SERENGETI, MARA.
Mkazi mmoja wa kijiji cha Gentamome wilayani Serengeti
mkoani Mara, amejeruhiwa vibaya katika sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya
kushambuliwa na fisi aliyevamia nyumbani kwake.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho cha Gentamome Bw
Elisha Sinda,amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Agosti tisa
mwaka huu.
Amemtaja mwananchi huyo kuwa ni Bw Juma Kurate ambaye mbali
na kujeruhiwa katika sehemu hizo za mwili wake pia fisi hiyo alimnyofoa kidore
gumba cha mkono wake wa kushoto.
Bw Sinda,amesema baada ya fisi huyo kuvamia nyumbani kwa
mwananchi huyo kwa lengo la kukamata mbuzi ndipo walipopambana na makazi huyo
kabla ya kumjeruhi na kukimbia na kidore hicho kabla ya kuuawa katika msako
mkali uliofanywa na wananchi wa kijiji hicho.
Kwa sababu hiyo mwenyekiti huyo wa kijiji,ameiomba idara ya
wanyamapori wilayani Serengeti kuendesha msako dhidi ya fisi hao ambao amesema
wamekuwa kero kubwa kwa wananchi kutokana na kupora kila wakati mifugo ya wananchi
lakini licha ya kutoa taarifa katika idara hiyo hakuna hatua ambazo
zimechukuliwa.
EmoticonEmoticon