Na Rich Sam
WAKATI mataifa mengi na wananchi wengi ndani ya mataifa hayo yakiendelea kupinga kabisa kitu kinachoitwa "UBAGUZI WA RANGI" safari hii huenda mambo yakawa magumu haswa kwa shirika la ndege Nchini Marekani (American Airlines) baada ya kulalamikiwa kwa mara nyingine tena
RAPPER Kutoka Nchini humo ambaye asili yake ni Nigeria Barani Afrika, WALE, ametoa kilio chake kup[itia account yake ya Twitter kwa madai kuwa alifanyiwa ubaguzi wa Rangi baada ya baadhi ya Wahudumu kumwambia kuwa hakustahili na hana hadhi ya kukukaa katika daraja la kwanza ndani ya ndege hiyo
Tukio hilo limetokea hivi karibuni ikiwa ni baada ya Wale kulalamika kuwa alikuwa amekata Ticketi ambayo ni sahihi na alitakiwa kukaa katika Seat yake sahihi kabisa, lakini baadaye alizuiwa kuingia katika daraja hilo kwa Takriban dakika 30 mpaka 45, na kisha baadaye safari yake kuahirishwa
Wale ambaye ni "member" wa MMG, kundi ambalo liko chini ya Rapper Rick Ross, aliona hana budi kulalamika kupitia Twitter huku akiripoti kuwa ataenda kuwashtaki polisi kwa kitendo hicho
"Vipi kuhusu wafanyakazi wenu MEGUUMI na DON waliponiambia kuwa sitakiwi kuwa katika Daraja la Kwanza?... ninawapigia Polisi" alilalamika hivyo Wale
Ukiachilia mbali Twitter hiyo, Wale alidirikikuhoji ni hatua gani zitachukuliwa zidi ya wafanyakazi hao wawili
"Nyie nyote ni wabaguzi wa Rangi. Ninataka kujua ni hatua gani itachukuliwa. MEGUUN na DON ndio majina yao"
EmoticonEmoticon