George Kavishe kutoka TBL ambao ndio Wadhamini
wa tuzo hizi amesema
“‘Maboresho makubwa ambayo tumefanya mwaka huu
ni tofauti na mara zote ambazo tumekua tukihusisha Watanzania dakika za kupiga
kura tu hivyo wanakosa nafasi ya kupendekeza nani aingie kwenye category gani,
mwaka huu tumebadilisha kutokana na matakwa ya soko hivyo Watanzania ndio
watapendekeza nani aingizwe kwenye category gani. Kupitia Magazeti, website ya
Kilimanjaro na vipeperushi kuanzia kesho February 18 2014 kutaonyeshwa category
zote za mwaka huu za kupigiwa kura na Wananchi, Watanzania watatuma kura zao
kupitia simu ya mkononi kupitia 15440, unapendekeza msanii, kikundi au producer
gani aingie kwenye kipengele’’
‘’Kwa hiyo Mwaka huu Watanzania watapiga kura
mara mbili ambapo ya kwanza ni nani aingie kwenye category alafu tutarudi tena
kupiga kura nani awe mshindi wa kwanza, yani mwaka huu ile timu ya watu 100 ya
Waandishi, Watangazaji na wadau wa muziki kuchagua nani na nani aingie kwenye
category haitofanya hivyo bali itakutana kuhakikisha tu kama wimbo
uliopendekezwa na Wananchi ni wa mwaka husika, uko sehemu husika na pia kama
umekidhi vigezo vya kuingia KTMA’’ – Kavishe aliongeza
MABADILIKO KATIKA MWAKA HUU
Kwa mujibu wa Baraza la sanaa la Taifa (BASATA),
mabadiliko yaliyofanywa kwenye tuzo za mwaka huu wa 2014 ni kutokana na maoni
na mapendekezo ya wadau wa tasnia ya muziki kutoa sababu mbalimbali.
Mwaka huu KTMA itakua na category 36 ambapo category
34 ni za kuchaguliwa na mbili zilizobaki ni zile maalum za kuteuliwa.
Mwaka 2013 kulikua na category 37 ambapo Mwaka
huu imeondolewa moja kutokana na maoni mbalimbali ya wadau wa muziki ambapo
category yenyewe ni Mtayarishaji chipukizi wa mwaka.
Category zilizobadilishwa majina mwaka huu 2014
ni Mtumbuizaji bora wa kike wa muziki badala ya msanii bora wa kike ilivyokua
mwaka jana, mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki badala ya msanii bora wa kiume
mwaka jana, mwimbaji bora wa kiume Taarab ambayo mwaka jana ilikua msanii bora
wa kiume Taarab.
Mwimbaji bora wa kiume bongofleva badala ya
mwaka jana Msanii bora wa kiume bongofleva, mwimbaji bora kiume band ambayo mwaka jana ilikua msanii bora wa
kiume band, mwimbaji bora wa kike bongofleva badala ya mwaka jana msanii bora
wa kike bongofleva.
Mwimbaji bora wa kike Taarab badala ya mwaka
jana msanii bora wa kike Taarab, mwimbaji bora wa kike band badala ya msanii
bora wa kike band.
UPANDE WA BARAZA LA SANAA TANZANIA (BASATA)
BASATA katika maelezo yao, wamesema:
‘’kwa
nini kumekua na mabadiliko haya? ukiangalia maana halisi ya neno Msanii
linasadifu au linaleta maana za kuingia zaidi ya kitu kimoja, kunaweza kuwepo
na msanii wa uchongaji, msanii wa Uchoraji n.k kwa sababu wanafanya kazi ya
sanaa ndio maana tunatumia majina ya kimuziki kwa sababu huku tuko kwenye
muziki’
PIA Wakaongeza ‘ ‘mwaka huu tutakua na video
bora ya muziki ya mwaka badala ya video bora ya wimbo, neno muziki lina uwanja
mpana kuliko wimbo…….. pia tutakua na wimbo bora wa Afropop badala ya wimbo
bora wa bongopop, kutakua na wimbo bora wenye vionjo vya asili ya kitanzania
badala ya wimbo bora wenye vionjo vya asili.Jingine ni Msanii bora chipukizi
anaeibukia badala ya msanii bora anaechipukia…. wapo wasanii wengi sana
chipukizi huko mtaani na miziki yao haijasikika, inawezekana amekaa miaka mingi
akifanya kazi zake lakini akaibuka na ameonekana’’