WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
NEW VIDEO : SNURA in "SHOGA AKE MAMA"
Nah Aboud Jr.
IKO HIVI MAZEE.....
Finaly ile Video mpya iliyokuwa ikizungumziwa kwa saaaaana na Mkali wa FILAMU hapa Area 255, SNURA, Hivi sasa Iko Tayari.
Kwa Mujibu wa Dar Talk, Snura amesema Video Hiyo itakayokwenda kwa jina la "Shonga ake Mama", itaanza Kuonekana Muda Si Mrefu.
TIRIRIKA MAMA...
"Video imetoka sasa, na Mashabiki wangu wataiona muda si Mrefu. Kikubwa Malengo yangu ni kufanya kitu tofauti, na Baada ya kazi Hiyo kwenda hewani, nitaanza show za Kuitambulisha ili iweze kupokelewa Vizuri"
MISRI YAAHIDI KUTANGAZA VIVUTIO VYA KITALII VYA TANZANIA
Marwa Tawfik (Kulia) mmoja wa wajumbe waliowakilisha vyombo
vya habari nchini Misri kuja Tanzania kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii
akifafanua jambo kwa wajumbe wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na waandishi wa
habari (hawapo pichani) juu ya kile walichojionea walipofanya ziara katika
vivutio mbalimbali vya utalii Tanzania Bara na Zanzibar.Wengine ni baadhi ya
wawakilishi kutoka Misri.
**************************************************
DAR ES SALAAM
DAR ES SALAAM
VYOMBO vya habari nchini Misri vimeahidi kutangaza vivutio
mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini katika kuhakikisha Tanzania inapata
watalii wengi zaidi jambo litakaloendelea kudumisha mahusiano mema yaliyopo
kati ya nchi hizo.
Hayo yalisema Dar es Salaam juzi na mmoja wa wawakilishi wa
vyombo vya habari nchini Misri, Marwa Tawfik alipozungumzia ziara waliyofanya
katika vivutio vya utalii nchini ambapo waliahidi kutumia vyombo vyao kutangaza
walivyoviona.
Ujumbe wa watu sita uliowakilisha vyombo mbalimbali vya
habari nchini Misri yakiwemo magazeti na televisheni chini ya Ofisa wa Ubalozi
wa Tanzania nchini humo Jestas Nyamanga walifanya ziara ya siku tano nchini
kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii Tanzania Bara na Visiwani chini ya
uratibu wa Bodi ya Utalii nchini (TTB).
Alisema wanaporudi nchini kwao watakaa na uongozi wa vyombo
vyao na kuangalia jinsi ya kupata vipindi maalumu katika televisheni na makala katika magazeti
jambo litakalowezesha taarifa za utalii za Tanzania kuwafikia watu wengi zaidi
nchini mwao na nchi nyingine za ukanda huo.
Tawfik alisema ana imani ziara hiyo pamoja na kazi
watakayoifanya ya kuvitangaza vivutio husika itasaidia Tanzania kupata watalii
wengi zaidi kutoka nchini mwao na katika nchi za ukanda wa kiarabu. “Tumeona
utajiri wa asili wa ajabu uliopo Tanzania,sisi tunaahidi kutumia vyombo vyetu
kutangaza vivutio hivi katika kuhakikisha watu wengi zaidi wanahamasika kuja
Tanzania na hatimaye kuwaongezea pato lenu kupitia utalii,” alisema Tawfik.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TTB Aloyce Nzuki
alisema ziara hiyo pamoja na nyingine ni muendelezo wa jitihada za bodi hiyo ya
kuhakikisha sekta ya utalii inakua ndani na nje ya nchi.
Alisema ujio wa ujumbe huo kutoka Misri utaongeza idadi ya
watalii kutoka nchi hiyo pamoja na nyingize za ukanda huo ambapo takwimu za
sasa zinaonyesha Tanzania inapata watalii 25,000 kutoka nchi za ukanda huo.
Nzuki alisema pamoja na ujumbe huo kuahidi kutumia vyombo
vyao kutangaza walivyoviona pia bodi hiyo inaendelea na jitihada za kuhakikisha
matangazo ya vivutio vilivyopo nchini yanawekwa katika lugha ya Kiswahili
katika kukuza utalii wa ndani.
