REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MTANGAZAJI ALIYEACHA KAZI LIVE ILI AKAUZE BANGI, HUENDA AKAFUNGWA MIAKA 24 JELA

11:32:00 PM

CHARLO GREEN, aliamua Kuacha Kazi Ili akajikite zaidi katika Biashara yake ya Kuuza Bangi

Na Baba Juti
KAMA utakuwa ulikuwa hujui, basi inabisdi ufahamu kuanzia hivi sasa, kuwa, kazi zetu hizi sometimes huwa zinz changamoto hasa ukiwa umeajiriwa, halafu una ka biashara kako Kengine kuweza kujikimu japo kimaisha.



CHARLO GREEN, aliyekuwa Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ABC mwaka 2014 kisha akaacha Kazi kwa ajili ya kuuza Bangi, huenda akahukumiwa Miaka 24 pale atakapobainika na kosa.

November 2014, Baada ya Kutangazwa Kuidhinishwa Uvutaji wa Bangi Katika Baadhi ya Majimbo, Charlo Greene aliacha Kazi Miezi Miwili Baadaye


Mwaka 2014, akiwa Live katika TV kupitia Segement yake, CHARLO GREEN aliacha kazi huku wengi wakiwa wanafuatilia kipindi hicho, na kauli yake iliyowashtua wengi ni kusema "F**ck , I Quit" na kisha kuondoka.

Green alidai kuwa, ameamua kuacha kazi ili kujikita zaidi katika Club Yake ya kuuza Bangi- ALASKA CANNABIS CLUB, katika Jimbo hilo la Alaska Nchini Marekani.

Charlo amefunguliwa Mashtaka ya Makosa 8, na Endapo atakutwa na Hatia, basi atatumikia Kifungo cha Miaka 24 Jela


Lakini Kitu cha ajabu ni Kipi, Alaska ni Miongoni mwa Majimbo ambayo yameidhinishwa Kuuza Bangi, lakini Mpaka Kufikia FEBRUARY 2015, Sheria hiyo ndo ikaanza kufanya Kazi Rasmi.

Sasa, Green amekutana na Makosa 8, ambapo katika Club Yake, Polisi walikutana na Bidhaa za Bangi mara kwa Mara, katika Kipindi ambacho Sheria ilikuwa haijaanza kufanya Kazi


HIVI sasa ameanzisha Kampeni ambayo inalenga kumtetea na kumuepusha na Jela

Inasemekana Kuwa Bibie huyo aliychukua Vichwa Vingi vya habari, alipiga Chini Kazi hiyo Miezi Miwili Baada ya NOVEMBER 2014, wakati Tayari Bangi ilikuwa imeshatangazwa kuhalalishwa katika Baadhi ya Majimbo, lakini tangu zamani, Club yake ilikuwa ikifanya Biashara hiyo, yaani kabla haijahalalishwa.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER