REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

HATA WEWE UTAPIGWA NA BUTWAA KATIKA HILI!!!!

5:16:00 AM Add Comment


                                      Kim Kardashian na Kanye West katika matukio tofuti.

Na Frank M. Joachim


HATA WEWE UTAPIGWA NA BUTWAA KATIKA HILI!!!!

Mwanamitindo Kim Kaedashian ambaye ni mpenzi wa Kanye West, anasema anajivunia kutungiwa Wimbo unaokwenda kwa Jina la “PERFECT BITCH”(Kwa tafsiri ya Street American language, BITCH ni MALAYA, mwanamke asiye na uaminifu Fulani Hivi), na amevutiwa saaana na Track hiyo
Ninajivunia kupewa Heshima hiyo, na Ninaupenda sana Wimbo huo pamoja na Title lake. Ninajua hana maana au tafsiri mbaya napokuwa anatamka neon BITCH” alisema Kardashian.

Siku ya jana Kanye west katika Ukurasa wake wa “Tweeter” kuwa “Nimeaandika wimbo wa PERFECT BITCH kuhusu Kim Kardashian, lakini kitu cha kushangaza, Tweet ile ilifutwa hapo baadaye.
                                                  Tweet aliyo post Kanye West ktk ukurasa wake wa Tweeter

Cha ajabu ndo hicho, ambapo Kim Kardashian anajivunia huku akisema
“Wimbo unazungumzia namna ambavyo alikutana (Kanye West) na kuwa na mahusiano na wasichana Wengine wengi, ila hakuweza kumpata msichana sahihi na madhubuti mpaka alipokutana na Mimi
Na pia, Kim amevutiwa Mno na jinsi ambavyo Kanye West alivyouchanganua Mwili wake (Kim Kardashian mwenyewe) katika Mistari ya Song Hilo ambalo halijaachiwa
Kim is also real pleased about the way Kanye describes her body in the song.

Beyonce na Jay Z....hii ni kufuru aisee

5:09:00 AM Add Comment


Beyonce na Jay Z
Na Frank M. Joachim
Baba na Mama Blue Ivy, maarufu kama Jay Z na Beyonce, wameonekana kuwa Vinara si katika Mahusiano yao tu, bali hata katika Nguvu kubwa ya U-Star
Kwa mujibu wa Forbes ya Mwaka huu, orodha ya Couples ambao wanalipwa Mkwanja mrefu saaaana katika Mishe zao aza kila day, Wanandoa hao wameshika nafasi ya juu kabisa, yaani nafasi ya kwanza baada ya kulipwa Dollar za Ki-obama (USD) milioni 78 ($78 Millions) kwa mwaka 2011
Hata hivyo kali zaidi ni kwambaaaaaaaaa?
Beyonce anaonekana kumfunika mumewe katika malipo baada ya kuingiza kiasi cha $ Milioni 40 huku Jiga akiingiza $ Million 38.
Wengineo katika nafasi za juu ni
·         Gisele Bundchen na Tom Brady, wamevuna $72 million. (Nafasi ya Pili)
·         Victoria na David Beckham wamevuna  $54 million (Nafasi ya Tatu)
Kibongo bongo nani Couple gani inafunika?
Kazi ipo……..

Naibu Waziri alivyopata ajli katika eneo la Tumbi Kibaha

4:24:00 AM Add Comment



wananchi wakiwa katika ajali hiyo

gari la naibu waziri likiwa limepinduka
                                                            msamalia mwema kitoa msaada
mheshimiwa akiwa amejeruhiwa


 Naibu waziri wa Afrika Mashariki,Abdullah Juma Abdalla Saddallah na familia yake, wamekumbwa na  ajali mbaya eneo la Tumbi Kibaha wakati akitoka Bungeni.

Ajali hiyo mbaya ilitokea majira ya jioni hii wakati naibu waziri huyo akitokea Bungeni kuelekea jijini Dar es salaam akiwa na mkewe pamoja na watoto wake wawili sanjari na  dereva wake ambaye amejeruhiwa vibaya katika ajali hiyo na kukimbizwa hospital yaTumbi-Kibaha.
Kwa Mujibu wa Mashuhuda wa ajali hiyo akiwemno imesemekana  kuwa chanzo cha ajali hiyo Lori, ambapo dreva wa Kiongozi huyo alikuwa akijitahidi kupishana  nalo , hali iliyosababisha gari lake kuacha barabara na kupinduka .
Shukrani za dhati ziwafikie wananchi ambao walikusanyika katika eneo la tukio, katika jitihada za dhati za kuwazuia Vibaka kutokuiba mali yoyote katika Gari hilo.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Nchini, Kamanda Mohamed Mpinda, amethibitisha  kutokea kwa ajali hiyo
“Hali ya naibu waziri huyo si mbaya sana zaidi ya dereva wake ambaye ameumia kichwani." Alisema Kamanda Mpinga


Watanzania tutazame hapa....halafu tujiulize....