“Tumekuwa na jitihada endelevu za kuhakikisha vivutio
tulivyonavyo vinajulikana ulimwenguni kote jambo litakalosaidia kupata watalii
wengi zaidi kutoka nje lakini pia tunaendelea na jitihada za kuhakikisha utalii
wa ndani unakua,” alisema Nzuki.
HII NDIYO SABABU ILIYOSABABISHA DIAMOND PLATNUM KUPATA AJALI MBAYA....
Na Frank Magnus Joachim. DSM
FUNGUKA PLATNUM...
"Tarehe 10 ya mwezi wa 11 siku ya juma mosi ni moja ya siku
ambazo sitozisahau maishani mwangu.
Baada ya kumaliza majukumu yangu ya kila siku, nilikwenda
masaki kumwona mmoja wa jamaa zangu wa karibu nikiwa na Blogger wangu Bestizzo
pamoja na mwanafamilkia ya wasafi Dumi(Dancer) Mishale ya saa moja hivi nikiwa
maeneo ya masaki karibu na kona ya msasani nilipata ajali ambayo haikuwa kubwa
sana ingawa imesababisha uharibifu kwa kiasi kikubwa, Kama mjuavyo barabara ya
msasani ni ndogo na gari huwa haziko katika mwendo wa kasi... ghafla dereva wa
pikipiki alikatisha mbele yangu na katika kujaribu kumkwepa nikagonga gari
ndogo aina ya Rav 4 ambapo ilisababisha dereva wa pikipiki kuanguka katikati ya
gari zote mbili. Hiyo ndio hali halisi ya ajali niliyokutana nayo jumamosi
iliyopita.
Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutunusuru wote bila
majeraha makubwa zaidi ya maumivu tu ya hapa na pale."
MTOTO ALIYEFANYIWA UKATILI NA MAMA YAKE MDOGO NA KULAZIMISHWA KULA KINYESI CHAKE...AKATWA MKONO
Na Nah Aboud Jr,
MAJENGO,MBEYA
HALI IKO HIVI.......
MTOTO aliyejulikana kwa jina moja la Aneth (pichani)
anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka miwili, mkazi wa eneo la Majengo Kaskazini
jijini Mbeya ameunguzwa vibaya mwili wake na kulazimishwa kula kinyesi na Mama
yake Mdogo aliyejitambulisha kwa jina la Revina.
Tukio hilo la kikatili liligundulika juzi eneo hilo majira
ya saa tano asubuhi ambapo mwandishi wa habari hizi alifika eneo la tukio na
kuukuta umati wa watu na mtuhumiwa akimuogesha mtoto huyo.
MTOTO MWENYEWE ANSEMAJE?
Mtoto huyo alipoulizwa kuwa ilikuwaje, aliongea kwa woga
akisema kuwa alikuwa amefungwa mkono na kumwagiwa maji na kupigwa.
DAH....MAMA MDOGO ALIYEFANYA UKATILI HUO NAYE AKAWA HIVI
Mtuhumiwa huyo alipohojiwa alikataa kusema chochote na
kuishia kutaja jina lake moja la Revina, kisha wananchi wakaamua kumchukua mtoto
huyo na mtuhumiwa na kuwapeleka kituo cha Polisi cha Kati.
MASHUHUDA JE?
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa baada ya kutomuona
mtoto huyo mwenye historia ya kuteswa na mama yake huyo mdogo anayeelezwa kuwa
mama yake mzazi, Bahati Mkandara alifariki, wakaamua kumuuliza binti huyo
ambapo aliwajibu kuwa mtoto huyo alikuwa kucheza na walipompiga ndipo akaamua
kukimbilia chumbani na walipoingia wakamkuta mtoto amesimama akiwa uchi.
SERIKALI IKO WAPI?.....
Kwa upande wake, Mwenyekiti
wa Mtaa wa Majengo Kaskazini, Shack Mwakanyamale alisema kuwa binti huyo
amezoea kumtesa mtoto huyo huku mtoto wake akiwa na afya njema ambapo
aliwatuliza wananchi wenye hasira kali na kuongoza msafara wa kumpeleka katika
kituo cha polisi mtuhumiwa huyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)