Na Baba Juti
SASA majanga Mengine yameibuka, na safari hii mlengwa ni Fetty Wapp !!!!!!!!!!!!!!!!.
Mwandishi na Msanii kutoka Nchini Denmark, LAZAR LAKIC, amesema kuwa amefungua Mashtaka dhidi ya Fetty Wap na Producer Wake Tonny Fadd kwa kutumia Beat yake katika Wimbo wa TRAP QUEEN ambao kila mmoja hawezi kuusahau katika historia ya Muziki wa aina ya Trap.
Lazar anadai kuwa amelipia Beat ya Wimbo Huo Mwaka 2014 na ana haki miliki |
LAZAR amedai kuwa, Miaka Miwili iliyoakata, yaani 2014 alikutana na Producer huyo na kumlipa juu ya haki ya kumilik Beat Hiyo ya Trapp Queen, lakini kwake, ilitumika katika Mzigo wa Hello, na kila kitu kukamilika
Pia Lazar anaongeza kuwa, mnamo Mwaka 2015, alilip[ia tena Beat hiyo ya Tra Queen na bado kubaki katika hakimiliki yake kawaida.
Katika hali ya Kushangaza, Mkwaju huo wa Trap Queen ulianza kusikika 2014 na Lazar anadai hakuwa amefahamu, lakini Mwaka 2015, Mzigo huo ulianza kusikika na kukita Duniani Kote huku ukifika mpaka chati za Juu za Muziki ikiwemo Billboard 100, na Ndipo Lazar akagundua na kushangaa kwanini Beat yake imetumika katika Mkwaju huo ilihali ana Haki za Kumiliki Beat Hiyo.
Naye Mwanasheria wa Fetty Wap, NAVARRO GRAY, amesema kuwa FETTY WAPP hajaiba Beat
hiyo kama inavydaiwa hivi sasa, bali ana Mikataba ya makubaliano na malipo ya Sehemu ya haki ya Wimbo huo.
Lakini kama itatokea Producer kamuingiza Mkengeni, Basi Fetty Wap atatakiwa kulipwa na Producer Fadd kwa usumbufu na uharibifu utakaojitokeza
EmoticonEmoticon