaotarajiwa kufanyika mwezi Julai. Waziri
wa Ulinzi wa Yamoussa Camara alisema bungeni mwezi huu kwamba, swali kuhusiana
na kudhibitiwa mji wa Kidal na waasi wa MNLA litajibiwa ifikapo Mei 15.
Waasi wa MNLA walikataa wito wa serikali ya Bamako wa kuweka
chini silaha, wakisema kuwa watakabiliana na jitihada zozote za serikali za
kudhibiti tena mji wa Kidal, lakini walisema mlango wa mazungumzo ya kisiasa na
serikali upo wazi.
Katika upande mwingine Rais wa Chad ametangaza kuwa, askari
wa nchi hiyo waliokuwa wakipigana nchini Mali na makundi ya waasi, wanaanza
kurejea nchini kwao.
KATUNI: HAYA BHANA.......
Bwahaaa haaa haaa nani kachora hii? twitter.com/JideJaydee/sta…
— Lady JayDee (@JideJaydee) May 13, 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)