Na Dr. Felician Kiyando,
NI DHAHIRI kabisa kuwa Wanawake wanapenda sana kutumia Deodorant kwa ajili ya Manufaa ya Afya zao, na hata maumbile yao Pia
Lakini kwa Wanawake ambao wanatumia Deodorant zenye ALUMINIUM SALTS wanaweza kuwa katika hatari ya kukumbana na Ugonjwa wa Cancer ya Titi, na hii ni kwa Mujibu wa Utafiti ambao umefanyika hivi karibuni, yaani utafiti Mpya
Watafiti kutoka Uswiss wanasema kuwa, matumizi ya Muda Mrefu ya ALUMINIUM CHROLIDE, yanaweza kusababisha kusambaa kwa Cancer katika maeneo mengineyo pia ya Mwili
Ingawa utafiti wa awali, yaani wa zamani uliweka wazi kuwa, matumizi ya Deodorant hizo, ni salama kwa afya ya binadam
Utafiti huu mpya, umefanywa na Chuo cha Geneva, na inasisitizwa kuwa, kuna hatari ya ongezeko la Ugonjwa huu wa Cancer kwa Wanawake hasa wakitumia bidhaa hizi ambazo zinamadini haya ya ALUMINIUM, katika maeneo ya Vikwapa.
Pia utafiti huo unaongeza kuwa, Madini haya ya aluminium, huziba yale matundu yanayoruhusu utoaji wa jasho katika kikwapa kutoka katika tishu za Titi na kutengeneza oestrogen ambazo ni kama athari
EmoticonEmoticon