FISH KEEP LEFT: Usione Umati huo wa Watu umejaa hapo ukadhani kwenye hilo eneo kuna tukio la Hatari. Hapo kuna sanamu ya SAMAKI,ambaye Wakazi wengi wa Mwanza na Hata Wageni, hupenda kupiga Picha mbele ama Pembeni ya Sanamu hiyo ya Samaki
KAMANGA GARDEN: Hii ni Bustani katika Bara bara ya Kutoka Kamanga kuelekea CAPRIPOINT. Inavutia sana na Inang'aa Muda Wote. Karibu Mwanza
HALIDONDOKI HILO: Moja kati ya Mawe ya Ajabu yanayopatikana ROCK CITY Mwanza. Unaweza dhania linadondoka lakini hulidondoshi hata kwa Greda
RAILWAY STATION: Kwa wale tunaotumia Usafiri wa GOGO (Treni) Kutoka, Dar, Dodoma, Shinyanga, na Hata Kwingineko, Hapa ndo Mwisho wa Reli yetu kwa Jiji la Mwanza
LIKO IMARA HILO: Jiwe ambalo liko karibu na Reli ndani ya Jiji la Mwanza. Mwenyewe unawesza dhania pia kuwa litaidondokea Treni, lakini miaka na Miaka, jiwe hilo halijawahi hata Tikisika
MAGOROFANI: Hii ndio Magorofani ya Mitaa yetu ya Uswahilini. Nyumba zimejengwa juu kwajuu, na Hasa juu ya Jiwe hili na Lingine kama Unavyoona Mwenyewe
KIVUKO: Hiki ni Kivuko kilichopo Kamanga Ferry: PANTONZ haziko Da'slaam Peke ake, hadi huku zipo aisee
MVUTO WA AINA YAKE: Bismarck Rock katika Muonekano wa Karibu.
KARIBU SATO: Utambulisho wa Kitoweo kikuu cha Jiji la Mwanza na Kanda Ya Ziwa
KISIWA: Hiki Ni Kisiwa cha SAA NANE,ambacho pia Ni Hifadhi ya Wanyama Mbali mbali na Kituo cha Utalii hasa kwa Jiji la Mwanza
KUMBUKUMBU: Hii Ni Kumbu Kumbu ya Kihistoria kwa Jiji la Mwanza.
KARIBU MWANZA: Mandhari Yetu Ni Nzuri Sana.
EmoticonEmoticon