REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

2 CHAINZ: MIE NI MTU MZIMA/ MSINIKAGUE KIJINGA.

7:17:00 AM Add Comment

  Na Hezron Munis  
RAPPER 2 CHAINS hakufurahishwa na Ukaguzi aliofanyiwa alipokuwa Airport Nchini Dubai huku akidai nkuwa umepitiliza na kumkwa yeye kama mtu mzima ambaye anastahili kuheshimiwa

Tukio limetokea Hivi karibuni ambapo 2 Chainz anadai kuwa, hakukataa kukaguliwa, lakini ule Ukaguzi ulizidi kiwango kiasi kwamba akahisi kusumbuliwa na hata kuingiliwa katika uhuru wake hasa mahali ambapo watu wengine wa kawaida hawakustahili kufika

  PICHA LIKO HIVI     
Kwa Mujibu wa Malalamiko ya 2 Chainz kupitia Instagram account yake, anadai kuwa Wahusika wa ukaguzi katika Airport hiyo, walimkagua mpaka mifukoni mwake na hata katika Begi lake Binafsi wakidhani kuwa huenda amebeba "Bangi" kitu ambacho yeye asingeweza kufanya kwa sababu anajua sheria nzi Nchi hiyo haziruhusu kabisa utaratibu huo wa Bangi.

Tofauti na hilo, 2 Chainz anadai kuwa, Wakaguzi walifikia mpaka hatua ya "Kumnusa" mikononi mwake ili kuthibitisha kuwa hajavuta kabisa hicho kitu kabla hajafika katika uwanja huo wa ndege.

Aidha Rapper Huyo ameongeza, yeye ni mtu mzima na wala hakuna kinachomzuia kuvuta "Bangi" , lakini isfikie hatua wakamkagua kupita kiasi ilihali yeye anafahamu sheria zote

VERA SIDIKA: HUWA SIPENDI NGUMZUNGUMZIA OTILE BROWN/ SIJUTII CHOCHOTE

6:59:00 AM Add Comment

VERA SIDIKA:Amesema kuwa Huwa hazungumzii Mahusiano yake yaliyopita


Na Baba Juti   

SOCIALITE kutokea Nchini Kenya ambaye pia ni msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, VERA SIDIKA maarufu kama "Queen Vee Bosset" ameweka wazi kuwa hajutii kamwe kuachana na aliyekuwa mpenzi Wake OTILE BROWN

Akifanya mahojiano na Kituo cha Redio cha Milele Kilichopo Nchini Kenya, Vera Sidika ambaye hivi sasa ana mahusiano mapya tayari, amesema kuwa mara nyingi hajutii kitu hata kidogo kwa Otile Brown ambaye hawakuachana vizuri, na ndio maana mara kwa mara huwezi kukuta anamzungumzia.

OTILE BROWN


Vera Sidika ambaye pia ni Mjasiriamali kutoka Nchini Kenya, amesema kuwa mara kadhaa amekuwa akisikia baadhi ya "Madongo" na habari nyingine tofauti kuhusu yeye ambazo Otile amrkuwa akizizungumza juu yake, lakini hawezi kujibu kwa sababu ni Takribani Miaka miwili na Ushee sasa imepita Tangu waachane

Pia ameongeza kuwa, huwa hana tabia ya kuzungumzia mambo ambayo yalishapita na hata kutoweka katika maisha yake, hivyo haoni haja ya kuendelea kumzungumzia mtu kama huyo

Kauli hiyo ya Vera Sidika ambaye hivi sasa ana mahusiano ya Kimapenzi na Msanii kutoka Nchini Tanzania JIMMY CHANSA, imetoka baada ya Otile Brown kutembelea Nchini Tanzania na kudai kuwa kuna baadhi ya mambo ambayo Vera amewahi kumfanyia na hawezi kuyasahau.

Msikilize Hapa
CHANZO: Milele FM-KENYA

MWANDISHI WA HABARI ASIMAMISHWA KAZI KWA KUPOST TUHUMA ZA UBAKAJI ZILIZOKUWA ZIKIMUANDAMA KOBE BRYANT

6:34:00 AM Add Comment

  Na Hezron Munisi   
GAZETI la Washington Post linalochapisha Taarifa za kila Siku kupitia machapisho yake Nchini Marekani, limemsimamisha Kazi mwandishi wake wa Habari kwa kitendo cha "Kutweet" taarifa za Unyanyaaji wa kijinsia kupitia Ubakaji alizowahi kutuhumiwa Marehemu KOBE BRYANT mnamo mwaka 2016

FELICIA SONMEZ alipost "Link" a,bayo ilichapishwa mwaka 2016 kuhusu tuhuma hizo zilizokuwa zikielekezwa kwa Mkongwe huyo wa mpira wa kikapu katika Ligi ya NBA katika kipindi ambacho Mataifa mewngi na wadau wengi wa Marehemu Kobe Bryant wakiwa katika majonzi mazito.

