REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

UTAFITI: WANAWAKE WENYE MIAKA YA 40 MPAKA 50 NA...HUFURAHIA TENDO LA NDO KULIKO WENYE MIAKA 20 NA...

12:19:00 AM

Na Baba Juti
UTAFITI mpya Umeibuka kuwa, wanawake ambao wapo katika Umri wa Kati, yaani kuanzia Miaka 40 hivi na kuende mpaka 50 Na Kitu Hufurahia Tendo la Ndoa kuliko Vijana wenye Umri wa Miaka 20 na kuendelea.


Ingawa Mabadiliko ya Kimaumbile  huwafanya wakutane na Ugumu fulani katika mpangilio wa Mapenzi na hata vitu vingine, Watafiti wa UNIVERSITY HOSPITALS CLEVELAND MEDICAL CENTER wanasema kuwa wanawake ambao wako katika Umri huo, huwa na Ujasiri unaoambatana na mbinu mbali mbali za kimapenzi ambazo huwafanya kuboresha Msisimkuo wa Mahusiano ya Kimapenzi

Tofauti na Hilo, wanawake Wenye Umri huo, hufurahia mawasiliano mazuri, na kwa silimia kubwa hufurahia sana sana kuvaa mavazi ya kutamanisha hasa wanapokuwa chumbani tu, hali ambayo huongeza chachu ya kutamanika kwa mwanaume pindi wanapojiandaa kwa Supa Mechi ya Mtinduo.

Watafiti wamefanya mahojiano na Wanawake Zaidi ya 500 walio na Umri wa Miaka kati ya 40 na 75 walioko kwenye mahusiano kuhusu kinachotokea katika Tendo la ndoa linapopungua kwa sababu ya Umri Mkubwa.

Majibu makuu mawili waliyotaja ni pamoja na Kukauka kwa UKE pamoja na kukosa kwa hamu ama kuwa na hofu na Kufanya Tendo la Ndoa

Pia ikabainika kuwa, Wanawake walio na Umri Kati ya Miaka 40 na kuendelea, na wako katika mahusiano na watu wazima wenzao, hukosa "Shibe" ya tendo la ndoa na kuachwa na hamu, jambo ambalo huwafanya wengi wao walio katika idadi ya asilimia 50 hutumia Vifaa vyenye maumbile ya Uume, vinavyotetemesha ili kuwafanya wafurahie.

DR. SHERLY KINGSBERG, ambaye ni mtaalamu aliyebobea katika Matatizo na masuala ya Kitabia, anasema kuwa Utafiti unaonesha kuwa, Ni kweli wanawake wengi walio katika Umri huo, huenjoy tendo la Ndoa na hata kuridhika balaa, lakini Wengi wao, hushindwa kulifurahia sababu ya kutoridhishwa na Wenzi wao ambao labda wanawazidi kiumri au wapo katika Umri mmoja.

DR JOANN PINKERTON, Mkurugenzi wa NAMS ( NORTH AMERICAN MENOPAUSE SOCIETY) amesema kuwa Utafiti huo utawasilishwa katika Mkutano wao Mkuu wa Mwisho wa Mwaka 2016, utakaofanyika Huko ORLANDO Nchini Marekani, OCTOBER 05.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER