AHSANTENI SANA KWA UKARIMU WENU : Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na maafisa mbalimbali wa ubalozi wa Tanzania
Nchini Ethiopia katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa
jana jioni ya Februari 24, 2013 baada ya kuhudhuria hafla ya Utiaji saini
Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Rais Kikwete, kabla ya kurejea Dar es salaam leo,
alikwenda Uganda kuhudhuria mazishi ya baba mzazi wa Rais Yoweri Kaguta
Museveni, Mzee Amos Kaguta, aliyefariki siku ya Ijumaa na kuzikwa kijijini
kwake
KWA HERI MHESHIMIWA..KARIBU TENA : Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Profesa Joram M. Biswaro
akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Balozi Naimi Aziz (kati)
na Afisa ubalozi Samwel Shelukindo wakipungia kumuaga Rais Kikwete wakati ndege
yake ikiondoka uwanjani hapo leo jioni ya
Februari 24, 2013.
Picha na IKULU
EmoticonEmoticon