Na Hezron Munis
RAPPER 2 CHAINS hakufurahishwa na Ukaguzi aliofanyiwa alipokuwa Airport Nchini Dubai huku akidai nkuwa umepitiliza na kumkwa yeye kama mtu mzima ambaye anastahili kuheshimiwa
Tukio limetokea Hivi karibuni ambapo 2 Chainz anadai kuwa, hakukataa kukaguliwa, lakini ule Ukaguzi ulizidi kiwango kiasi kwamba akahisi kusumbuliwa na hata kuingiliwa katika uhuru wake hasa mahali ambapo watu wengine wa kawaida hawakustahili kufika
PICHA LIKO HIVI
Kwa Mujibu wa Malalamiko ya 2 Chainz kupitia Instagram account yake, anadai kuwa Wahusika wa ukaguzi katika Airport hiyo, walimkagua mpaka mifukoni mwake na hata katika Begi lake Binafsi wakidhani kuwa huenda amebeba "Bangi" kitu ambacho yeye asingeweza kufanya kwa sababu anajua sheria nzi Nchi hiyo haziruhusu kabisa utaratibu huo wa Bangi.
Tofauti na hilo, 2 Chainz anadai kuwa, Wakaguzi walifikia mpaka hatua ya "Kumnusa" mikononi mwake ili kuthibitisha kuwa hajavuta kabisa hicho kitu kabla hajafika katika uwanja huo wa ndege.
Aidha Rapper Huyo ameongeza, yeye ni mtu mzima na wala hakuna kinachomzuia kuvuta "Bangi" , lakini isfikie hatua wakamkagua kupita kiasi ilihali yeye anafahamu sheria zote
EmoticonEmoticon