FELICIA SONMEZ: Amesimamishwa Kazi Baada ya Kutweet Kuhus Tuhuma za Ubakaji zilizokuwa zikimuandama Marehemu Kobe Bryan



Uongozi wa Gazeti hilo la Washington Post, umedai kuwa, haikuwa sawa kabisa kwa mwandishi huyo wa Habari kupost kitu kama hicho katika kipindi hiki kigumu hasa kwa familia ambayo mpaka hivi sasa bado ipo katika majonzi makubwa ya Kumpoteza Kobe Bryan na Binti yake Gianna Bryant katika Ajali mbaya ya Helcopter

"Badala ya Kumlinda na kuendelea kumuunga Mkono mwanahabari katika Sura ya Udhalilishaji, Uongozi umemsimamisha kwa kumpa likizo ya Lazima" Barua kutoka katika Idara ya Uhalili ya Gazeti hilo ilinukuliwa hivyo

Tweet Aliyopost Mwandishi Huyo


Felicia Sonmez alitweet taarifa hiyo ambayo ilikuwa ikizungumzia tuhuma za Ubakaji zilizokuwa zikimuhusu Marehemu Kobe Bryant mnamo mwaka 2003, ambazo zilitia Doa kubwa katika Shughuli zake. Tuhuma hizo za ubakaji zilikuwa zikidai kuwa Marehemu Kobe alimbaka Mchezaji mwenzake wa kike aliyekuwa na Umri wa miaka 19 katika Kipindi hicho.

Hata hivyo mwandishi huyo aliondoa Tweet hiyo baada ya kuandamwa sana, huku akidai kuwa alianza kutishiwa kuuwa na baadhi ya watu


AMBER LULU : “MNATAKA NICHEKE CHEKE TU?”

6:14:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
#WatuWaMungu Malkia wa “Watakoma” Amber Lulu kuna namna ambavyo akiongea ama kuandika chochote katika Social Network accounts zake, lazima utajua tu kuwa kuna jambo “Limemvuruga”

Na hii inatokana na kile ambacho ameamua kukivunjia ukimya Baada ya waungwana wengi kuanza kumuandama kuwa ni kwanini amemficha “Chalii” ambaye inaaminika ndiye Mpenzi wake Mpya baada ya kutokuonekana akijihusisha na Mahusiano ypoyote ya kimapenzi kwa muda sasa

Sasa, Amber lulu ambaye hivi sasa anasukuma vizuri katika Game la muziki wa bongo Flava kupitia Track yake mpya ya “HATERS” , ameamua kuwafyatukia waungwana wanaopenda kutokumuona akipost mahusiano yake kuwa ni kwanini wanataka awe ni mtu wa kucheka cheka tu, na wala hawafurahii yeye kuwa katika mahusiano yake
 ' Ivi nyie mbona watu mnapenda kuwapangia watu maisha yao mnataka nianze kucheka cheka ovyo mana nyege zikizidi ndo nakoelekea nimekaa muda bila mahusiano so vyovyote ndo uyoo shemeji yenu mtake msitake imeishaa iyoooo ….size yangu '



TAARIFA: HUU NDIO UFAFANUZI WA RAPPER PREZZO KUHUSU KUBAKWA

5:53:00 AM Add Comment

 Na Hezron Munisi  

#WatuWaMungu kama utakuwa umetembea katika mitandao kadhaa ya Kijamii, utakuwa unafahamu vizuri kuhusu taarifa za Msanii kutoka Nchini Kenya, PREZZO kuwa amepelekwa Hospitali baada ya Kubakwa na Wanawake Watatu Nchini Humo

Taarifa hizo zimeibuka hivi karibuni kuwa Hitmaker huyo wa “PREZZO” kutoka katika Mitandao miwili kutoka Nchini UGANDA na Mwingine kutoka Nchini TANZANIA , kuwa Rapper huyo amefanyiwa tukio hilo baada ya kuwekewa madawa ya Kulevya aina ya COCAINE.

Tofauti na hilo, pia mitandao hiyo imefafanua kuwa, Prezzo hakuwekewa Dawa za Kulevya tu, bali hata zile za kuongeza nguvu za kiume aina ya VIAGRA, kitu ambacho yeye mwenyewe amekikanusha na kuongeza kuwa hakuna kitu kama hicho na wala hayuko hiospitali

Tunamnukuu
“ Niko salama kabisa, na wala sipo hospitali. Taarifa hiyo ni Uwongo Mtupu na imetengenezwa na watu ambao wana mpango wa kuharibu jina Langu”



Katika hatua Nyingine, Pia Prezzo amesema kuwa hiyo ni sehemu ya Njama za kutaka kumuondoa katika Malengo yake ya kugombea katika uchaguzi wa mwaka 2022

“ Ukikaa Mbali na watu, huwa wanatafuta aina ya taarifa za Uwongo kuzungumza kuhusu wewe. Nimejikita katika Mlengo wa Kisiasa hivi sasa. Nina uhakika wa Asilimia MIA MOJA NA KUMI kuwa nitawatumikia Wananchi wa Kenya 2022”

#BAABEKI !!: NELLY ANATAKA ALIYEMSINGIZIA KWA KESI YA UNYANYASAJI WA KINGONO AJITOKEZE HADHARANI !!!!!

