Na Hezron Munisi
#WatuWaMungu kama utakuwa umetembea katika mitandao kadhaa
ya Kijamii, utakuwa unafahamu vizuri kuhusu taarifa za Msanii kutoka Nchini
Kenya, PREZZO kuwa amepelekwa Hospitali baada ya Kubakwa na Wanawake Watatu
Nchini Humo
Taarifa hizo zimeibuka hivi karibuni kuwa Hitmaker huyo wa “PREZZO”
kutoka katika Mitandao miwili kutoka Nchini UGANDA na Mwingine kutoka Nchini
TANZANIA , kuwa Rapper huyo amefanyiwa tukio hilo baada ya kuwekewa madawa ya
Kulevya aina ya COCAINE.
Tofauti na hilo, pia mitandao hiyo imefafanua kuwa, Prezzo
hakuwekewa Dawa za Kulevya tu, bali hata zile za kuongeza nguvu za kiume aina
ya VIAGRA, kitu ambacho yeye mwenyewe amekikanusha na kuongeza kuwa hakuna kitu
kama hicho na wala hayuko hiospitali
Tunamnukuu
“ Niko salama kabisa, na wala sipo hospitali. Taarifa hiyo
ni Uwongo Mtupu na imetengenezwa na watu ambao wana mpango wa kuharibu jina
Langu”
Katika hatua Nyingine, Pia Prezzo amesema kuwa hiyo ni
sehemu ya Njama za kutaka kumuondoa katika Malengo yake ya kugombea katika
uchaguzi wa mwaka 2022
“ Ukikaa Mbali na watu, huwa wanatafuta aina ya taarifa za
Uwongo kuzungumza kuhusu wewe. Nimejikita katika Mlengo wa Kisiasa hivi sasa.
Nina uhakika wa Asilimia MIA MOJA NA KUMI kuwa nitawatumikia Wananchi wa Kenya
2022”
EmoticonEmoticon