REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

DR. ULIMBOKA IS BACK !!!!!!!!!

11:15:00 AM Add Comment
Na Frank Joachim

"Mbona Hatokelezei?.....na Hatuondoki Kudadadeki...Labda sisi sio Wanahabari"

"Dah...Bongo pako vile vile...Siamini kama nimerudi napumua...Hivi hapa ndo nilipitishwa wakati naumwa?...hata sikupaona"

"Msijali wapendwa...naombeni nipite Kimtindo....ntawapa Story tu...msijali...najua ndo Njaa yenu"

"Okay...Nihoji basi....nakusikiliza swahiba...Enheee"

"Thank yuuu....Thenki Yuuu...Let me go home now....nimeimiss Familia yangu...Theeeenk Yuu"
Picha Kwa Hisani ya Global Publishers..(Samahani, Maneno hayo ni ya Kubuni Tuu...Hakuna ukweli wowote"

TEMBO WAVAMIA KIJIJI, NA KUUA MTU MMOJA WILAYANI ROMBO

10:51:00 AM Add Comment




ROMBO, KILIMANJARO


ZAIDI ya Tembo tisa wamevamia kijiji cha Mahida Mangoni wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, na kuua mtu mmoja na kujeruhi pamoja  na kuharibu mazao ya migomba.

Mkuu wa wilaya hiyo Elinasi Pallangyo alisema tembo hao waliigia kjijini hapo na kuanza uharibifu huo haliiliyopekea wananchi kuanza kuwafukuza na hatimae tembo hao kuua mtu mmoja pamoa ja kujeruhi.

Alisema baada ya tembo hao kuua wananchi mmoja na kujeruhi, wananchi hao waliwashambulia tembo hao na kuua tembo mmoja.

Mkuu huyo amewataka wananchi wilayani humo kutosumbua wanyama hao pindi wanapoingia ndani ya wilaya hiyo na badala yake kutoa taarifa kwa vituo vya askari vya  wanyama pori vilivyopo wilayani humo.

Kamanda  wa polisi mkoani hapa Robert Boaz amethibitisha kutokea kwa kutukio hilo na kwamba lilitokea agusti 10 mwaka huu majira ya saa 8:00 mchana na ambapo tembo hao walisababisha kifo cha Veronica John (44) na kumjeruhi vibaya Stiven Shirima.

Boaz alisema marehemu alikuwa shambani akiwa anajishughulisha na shughuli za kilimo ambapo tembo hao walimkanyagakanyaga sehemu mbalimbali za mwili  pamoja na kuchumwa na pembe mbavuni upande wa kushoto.

Kamanda huyo alisema hali hiyo ilimfanya  avuje damu nyingi hali iliyopelekea kupoteza uhai na kwamba majeruhi wanapatiwa matibabu katika hospitali ya huruma huku mwili wa marehemu ukiwa umehifadhia katika hospitali hiyo.

MTOTO AUAWA BAADA YA KUPIGWA FIMBO NA BABA YAKE MZAZI

10:46:00 AM Add Comment
IGP SAID MWEMA


TARIME, MARA


MTOTO mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja ameuwawa baada ya kupigwa fimbo kichwani na baba yake mzazi Migengo Mseti (68) Mkazi wa Kijiji cha Nyakunguru kata ya Kibasuka Wilayani Tarime.

Kamanda wa Mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya Justus Kamugisha alithibitisha kutokea kwa tukio hilo nakwamba lilitokea Agosti 8 majira ya saa 10.30 jioni kitongoji cha Turuturu kijiji cha Nyakunguru ambapo mtoto aitwaye Buyuri Mseti aliuwawa.

Kamanda Kamugisha alisema kupigwa kwa mtoto huyo kulitokana na sababu za ugomvi kati ya baba na mama yake Magreti wakati baba huyo akimpiga mke wake alikuwa amebeba mtoto mgongoni na kwamba wakati baba akijaribu kumpiga mke wake kwa fimbo mama huyo alikwepa fimbo na ndipo ilipompata mtoto Kichwani na kumsababishia kifo papo hapo.

Kamugisha aliongeza kuwa mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi tayali kwa mazishi nakwamba mtuhumiwa amekamatwa na yuko chini ya ulinzi na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.

ASHAMBULIWA NA FISI....

10:42:00 AM Add Comment




SERENGETI, MARA.

Mkazi mmoja wa kijiji cha Gentamome wilayani Serengeti mkoani Mara, amejeruhiwa vibaya katika sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya kushambuliwa na fisi aliyevamia nyumbani kwake.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho cha Gentamome Bw Elisha Sinda,amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Agosti tisa mwaka huu.

Amemtaja mwananchi huyo kuwa ni Bw Juma Kurate ambaye mbali na kujeruhiwa katika sehemu hizo za mwili wake pia fisi hiyo alimnyofoa kidore gumba cha mkono wake wa kushoto.

Bw Sinda,amesema baada ya fisi huyo kuvamia nyumbani kwa mwananchi huyo kwa lengo la kukamata mbuzi ndipo walipopambana na makazi huyo kabla ya kumjeruhi na kukimbia na kidore hicho kabla ya kuuawa katika msako mkali uliofanywa na wananchi wa kijiji hicho.

Kwa sababu hiyo mwenyekiti huyo wa kijiji,ameiomba idara ya wanyamapori wilayani Serengeti kuendesha msako dhidi ya fisi hao ambao amesema wamekuwa kero kubwa kwa wananchi kutokana na kupora kila wakati mifugo ya wananchi lakini licha ya kutoa taarifa katika idara hiyo hakuna hatua ambazo zimechukuliwa.

WANAHABARI HILI LENU......

10:34:00 AM Add Comment

Dr. Christine Ishengoma




Na Edwin Moshi.
IRINGA


Mkuu wa mkoa wa Iringa DKT Christine Ishengoma amewataka wanahabari kulisaidia Taifa katika zoezi la sensa ya watu na makazi kwa kuendelea kuhamasisha wananchi kujitokeza katika zoezi hilo.

Mkuu huyo wa mkoa ametoa Rai hiyo leo katika ukumbi wa Ruco mjini Iringa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili ya wanahabari kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini pamoja na mkoa wa Lindi na Mtwara.

Alisema kuwa zoezi hilo la sensa ya watu na mkazi lina nafasi kubwa katika Taifa ili kuwezesha kupanga bajeti kulingana na mahitaji sahihi ya wananchi wake,hivyo kuwataka wanahabari hao kusaidia kutoa elimu zaidi kwa umma .

Hivyo alisema kuwa ni wajibu kwa wanahabari kuelimishwa zaidi juu ya zoezi hilo litakavyofanyika Kama njia ya kuwezesha Taifa kufanikisha zoezi hilo.

Alisema kuwa vyombo vya habari ni miongoni mwa wadau wakubwa ambavyo vinategemea zaidi Takwimu katika kufikisha ujumbe kwa Taifa hivyo ili zoezi hilo liweze kufanikiwa lazima kuwepo na ushirikiano mkubwa kutoka kwa vyombo hivyo vya habari.

DKT Ishengoma alisema kuwa hadi kufikia siku ya zoezi hilo la sensa ni siku 13 ndizo zilizosalia hivyo ni matumaini ya serikali kuona siku zilizobaki zinatumika vema katika kufikisha taarifa kwa wananchi.

Alisema kuwa sensa ya watu na makazi ni zoezi ambalo limekuwa likifanyika kila baada ya miaka 10 hivyo lazima umma kujulishwa ili kujitokeza kwa wingi katika zoezi Hilo.

Mkuu huyo wa mkoa alishauri wakuu wa kaya kuweka kumbukumbu sahihi ambazo zitawezeshwa makalani wa sensa kupata taarifa zilizo sahihi katika kufanikisha zoezi Hilo.

JELA KWA KUJARIBU KUMUZA MTOTO

10:21:00 AM Add Comment

sumbawanga


Na Edwin Moshi.
Sumbawanga, RUKWA..

Mkazi wa kijiji cha Ulumi tarafa ya mwimbi wilayani sumbawanga katika mkoani Rukwa Issack Lunguya (40) amehukumiwa kifungo cha miaka 2 jela ,sanjari na kulipa faini ya 2,000,000/=kwa kosa la kujalibu kumuuza mtoto wa jirani yake ili akatumikishwe kazi za ndani bila ridhaa.

Mwandishi wa habari hizi  anaripoti kutoka Sumbawanga kuwa ,Adhabu hiyo imetolewa katika mahakama ya Hakimu mkazi mjini Sumbawanga wakati hakimu wa mahakamani ya hakimu mkazi Rozalia Mugissa baada ya kuridhishwa na ushaidi wa upande wa mashtaka katika kesi hiyo iliyoongozwa na mwendesha mashtaka wa polisi Assistant Ispector Emmanuel Shani.

Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha mashtaka Mkaguzi Msaidizi wa Polisi
kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo 07,08 mwaka huu,amapo alikamatwa febr 21/2012 saa nne asubuhi huko ulumi alipokuwa katika harakati za kumuuza mtoto huyo mwenye umri(14)kwa mfanyabiashara mmoja ili asafirishwe kupelekwa mjini sumbawanga tayari kwa kwenda kufanya kazi za ndani.

Shani aliendelea kuileza mahakama hiyo mbele ya Hakimi Mkazi wa Rosaria Mugissa kuwa siku ya tukio mshtakiwa, kabla ya hapo kulikuwa na taarifa za siri kwamba mtuhumiwa, alikuwa akitafuta mteja wa kumuuzia mtoto huyo ambaye ni jirani yake ile hali ni yatima kwa kiasi cha 2,000,000, alimvizia binti huyo akitoka nje kwenda kujisaidia.


Aliendelea kuielezea mahaka hiyo kuwa uliandaliwa mtego kwa kumtumia mtendaji wa kijiji hicho na hatimaye mwanaume huyo akanaswa akiwa amemleta mtoto huyo sokoni huku akiwa anamdanganya kuwa anaenda kumtafutia kazi nzuri ya kuuza duka.

Hakimu Mugissa alisema kuwa ameridhishwa pasipo kuwa na shaka kwani ushahidi,watu watatu akiwamo binti huyo aliyetaka kuuzwa ambaye aliielezea mahakama kuwa yeye ni yatima na hasomi shule kutokana na kukosa mtu wa kumsomesha ikiwa kwamba siku ya tukio alirubuniwa na jirani huyo.

Alisema kutokana na shida alizokuwa nazo alilazimika kuongozana na jirani yake,mpaka walipofika kwenye nyumba moja pale ulumi alielezwa abakie nje kwanza huku yeye aingie ndani,baada ya muda mfupi alishtukia mwenyeji wake anakamatwa akiwa anapokea fedha.

Akitoa hukumu hiyo Mugissa alisema kutokana na upande wa mashtaka umethibitishwa pasipo kuacha shaka kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kwa vile vitendo vya wananchi kuwauza,pamoja na kuwasafirisha watoto kwa lengo la kuwatumikisha kazi ngumu vimeshamiri,ile hali akititoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa mshtakiwa mwenyewe na wengine wenye tabia kama hizo tayari ameanza kutumikia kifungo kwa kukosa fedha za kulipa faini.

MNADA BANNER