3:42:00 AM Add Comment


viti vipya vya jengo jipya la bunge nchini kenya. viti hivi vimetengenezwa na kitengo cha magereza nchini humo

Na Frank M. Joachim


Bunge la Kenya lililokarabatiwa na ambalo limekuwa gumzo kubwa kwa sababu ya gharama ya viti vya bunge hilo, hatimaye limefunguliwa rasmi na rais wa nchi hiyo Mwai Kibaki.

Viti hivyo vimegharimu dola 3,000 za kimarekani kwa kila kiti kimoja vikiwa jumla ya 350 vimetengenezwa na kitengo cha magereza nchini humo.

Zabuni ya kwanza ya kutengeneza viti hivyo ilitolewa kwa kampuni moja ya nje lakini ilifutwa baada ya baadhi ya wabunge kugundua kila kiti kingegharimu dola 5000 za kimarekani.

Maafisa wanasema ukarabati huo uliogharimu dola milioni 12 utaliweka bunge katika mfumo mpya wa kisasa wa komputa.

Je, sisi viti vyetu vilitengenezwa na kitengo kipi....hapa nchini

15 wapoteza maisha.

3:34:00 AM Add Comment



Wakazi wa ufilipino wakiwa katika paa za nyumba zao, baada ya mafuriko.


Timu ya waokoaji katika shughuli zao nchini ufilipino

Na Frank M, Joachim
Mafuriko makubwa yamewaua watu wapatao 15 nchini Ufilipino. Mafuriko hayo yanaelezwa kuwa mabaya kabisa kuwahi kuimbuka nchi hiyo tangu mwaka 2009, huku maji yakifikia urefu wa mita moja unusu katika mji mkuu, Manila. Makazi yalifunikwa na mafuriko hayo huku yakisababisha maporomoko ya tope. Maelfu ya wakaazi wamelazika kuzikimbia nyumba zao, lakini wengi bado wamekwama. Kampuni za umeme zimekata huduma za umeme baada ya maji kuingia katika mitambo ya umeme, hivyo kuuacha mji wa Manila bila umeme. Kwa mujibu wa idara ya utabiri wa hali ya hewa, mafuriko hayo yalisababishwa na upepo mkali na mvua kubwa zilizonyesha nchini humo wiki iliyopita.

WANAJESH WAWILI WAUAWA

2:59:00 AM Add Comment

WANAJESHI WA NIGERIA


RAIS WA NIGERIA, GOODLUCK JONATHAN

 Wanajeshi wawili wamepigwa risasi na kuuwawa na washambuliaji walioufyetulia risasi msafara wao katika mji wa Okene katika jimbo la Kogi nchini Nigeria. Msemaji wa polisi katika jimbo hilo ameliambisha shirika la habari la AFP kuwa wanashuku mauaji hayo yamefanywa na wanaume waliowaua waumini wasiopungua 19, katika kanisa moja la Kiinjili katikati mwa Nigeria. Hapo jana maafisa walisema waumini hao waliuwawa wakati wanaume waliokuwa wamejihami na bunduki walipolivamia kanisa hilo na kukata umeme kabla kuanza kufyetua risasi wakati giza lilipotanda ndani ya kanisa hilo. Mashambulizi ya jana ni mfululizo wa hivi karibuni wa mashambulizi ya risasi na mabomu dhidi ya Wakristo nchini Nigeria.

IRAN KUMPA SHAVU BASHAR AL ASSAD

2:55:00 AM Add Comment


RAIS WA IRAN MOHAMMED NEDJAD



Iran imeahidi kumsadia rais wa Syria, Bashar al Assad huku vikosi vyake vikiendelea kukabilian ana waasi katika mji wa kaskazini wa Aleppo. Kiongozi wa baraza kuu la usalama wa kitaifa la Iran, Saeed Jalili alikutana jana na rais Assad mjini Damascus, ambapo alisema Iran haitoruhusu ushirika wake wa karibu na utawala wa Syria uyumbishwe na machafuko yanayoendelea nchini humo au na maadui kutoka nje. Rais Assad ameapa kuendelea kupambana na waasi wa Syria bila huruma. Imeripotiwa kwamba vikosi vya Assad vinauzingira mji wa Aleppo.

MNADA BANNER