Kutangazwa kwa taarifa hiyo kunakuja siku chache baada ya
Tanzania Daima kuandika habari juu ya polisi hao kwa kushirikiana na watendaji
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuunda mtandao wa kihalifu.
Taarifa ya kukamatwa kwa askari hao zilitolewa jana jijini
Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman
Kova.
Kova alisema askari hao wanatuhumiwa kuunda mtandao wa
kukusanya fedha kutoka kwa wafanyabiashara wasiotaka kulipa ushuru wa serikali.
Licha ya kuweka wazi idadi hiyo kamanda Kova aligoma
kuyataja majina ya wahusika bila kuweka wazi kwa nini ameamua kufanya hivyo.
Kova pia alitumia muda huo kuilaumu Tanzania Daima, kwa
kuandika habari za uhalifu huo juzi ikiwa ni baada ya uchunguzi wa zaidi ya
wiki moja tangu kukamatwa kwa askari hao.
Alisema kabla ya gazeti hili kuandika habari hizo kwa mara
ya kwanza mwishoni mwa wiki iliyopita, jeshi hilo lilikuwa limeshawakamata
askari wake wanane kutokana na tukio hilo.
“Si kwa kuwa gazeti moja liliandika na ndiyo tumesukumwa
kuwakamata wahalifu hawa; tulianza taratibu hizi mapema na tukawa tunasubiri
muda muafaka wa kuweka mambo yote hadharani,” alisema Kova.
Hata hivyo Kova jana alishindwa kuweka wazi yalikopelekwa
magari yaliyokamatwa kwenye uhalifu husika.
Wakati akishindwa kutaja kama kuna magari yaliyokamatwa,
baadhi ya askri waliozungumza na gazeti hili wameshangazwa na hatua hiyo na
kumtaka DCP Kova awe mkweli juu ya sakata hilo.
Askari hao wamehoji hatua ya Kova kuwakamata wenzao
walioonekana katika picha za video za mnato na kushindwa kuyakamata magari
yaliyokubali kushiriki katika uhalifu huo.
“Mnapaswa kujiuliza kama askari wameshafika 16 halafu hakuna
gari hata moja lililokamatwa, hao watakuwa wanapelekwa mahakamani kwa ushahidi
wa namna gani na kwa nini hayo magari hayakuweza kuchukuliwa katika hizo picha
au ni siasa za mzee wetu zimewafanya mkashindwa kuhoji hilo?” alisema mmoja wa
askari.
Mtandao huo unadaiwa kufanya kazi kwa takriban miezi sita
kabla ya kujulikana na kuchukuliwa kwa hatua dhidi yao.
Kwa mujibu wa Chanzo cha habari, mbinu inayodaiwa kutumiwa
ni kwa askari hao kuwasaidia wafanyabiashara kuingiza bidhaa kupitia bandari
bubu ya Mbweni, kisha kuzipakia kwenye magari makubwa kwa ajili ya kutawanya
bidhaa hizo katika masoko ya jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya bidhaa zinazodaiwa kuingizwa kwa wingi ni runinga,
redio, pasi za umeme na kompyuta mpakato.
EmoticonEmoticon