REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

SUBIRI KWANZA !!!!! : JUSTIN BIEBER NA HAILEY BALDWIN WAMEFUNGA NDOA TAYARI?

2:57:00 AM

Na Hezroni Munisi  
WATU WA MUNGU inawezekana kabisa kuwa Justin Bieber na Mchumba wake HAILEY BALDWIN wakawa wameshafunga ndoa "Kimya Kimya" ?

Kipindi cha nyuma kidogo, taarifa zilikuwa zimeshaenea kabisa kuwa Justin Bieber ambaye awali alikuwa katika mahusiano na Selena Gomez, amezama kwa bibie huyo ambaye anatokea katika familia ya watu maarufu hapa ulimwenguni.

Sasa baada ya kutokuambiwa Ndoa ya wawili hao ni lini, huku wao wakificha licha ya kwamba wameshavalishana pete ya Uchumba, hatimaye Mjomba wa Hailey Baldwin, muigizaji ALEC BALDWIN amejikuta akitoa taarifa ambayo inashabiliana kabisa na wawili hao kufunga Ndoa tayari na ilikuwa ni ya Siri haswa

Akiwa katika upande wa "Red Carpet" kunako Tuzo za EMMYS (Emmys Awards 2018), Alec ambaye ni Mjomba wa Hailey alisema kuwa wamefunga ndo ya Haraka na ya siri kwa asilimia kubwa kwa sababu kwao , suala zima la ndoa, ndicho kitu ambacho wamekuwa wakikitamani muda mrefu na kitawaunganisha na kuwapa Furaha

"Kilichotokea mahakamani, ni kitu cha mahakamani na ni suala la kisheria. Ila Ndoa, ni pale ambapo watu wawili wanaweka wakfu mbele ya mwenyezi mungu na watu wanaowapenda...."
alisema Mjomba mtu

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER