Na Baba Juti
#WatuWaMungu Beef la 50 Cents na master P linazidi kuchukua nafasi ya pekee hasa baada ya majibu ya hapa na pale baina ya Rappers hawa wawili
Awali iliwahi kuibuka inf kuwa , Master P amekuwa akikwazwa na namna ambavyo 50 Cents anaongea upuuzi hasa juu yake, kitu ambacho kiliamsha Hisia za Wengi
Lakini miaka kama miwili iliyopita, Master P alidai kuwa yeye ndiye aliyelipia TOUR ya kwanza kabisa ya Rapper 50 Cents, licha ya dharau anazozidi kuonesha juu yake na wengine, bado kamsamehe.
Katika hatua Nyingine, inasemekana kuwa, Master P ndiye alikuwa mtu wakwanza kabisa kuonesha kila aina ya Support kwa Hit maker huyu wa I GET MONEY hasa katika album yake ya Get Rich Or Die Trying.
Sasa, mapema safari hii, Master P ameibuka na kusema kuwa, Ujinga anaoufanya 50 Cents kwa ajili ya kutafuta Kick, basi unaua sana Soko la Rap, maana hata kama unahitaji kuuza kitu, haina ulazima kufanya Vitu kama hivyo ambavyo vinaonekana ni vya kitoto.