Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli ameahidi
kununuliwa kwa ndege zingine mbili kubwa kwaajili ya shirika la ndege la
Tanzania, ATCL.
Ametoa kauli hiyo Jumatano hii kwenye uzinduzi wa ndege mbili mpya za
ATCL kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.
Ndege hizo ni aina ya Bombadier Q 400 zimetengenezwa nchini Canada.
Amesema ndege mbili kubwa zikazonunulia hapo baadaye zitakuwa na uwezo
wa kubeba abiria 160 na nyingine kubwa zaidi itakayobeba abiria 240 pamoja na
mizigo yao. Amewahakikishia Watanzania kuwa fedha za kununua ndege hizo zipo.
Kuhusu ndege mbili zilizotua tayari kwa kuanza kazi, Rais Magufuli
amesema serikali ilianza kwa kuzilipia asilimia 40 ya gharama zake na kisha
kumalizia asilimia 60 iliyokuwa imesalia na kwamba zingekuwa na gharama zaidi
kama zingelipiwa kidogo kidogo.
Rais amedai kuwa ndege hizo zina ubora wa uhakika na zinaweza kufanya kazi katika mazingira yoyote. “Nataka niwahikishie watanzania ndege hizi ni mpya, mzitumie kwa kujua ni mali inayotokana na kodi zenu,” alisema.
Ndege hizo zina uwezo wa kubeba abiria abiria 76, 6 wakiwa daraja la juu
na 70 ni daraja la chini.
Pia alitumia fursa hiyo kukanusha madai ya baadhi ya watu kuwa ndege
hizo hazikimbii.
“Natamani huyo aliyesema hazina spidi nimjue nimlipie nauli akae mbele
aone zinavyokata mawingu,” alitania
Kwa upande mwingine Rais
Magufuli amewakumbusha wafanyakazi wa ATCL kufanya kazi kwa weledi na kuepuka
kufanya kimazoea huku wakitambua kuwa kuna ushindani katika sekta hiyo. Pia
ameagiza wasiruhusu mtu yeyote asipande bure hata kama ni viongozi wa nchi
EmoticonEmoticon