12:33:00 AM Add Comment

Na Rich Sam 
#WatuWaMungu yule Hitmaker wa Mkwaju wa "Dilemma" , NELLY, bado hajaridhika kabisa na kitendo cha Bibie aliyemsingizia na kumfungulia kesi ya Unyanyasaji wa Kingono, aendelee kujificha, anatakiwa kujitokeza.

JANE DOE, ndiye mwanamke ambaye Mwezi November 2018 aliushangaza ulimwengu kwa kumfungulia Mashtaka Rapper Nelly, akidai kuwa msanii huyo alimdhalilisha kijinsia mnamo mwaka 2017 katika Tamasha ambalo lilifanyika Nchini Uingereza, na Nelly alikuwa ni msanii ambaye alikuwa akishusha show yake katika jukwaa hilo

Katika maelezo yake, Jane alidai kwamba alielekea upande wa "BACKSTAGE" kwa ajili ya kumuona Rapper huyo na kusalimiana nae, lakini alipofika pale, alishangaa kumuona Nelly akianza kumshawishi kingono, kisha akaanza kujichua uume wake, na kisha akamlazimisha JANE kufungua mdomo wake ili Nelly amalizie haja yake kwa  njia ya mdomo

Aidha, Mlalamikaji anadai kuwa, awali hakutoa taarifa kuhusu tukio hilo kutokana na kuwa na hofu kama Jeshi la Polisi lingemuamini.

Sasa Basi, January 24, Rapper Nelly ameiomba mahakama kufutilia mbali mashtaka na malalamiko ya mwanamke huyo, huku akisihi mahakama imuamuru mwanamke huyo kujitokeza mbele ya umma ili watu wamfahamu, pengine huenda ukapatikana ushahidi imara zaidi.


KUTANA NA KASHFA NYINGINE KUHUSU MTANDAO WA FACEBOOK..SAFARI HII NI "UBAGUZI"

1:20:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
MTANDAO wa Facebook umekutana na tuhuma nyingine za kutoa matangazo ya ajira ambayo kwa asilimia kubwa yamekuwa yakionekana kuwa na ubaguzi wa “kijinsia”

Kwa mujibu wa mashtaka hayo mapya yaliyofunguliwa na Taasisis mbili ambazo ni ACLU na  Equal Employment Opportunity Commission, inasemekana kuwa Matangazo mengi ya ajira ambayo huwa yanapostiwa Facebook, yamekuwa yakikiuka Haki za Ajira kwa sababu Waajiri wengi huonekana kupendekeza na kutangaza nafasi za kazi kwa jinsia ya kiume tu na sio ya kike kwa wingi

Aidha, Pia Taasisis hizo zimeweka wazi orodha ya Waajiri/Makampuni 10 ambayo yamekuwa yakitoa nafasi za kazi kibaguzi hasa wanawake wakiwa ndio waathirika wakubwa.

Makampuni ama waajiri 10 ambao wametajwa kutangaza nafasi za kazi zenye ubaguzi wa kijinsia katika Mtandao wa Facebook ni pamoja na Abas USA, Defenders, Nebraska Furniture Mart, City of Greensboro North Carolina, Need Work Today, Renewal by Andersen LLC, Rice Tire, JK Moving Services, Enhanced Roofing & Modeling and Xenith.

Uongozi wa Mtandao wa Facebook umeweka wazi kuwa, wao kama njia ya kuunganisha watu wote ulimwenguni katika suala la mawasiliano, hajaruhusu na wala hawakubaliani na “Ubaguzi” wa aina yoyote katika mtandao huo, na wako tayari kufuatilia kile kinachodaiwa  ili wachukue hatua haraka iwezekanavyo

REDSAN KAFANYA FUJO...TAARIFA HII HAPA

3:37:00 AM 1 Comment

Na Baba Juti
MAPEMA asubuhi ya leo, taarifa zimefikishwa katika dawati la "Hit Zone" kuhus kitendo cha Producer SAPPY kutoka jijini Mwanza ambaye muda mwingi hufanya kazi zake Nchini Kenya, kuvamiwa na kujeruhiwa akiwa studio kwake Nchini Humo

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka kwa ERVIX ambaye pia ni Msanii kutoka nchini Tanzania anayefanya kazi Nchini humo chini ya SAPPY MUSIC LAB inayomilikiwa na Producer Sappy, tukio hilo limetokea Siku ya jana na Vurugu hizo ziliznzishwa na msanii nguli kutoka nchini Kenya, REDSAN.

Msanii huyo amezidi kueleza kuwa, chanzo cha ugomvi huo, ni kitendo cha wao (Ervix na Sappy) kutokuhudhuria katika Uzinduzi wa Album ya REDSAN ilihali Sappy ndiye aliyeproduce nyimbo nyingi zinzopatikana katika Album hiyo.

Sababu ambazo ziliwafanya wawili hao kutokuhudhuria katika Uzinduzi huo, ni pamoja na Sappy kupata safari ya kikazi Mombasa, kutokuelewa mustakabali wa faida ambayo ataiapata sababu ameproduce nyimbo kadhaa na hajui atanufaika vipi maana nyimbo iliyolipiwa ni moja, Ervix kutokuhudhuria katika Shughuli hiyo sababu ya mizunguko ya hapa na pale....

SIKILIZA sauti ya ERVIX

SUBIRI KWANZA !!!!! : JUSTIN BIEBER NA HAILEY BALDWIN WAMEFUNGA NDOA TAYARI?

2:57:00 AM Add Comment

Na Hezroni Munisi  
WATU WA MUNGU inawezekana kabisa kuwa Justin Bieber na Mchumba wake HAILEY BALDWIN wakawa wameshafunga ndoa "Kimya Kimya" ?

Kipindi cha nyuma kidogo, taarifa zilikuwa zimeshaenea kabisa kuwa Justin Bieber ambaye awali alikuwa katika mahusiano na Selena Gomez, amezama kwa bibie huyo ambaye anatokea katika familia ya watu maarufu hapa ulimwenguni.

Sasa baada ya kutokuambiwa Ndoa ya wawili hao ni lini, huku wao wakificha licha ya kwamba wameshavalishana pete ya Uchumba, hatimaye Mjomba wa Hailey Baldwin, muigizaji ALEC BALDWIN amejikuta akitoa taarifa ambayo inashabiliana kabisa na wawili hao kufunga Ndoa tayari na ilikuwa ni ya Siri haswa

Akiwa katika upande wa "Red Carpet" kunako Tuzo za EMMYS (Emmys Awards 2018), Alec ambaye ni Mjomba wa Hailey alisema kuwa wamefunga ndo ya Haraka na ya siri kwa asilimia kubwa kwa sababu kwao , suala zima la ndoa, ndicho kitu ambacho wamekuwa wakikitamani muda mrefu na kitawaunganisha na kuwapa Furaha

"Kilichotokea mahakamani, ni kitu cha mahakamani na ni suala la kisheria. Ila Ndoa, ni pale ambapo watu wawili wanaweka wakfu mbele ya mwenyezi mungu na watu wanaowapenda...."
alisema Mjomba mtu

RAPPER WALE AZUIWA KUKAA KATIKA DARAJA LA KWANZA KWENYE NDEGE YA AMERICAN AIRLINES

2:10:00 AM Add Comment




Na Rich Sam
WAKATI mataifa mengi na wananchi wengi ndani ya mataifa hayo yakiendelea kupinga kabisa kitu kinachoitwa "UBAGUZI WA RANGI" safari hii huenda mambo yakawa magumu haswa kwa shirika la ndege Nchini Marekani (American Airlines) baada ya kulalamikiwa kwa mara nyingine tena

RAPPER Kutoka Nchini humo ambaye asili yake ni Nigeria Barani Afrika, WALE, ametoa kilio chake kup[itia account yake ya Twitter kwa madai kuwa alifanyiwa ubaguzi wa Rangi baada ya baadhi ya Wahudumu kumwambia kuwa hakustahili na hana hadhi ya kukukaa katika daraja la kwanza ndani ya ndege hiyo

Tukio hilo limetokea hivi karibuni ikiwa ni baada ya Wale kulalamika kuwa alikuwa amekata Ticketi ambayo ni sahihi na alitakiwa kukaa katika Seat yake sahihi kabisa, lakini baadaye alizuiwa kuingia katika daraja hilo kwa Takriban dakika 30 mpaka 45, na kisha baadaye safari yake kuahirishwa


Wale ambaye ni "member" wa MMG, kundi ambalo liko chini ya Rapper Rick Ross, aliona hana budi kulalamika kupitia Twitter huku akiripoti kuwa ataenda kuwashtaki polisi kwa kitendo hicho

"Vipi kuhusu wafanyakazi wenu MEGUUMI na DON waliponiambia kuwa sitakiwi kuwa katika Daraja la Kwanza?... ninawapigia Polisi" alilalamika hivyo Wale

Ukiachilia mbali Twitter hiyo, Wale alidirikikuhoji ni hatua gani zitachukuliwa zidi ya wafanyakazi hao wawili

"Nyie nyote ni wabaguzi wa Rangi. Ninataka kujua ni hatua gani itachukuliwa. MEGUUN na DON ndio majina yao"



TAYARI !!!!!! : FLOYD MAYWEATHER JR NATARAJIA KUPATA MTOTO NA MREMBO HUYU !!!!

1:37:00 AM Add Comment

Na Rich Sam 
#WatuWaMungu Mzinga wa Heshima kwa Floyd Mayweather Jr, mwanamasumbwi mstaafu aliyejivunia mkwanja mrefuu sana kupitia "Kupigana Makonde" na mahasimu wake mbali mbali.

Sasa Mzinga wenyewe Wa Heshima ni Upi, Ni Mara baada ya kugundua kuwa, Mama of The Mamas ambaye anafahamika kwa jina la JENN DURAN ameweka hadharani kuwa anatarajia kupata Mtoto ambaye inasadikika kuwa ni wa Floyd Mayweather Jr

Taarifa hizo zilinyakwa moja kwa moja kutoka katika account ya Instagram ya Mrembo huyo ambaye hivi sasa ndiye "anatinduana" na Bondia Huyo mwenye Mihela kibao

JENN DURAN alipost Video Clip ambayo ilikuwa ikimuonesha akishika Ujauzito wake huo, huku akiandika na kuweka wazi kuwa, kuwa na hicho kitu ni Baraka za Dhati kutka kwake Mwenyezi Mungu.
A post shared by Jennifer (@iamjenduran) on

MUNGU OKOA JAHAZI !!!! : HUYU NDIYE RAPPER WA KIKE ALIYEKULA PINGU KWA KUIBA KUPITIA INSTAGRAM !!!!

2:54:00 AM Add Comment

Na Hezroni Munisi  
#WatuWaMungu kumbe bado kuna masuala ya kuibiana bado kupitia Instagram na watu bado wanapumbazika kabisa hivi hivi !!!!

Sasa , Soko la Muziki wa Hip Hop hasa kwa upande wa "Wachanaji" wa Jinsia ya Kike, limeingiwa na ka-dosari ambako wakikachukulia poa katakuja kuwaaibisha

Rapper ambaye amejipatia Umaarufu kupitia Instagram, wengine mnasemaga "Instagram Rapper", anayefahamika kwa jina la YOUNG ASH, amejikuta akiramba Pingu bila matarajio baada ya kubainika kuwa amekuwa akiwaibia Followers wake zaidi ya 360,000 kupitia card ya Benki ambayo ni Feki

Picha Liko Vipi sasa Wazee wa Kazi !!!!!
Young Ash ambaye ameachia Tracks kadha wa kadha ikiwemo PRETY AGAIN, RIDE OR DIE, LETTING YOU GO na nyinginezo kibao, amekuwa akitoa taarifa za uwongo kwa baadhi ya Watu na wale ambao wangeingiwa na mioyo ya Huruma, basi wangesalimisha pesa na hata kujikuta wakitoa taarifa zao nyingi sana za Kibenki.


Pia inasadikika kuwa, Kumekuwa na jengo lililojificha huko huko Nchini Marekani, ambalo lina vifaa mbali mbali , ambalo hupokea taarifa hizo na ndani ya Dakika Moja tu vijana hukomba kila kitu kutoka kwenye account zao za Bank

Ingawa yeye kwa upande wake amekanusha kashfa hizo kupitia Instagram account yake YOUNG ASH MUSIC, ila polisi bado wanashughulikia madai hayo ya walioibiwa

ETI NINI !? : MZAZI MWENZAKE NA RAPPER FUTURE ATAMANI AMRUDISHIE MBEGU ZAKE ZA KIUME

2:37:00 AM Add Comment

Na Rich Sam 
Wahenga walisema, "NINGEJUA HUJA BAADA YA......" na hiki ndicho ambacho inabidi ukifahamu hivi sasa ili baadaye usije ukajuta hata kidogo

Wiki Hii imekuwa na Matukio ya aina mbali mbali, lakini hili la Rapper FUTURE na Mzazi mwenzake Brittni, lilichukua nafasi ya aina yake ikiwa ni kitu kinachotafsiriwa kuwa ni "Wivu uliokithiri kwa mtu ambaye unajua ni Kicheche ama ni Msaliti ama ni Mchepukaji maridadi kuliko Kawaida"

Hii ilitokea baada ya Future kubainika kuwa alionekana akichepuka na mmoja kati ya Mabinti alipokuwa ameenda kwenye "kimeo" chake huko Nchini Canada kwa ajili ya kupiga mkwanja, na hii ilinaswa na mapaparazi na wadakuzi wa mambo na hatimaye kuanza kusafirisha Picha kadha wa kadha za Future na Mrembo huyo kunako mitandao ya Kijamii...

Sasa, Hali imeonekana kuwa Ngumu kupita maelezo, maana maumivu ya Wivu yanazidi kumtafuna sana Brittni, Mama wa PRINCE ambaye alimzaa na Hitmaker huyo wa MASK OFF, pengine alidanganywa danganywa na bata la siku ile.

Safari Hii Brittni amefikia hatua ya kujuta na hata kutamani kuzirudisha Mbegu za Kiume za Future ambazo hazina nidhamu katika maisha yake licha ya kwamba tayari keshapata naye mtoto.

Kukazia Zaidi, Brittni ambaye hivi sasa ameweka wazi kuwa Yuko Single, amedai kuwa anajuta kupata mtoto kabla hajafunga Ndoa ama hajaolewa, ahadi ambayo alipewa na Rapper Huyo, namnukuu

" Ninataka Yule atakayemjali mwanamke kama mwanamke bila chenga chenga za huku na kule, na sifanyi hili kwa ajili ya kuweka kitu sawa zaidi kuhitaji Hilo nililoanza nalo"

Bibie huyu hakuishia hapo, bali aliamua kutoa ushauri kwa mabinti ama wanawake wengine hasa akitumia uzoefu wa kile alichopitia...namnukuu

"Msizae watoto mpaka mtakapofunga Ndoa!"


SHIKILIA HAPO HAPOOO !!!!! : LICHA YA KUCHEPUKA KWA RAPPER T.I, MKE WAKE HATOMUACHA NG'O !!!!

2:34:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
#WatuWaMungu tunaomba "Mshikilie Hapo Hapooooo "
Kama wewe umeamua kukata tamaa juu ya yule uliye naye kisa amekusaliti, basi unaweza kujikuta unakata tamaa katika kila kitu ambacho kitakuzingua hapo Mbeleni

Wiki Kadhaa zilizopita, Ilikuja kuvuja kuwa Rapper T.I ameonekana akimshika "Tamnye" mmoja kati ya mabinti ambaye anasadikiwa "kutinduana naye kiwizi wizi" walipokuwa Back Stage, hali iliyozua utata katika Ndoa yake na Mke wake wa Muda Mrefu sana, Tameka a.k.a TINY.

Pia baada ya hilo "Ngenje (Noma)" kuchukua nafasi kubwa sana na kuzagaa kunako Mitaa ya Social Networks, ilikuja kubainika kuwa Tiny amechukia haswa na hata kushea kunako Account yake ya Instagram Clip ya Snoop Dog Doggy akizungumzia namna ambavyo mwanaume anatakiwa kumheshimu mkewe, dongo ambalo lilielekezwa moja kwa moja kwa T.I.

Sasa, baada ya mengi kuzungumzwa, haya na yale kusemwa, hiki na kile kutabiliwa, hili na lile kuchambuliwa, hatimaye Mke wa ndoa kasema kuwa, HABANDUKI, HALEGEZI , HACHOMOI na wala HAACHII kwa Rapper Huyo.

Kupitia Instagram Story yake, Tinny amedai kuwa ataendelea "kushikilia" kama kote katika ndoa yake licha ya kwamba mumewe ni mchepukaji kimtindo

Nanukuu
"Unapotaka kukata tamaa (Katika Ndoto zako, kipaji chako, Ndoa yako, watoto, familia, Kazi, Mungu, Ukristo, katika dhamira yako ama kila kitu unachotaka kukatia tamaa) kumbuka na kwanini ulikianza"

NGOJA KWANZA !!!!! : KUMBE EX MANAGER WA CARD B NDIYE ALIYEMTAFUTIA MENO MAPYA NA KUMFUNGULIA ACCOUNT YA KWANZA YA BANK?..SHABAAAAASH !!!!

2:21:00 AM Add Comment

Na Hezron Munisi 
KABLA ya Yote, "Mzinga Wa Heshima" kwa the baddest Female Rapper Card B kwa Kupata mtoto wa Kike mwenye afya ya kutosha.

Lakini Waungwana bwana, Hata kama Umepata Furaha ya kupongezwa na Mamilioni ya watu, bado kama tunakudai chetu, tutaendelea kukudai tu Mtu wa Mungu.

Kama utakuwa unakumbuka Vizuri, Tuliwahi kuwahabarisha kabisa kuwa Rapper huyo wa kike na Manager wake wa awali walifikishana mahakamani kwa madai kuwa Card B anatakiwa kumlipa kiasi fulani cha fedha kutokana na kuwa yeye ndiye alimpatia Umaarufu na kumsaidia katika mambo mengi kama yote

Sasa Ex- Manager huyo , Klenord “Shaft” Raphael ambaye amefungua mashtaka ya kulipwa USD Milioni 10 na Rapper huyo , amedai kuwa yeye ndiye aliyemtengenezea Card B Meno na kuwa na muonekano mzuri tofauti na yale ya awali yaliyokuwa yakimpa tabu kuongea fresh na hata kuwa na muonekano Mzuri.

Ukiachilia mbali Madai hayo, Pia Manager huyo wa zamani, amedai kuwa, yeye ndiye aliyemfungulia account ya kwanza kabisa ya Bank hit Maker huyo wa BE CAREFUL na hata kumtafutia mjengo wa kwanza kwa yeye kuishi


KIMENUKA !!!!! : KILICHOTOKEA KATIKA UGOMVI WA RIHANNA NA BOYFRIEND WAKE BILIONEA....

