REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

VERA SIDIKA: HUWA SIPENDI NGUMZUNGUMZIA OTILE BROWN/ SIJUTII CHOCHOTE

6:59:00 AM

VERA SIDIKA:Amesema kuwa Huwa hazungumzii Mahusiano yake yaliyopita


Na Baba Juti   

SOCIALITE kutokea Nchini Kenya ambaye pia ni msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, VERA SIDIKA maarufu kama "Queen Vee Bosset" ameweka wazi kuwa hajutii kamwe kuachana na aliyekuwa mpenzi Wake OTILE BROWN

Akifanya mahojiano na Kituo cha Redio cha Milele Kilichopo Nchini Kenya, Vera Sidika ambaye hivi sasa ana mahusiano mapya tayari, amesema kuwa mara nyingi hajutii kitu hata kidogo kwa Otile Brown ambaye hawakuachana vizuri, na ndio maana mara kwa mara huwezi kukuta anamzungumzia.

OTILE BROWN


Vera Sidika ambaye pia ni Mjasiriamali kutoka Nchini Kenya, amesema kuwa mara kadhaa amekuwa akisikia baadhi ya "Madongo" na habari nyingine tofauti kuhusu yeye ambazo Otile amrkuwa akizizungumza juu yake, lakini hawezi kujibu kwa sababu ni Takribani Miaka miwili na Ushee sasa imepita Tangu waachane

Pia ameongeza kuwa, huwa hana tabia ya kuzungumzia mambo ambayo yalishapita na hata kutoweka katika maisha yake, hivyo haoni haja ya kuendelea kumzungumzia mtu kama huyo

Kauli hiyo ya Vera Sidika ambaye hivi sasa ana mahusiano ya Kimapenzi na Msanii kutoka Nchini Tanzania JIMMY CHANSA, imetoka baada ya Otile Brown kutembelea Nchini Tanzania na kudai kuwa kuna baadhi ya mambo ambayo Vera amewahi kumfanyia na hawezi kuyasahau.

Msikilize Hapa
CHANZO: Milele FM-KENYA

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER