SERIKALI
Ya Nchi ya Rwanda, Imekanusha Kutokea Kwa Kifo cha Rais wa Nchi Hiyo PAUL
KAGAME, kama ambavyo Uvumi Ulikuwa Umeshaanza Kuzagaa Maeneo Mbali mbali Ya
Afrika.
Kanusho
hilo limetoka muda Mchache Baada ya Kusikika Kwa Shangwe na Chereko Katika
Mitaa ya Mji wa Goma ulioko Jamhuri ya Kidemokrasia ya KONGO, Huku Baadhi ya
watu Wakishangilia kwa nguvu zote huku wakiwa wameshikili Bango Lenye Umbo la
MSALABA, lililoandikwa R.I.P KAGAME, yaani PUMZIKA KWA AMANI KAGAME
Lakini
AFISA na Msemaji Mkuu wa OFISI Ya Rais Paul kagame, alithibitisha Kuwepo kwa
Uvumi huo, na kukanusha Kuwa, Hakuna Ukweli wowote juu Hilo, Rais Kagame Yuko
hai, na Yuko Nchini Marekani katika Ziara ya Kikazi, na alitakiwa kukutana na
wanafunzi ambao ni Raia Wa Rwanda wanaosoma Nchini Marekani.
Katika
Kukazia Hilo, WAZIRI MKUU Wa Rwanda naye alitweet Kywa Rais Kagame hajafariki,
yuko Salama na Mzima wa Afya, huku akisisitiza kuwa Kitendo Kilichofanywa na
Vijana hao ni UCHAFU na UPUUZI Mtupu, Ukizingatia Nchi Ya RWANDA na DRC haiku katika
mahusiano Mazuri ya Kisiasa.
Baada
ya Kanusho hilo Pia, serikali ya Rwanda Ilitweet Picha ya rais kagame akipeana
mikono na Raia wa Rwanda wanaosoma katika Chuo Cha PENNYSLAVIA kilichoko nchi
marekani, kama uthibitisho wa Taarifa za Uwongo dhidi yake