Gordon Kalulunga, Mbeya
WAUGUZI nchini wameshauriwa kuacha simu zao katika vyumba
maalumu au kuzizima wakati wanapotoa huduma kwa wagonjwa.
Wito huo ulitolewa juzi na muuguzi mstaafu Andulile
Mwansyange (68) alipokuwa akitoa tofauti ya utumishi wake na uuguzi wa sasa
katika maadhimisho ya Siku ya Uuguzi Tanzania iliyofanyika Mbalizi-Ifisi,
Mbeya.
Mwansyange alisema mjadala unahitajika kuhusu umuhimu wa
wauguzi kutotumia simu za viganjani wakiwa kazini.
“Kuwe na mjadala wa wauguzi kutotumia simu wanapokuwa kwenye
vyumba vya kutolea huduma muhimu pia wagonjwa wafunge simu wanapoingia kwenye
matibabu.
…Unaweza kupigiwa simu ya msiba au kupokea ujumbe wa mtu
anayekuhusu hali inayoweza kusababisha kuacha kutoa huduma kwa mgonjwa,’’
alisema muuguzi huyo mstaafu.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Upendo Sanga,
alisema angekuwa mkufunzi wa wauguzi angewafundisha maadili na watakaoshindwa
angewafukuza uuguzi.
Akisoma risala kwa niaba ya mkurugenzi huyo aliyekuwa mgeni
rasmi, mwanasheria wa wilaya hiyo, Prosper Msivala, alisema suala la matumizi
ya simu kwenye maeneo ya kutolea huduma limekatazwa na lipo kisheria hivyo
halihitaji mjadala.
Naye Muuguzi Mkuu wa hospitali ya Mbalizi Ifisi
inayomilikiwa na kanisa la Uinjilisti Tanzania, Sikitu Mbilinyi, alisema upendo
kwa wagonjwa ni tiba, hivyo umefika wakati kwa kila muuguzi kubadilika.
EmoticonEmoticon