2:08:00 AM Add Comment

Na Rich Sam....     
#WatuWaMungu Shabaaaaaaaaaaaaaaash
Kila Kitu huwa kinaenda Vizuri lakini kama ikitokea Dosari katika safari yake, lazima mambo yawe Magumu kidogo, na hii ndiyo tafsiri ya kile kilichotokea Hivi Karibuni

Taarifa za Umbea ambazo wengi hatukuzitilia maanani, zilikuwa ni zile ambazo zilifumuka kuwa hatimaye Mahaba yaliyotishia Dunia, kati ya mamito Robbin Fenty-RIHANNA na Boyfriend wake mwenye Mkwanja Mrefu sana, Hassan Jameel, yamefikia mwisho !!

lakini baadae taarifa Nyingine zikaibuka kuwa wawili hao hawajapigana Chini hata kidogo na mahaba still yapo, lakini kuna jambo ambalo si sawa baina yao kiasi kwamba kichambo kikamuhusu bwana Jameel

Picha ambazo zinaendelea kusambaa kunako kimtaa ya Social Networks, ni kwamba kulikuwa na "Msuguano Heavy" baina ya Wawili hao kutokana na kile kilichoonekana Rihanna kufoka na kumsonta kwa hasira Boyfriend Wake, huku Boyfriend wake akionekana kufafanua jambo, na kisha kuondoka eneo la tukio akiwa ni mwingi wa hasira
A post shared by badgalriri (@badgalriri) on
Sasa, Baada ya kutapakaa kwa Picha Hizo, Rihanna aliamua kuingia kunako Instagram account Yake na kupost picha inayomuonesha SIMBA JIKE akimuungurumia Simba Dume ambaye alionekana kutia Uwoga na kuandika

"Pale unapodhani unajua sana kuhusu Soccer"

Ukiachilia mbali suala hilo, Pia Rihanna alionekana kukwazwa sana na Comments za baadhi ya watu kudai kuwa Rihanna huwachoka mapema ma-ex wake na kuwasumbua na tabia zake kisha huachana nao huku wao wakiishia kuwa na furaha na wanawake wengine

Alipost kitu kilichosomeka hivi:

"Hakuna hata mmoja wa Ma-ex wangu waliooa au kuwa na mahusiano yenye furaha. Hivyo ni salama kusema kuwa SIKUWA TATIZO"

Ukiachilia mbali hayo yote, inasemekana kuwa Ugomvi wa Rihanna na Hassan Jameel ulitokana na baadhi ya vitendo vya Rihanna kuendekeza kukubaliwa katika kila jambo ambalo analifanya, kitu ambacho Hassan Jameel hakufurahishwa nacho

MZINGA WA HESHIMA!!!!! : RICK ROSS ANATARAJIA KUPATA MTOTO WA 4

2:39:00 AM Add Comment

Na Hezron Munisi  
#WatuWaMungu Eeh !!!!!...... "Mzinga Wa Heshima" kwa Rapper Rick Ross kama hii itakuwa ni Taarifa ya ukweli kuhusu jambo hili la Neema kama ambavyo tumeliona.

Rapper Rick Ross ambaye pia ni "BIG BAWSE" wa MayBach Music Group (MMG)  huenda akawa anatarajia kupata mtoto wa nne kutoka kwa bibie ambaye ni mwanamitindo na mtaalamu wa mazoezi ya Viungo , BRIANA CAMILLE.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri, Briana Camille ni mama wa Moto wa Tatu wa Rick Ross ambaye anaitwa BERKELEY ambaye hivi sasa ana umri wa Mwaka mmoja.

Kitu ambacho kilitufanya tuamini kuwa Rozay anatarajia kupata mtoto mwingine, ni baada ya Briana ambaye ni Mpenzi wa Rick Ross kupost Picha Instagram akiwa na mtoto wake Huyo wa Mwaka mmoja, huku Tumbo likiwa limeshiba haswa, na ujauzito kuonekana kuwa Mkubwa kabisa


Ingawa mpaka hivi sasa hawajaweka wazi kuhusu suala hilo, lakini siku zote pembe la Ng'ombe huwa liko nje nje, yaani halifichiki

Tayari Rick Ross ana watoto wengine wawwili Njee aliowapata katika mahusianop ya kipindi cha Nyuma, ambao ni TOIE ROBERTS na WILLIAM ROBERTS III

KIMENUKA !!!!!! : "NIMEMBLOCK REMY MA"- 50 CENTS

1:58:00 AM Add Comment

Na Rich Sam  
#WatuWaMungu hii inaweza kuwa ni SHABAAAAAAAASH kwa hiki ambacho kinaendelea hasa kwa upande wa Rapper Nguli na Mkongwe 50 Cents

Sasa, kama ulikuwa Hufahamu, 50 Cents amechukua uamuzi wa Kum-block Remy Ma (Ambaye Pia ni Rapper wa Kike) kwa madai kuwa anatakiwa kumrekebisha mumewe kuwa na nidhamu na hata kufahamu namna ya kujibu watu wakubwa kwake

Timbwili lilianzishwa na Post ya 50 Cents kunako account yake ya Instagram kwa kumpost Remy Ma na kusema kuwa Female Rapper huyo amekuwa mwembamba, kisha akasema "Hey Kimbao mbao", kitu ambacho hakikumuingia akilini hata kidogo Mume wa Remy Ma, PAPOOSE ambaye hakuona ugumu kutoa Dongo lake

Papoose alicomment hivi
 "Aisee, Daphne Joy (ambaye ni Mpenzi wa 50 Cents Muda mrefu sasa), hakuna harufu ya ndoa Bado?. Kama 50 Cents hatokuoa, nitakutambulisha kwa Mshkaji wangu. Ni Mtu Mzima na anaonekana kukua zaidi...!"

Kitendo hicho kilionekana kumkwaza sana 50 Cents na kudai kuwa ameamua kumblock Remy ma kwa sababu anatakiwa kumuelimisha mumewe

Namnukuu
Remy ameblokiwa mpaka atakapofanya utaratibu wa kumuweka sawa Mumewe. Nilichokisema ni kwamba amepungua uzito, na Papoose akaanza kuzingua. Singombani na mtu hapa juu ya mke wake"

JULY 11: WORLD POPULATION DAY

1:27:00 AM Add Comment





Days Of The Year   

Every year the world continues to get more and more crowded. While we’ve a tendency to pack ourselves into massive cities, and there are presently still long open stretches of countryside, every year that gets whittled away at more and more. The power and food needs of the world continue to place a greater and greater strain on our ability to meet them, and resources in general are becoming harder and harder to come by. World Population Day comes along each year to remind us that our present rate of population growth is unsustainable, and the present social and logistical issues we are experiencing to meet the demand of that population will only get worse if we don’t do something.
History of World Population Day
In 1987 there was an event called “Five Billion Day”, which recognized when the human population boiled over the 5 billion mark. Since then the United Nations Development Programme has been working to anticipate, support, and offset the needs of a rapidly growing population. The population had been deemed to be growing out of control, and an awareness was being spread about the need for family planning, ways to offset poverty, and the ability to ensure that proper maternal health was observed.

The existing strain of supporting our present population is already causing grievous crimes in the areas of human rights and gender equality. As more people come into an a world that’s already doing a poor job of taking care of its citizens, there are more and more of them coming vulnerable to human rights violations such as human trafficking and child labor. World Population Day reminds us that we are part of an ever growing world, and that to ensure there’s a great future ahead for any of us, there has to be a great future for all of us.

How to celebrate Take Your Webmaster To Lunch Day
Not to start off too personal, but the first thing you can do is make sure that your own family planning schedule is properly taken care of. So many places in the world see an uncontrolled growth in population due to a lack of access of proper preventative measures and poor maternal health monitoring. If you’re lucky enough to not be in those areas, be sure you’re taking advantage of your privileges. While you’re at it, see what you can do to support those areas that don’t have access to these materials, and educate yourself on what we can do to help make the world a better place for all of us.

MKUBWA FELA: "ASLAY MWENYEWE HAJANITAFUTA, SIWEZI KUAMINI MAMBO YA MITANDAONI !!!"

1:53:00 AM Add Comment

Na Rich Sam   
#WatuWaMungu Kuvunjika kwa Mahusiano ya Aslay na Mzazi mwenzake Tessy Abdul Maarufu kama Tessy Chocolate yamekuwa ni moja kati ya mazungumzo makubwa sana kunako mitandao ya kijamii

Hali hiyo imewafanya wengi ambao walikuwa wakifuatyilia na kuenjoy mahusiano ya wawili hao kwa ukaribu, wajiulize maswali mengi vichwani mwao hasa kuhusu sababu kubwa iliyowafanya wawili hao wabwagane chini

Ukiachilia mbali watu wengine kuwa na Maswali, hata aliyekuwa Manager wa Aslay ambaye pia ni kama mlezi kwake, Mkubwa Fella, naye anashindwa kujua ni kipi ambacho kinaendelea kati ya wawili hao kiasi cha kufikia maamuzi hayo ilihali wana mtoto mdogo anayeitwa MOZAH

Katika Suala la kuwapatanisha kama ilivyo kwa Wengine, Mkubwa Fella amedai kuwa yeye mpaka muda huu hajaitwa kutoa ushauri ama kuelezwa tatizo ni nini, hivyo kama ataitwa, basi atafanya hivyo maana hata Aslay mwenyewe hajampigia simu bado

MNADA BANNER