REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MWANDISHI WA HABARI ASIMAMISHWA KAZI KWA KUPOST TUHUMA ZA UBAKAJI ZILIZOKUWA ZIKIMUANDAMA KOBE BRYANT

6:34:00 AM

  Na Hezron Munisi   
GAZETI la Washington Post linalochapisha Taarifa za kila Siku kupitia machapisho yake Nchini Marekani, limemsimamisha Kazi mwandishi wake wa Habari kwa kitendo cha "Kutweet" taarifa za Unyanyaaji wa kijinsia kupitia Ubakaji alizowahi kutuhumiwa Marehemu KOBE BRYANT mnamo mwaka 2016

FELICIA SONMEZ alipost "Link" a,bayo ilichapishwa mwaka 2016 kuhusu tuhuma hizo zilizokuwa zikielekezwa kwa Mkongwe huyo wa mpira wa kikapu katika Ligi ya NBA katika kipindi ambacho Mataifa mewngi na wadau wengi wa Marehemu Kobe Bryant wakiwa katika majonzi mazito.

FELICIA SONMEZ: Amesimamishwa Kazi Baada ya Kutweet Kuhus Tuhuma za Ubakaji zilizokuwa zikimuandama Marehemu Kobe Bryan



Uongozi wa Gazeti hilo la Washington Post, umedai kuwa, haikuwa sawa kabisa kwa mwandishi huyo wa Habari kupost kitu kama hicho katika kipindi hiki kigumu hasa kwa familia ambayo mpaka hivi sasa bado ipo katika majonzi makubwa ya Kumpoteza Kobe Bryan na Binti yake Gianna Bryant katika Ajali mbaya ya Helcopter

"Badala ya Kumlinda na kuendelea kumuunga Mkono mwanahabari katika Sura ya Udhalilishaji, Uongozi umemsimamisha kwa kumpa likizo ya Lazima" Barua kutoka katika Idara ya Uhalili ya Gazeti hilo ilinukuliwa hivyo

Tweet Aliyopost Mwandishi Huyo


Felicia Sonmez alitweet taarifa hiyo ambayo ilikuwa ikizungumzia tuhuma za Ubakaji zilizokuwa zikimuhusu Marehemu Kobe Bryant mnamo mwaka 2003, ambazo zilitia Doa kubwa katika Shughuli zake. Tuhuma hizo za ubakaji zilikuwa zikidai kuwa Marehemu Kobe alimbaka Mchezaji mwenzake wa kike aliyekuwa na Umri wa miaka 19 katika Kipindi hicho.

Hata hivyo mwandishi huyo aliondoa Tweet hiyo baada ya kuandamwa sana, huku akidai kuwa alianza kutishiwa kuuwa na baadhi ya watu


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER